Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Policcm sio wa kutegemea

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Mwisho wa siku Idd Amin alitoka madarakani na miaka mingi baadae alikuja kufariki Dunia.

Hii inatufundisha kuwa kila kitu kina mwisho ila ni suala la muda tu.

Get well soon Kamanda Lissu!!
 
Si rahisi kama unavyofikiria. Wauaji hawawezi kukubali kuchunguzwa. Kwa sasa kunahitajika jitihada na mbinu mchanganyiko ili kutoka hapa tulipo. Lakini kwa kutegemea kupewa haki kwenye sahani, tushau kabisa. Haki hutafutwa.

Tundu Lisu anatiimiza wajibu wake bila ya hofu ya maisha yake. Wengine tumefanya nini?
 
Hadithi za primary.... kwa kumezeshwa mabaya ya idd amini toka kwa whites...

Endelea kuwa mtumwa alafu ipo day utagundua amini ni nani na lengo la yoote ilikua nin.

Acha propaganda za primary.
na manyimbo ya mxhakamchaka ya miaka ile hujui lolote ndio umekua nayo.. now unajua hautak kuchambua.

Mi ni mganda by birth niulize nikupe info za ile nchi

Sent from "La -Vista"
Hayo si maoni tu mkuu povu la nn ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si rahisi kama unavyofikiria. Wauaji hawawezi kukubali kuchunguzwa. Kwa sasa kunahitajika jitihada na mbinu mchanganyiko ili kutoka hapa tulipo. Lakini kwa kutegemea kupewa haki kwenye sahani, tushau kabisa. Haki hutafutwa.

Tundu Lisu anatiimiza wajibu wake bila ya hofu ya maisha yake. Wengine tumefanya nini?
well said
 
Taratibu naanza kuiona nchi ikirithi tabia za nchi kama rwanda, Zimbabwe, DRC Congo na nyinginezo ambazo marais wake wanandoto za kutawala mpaka kifo kitakapo wachukua
 
Ujue tuacheni ujanja ujanja waficha na kufunikafunika Mambo,,,,, Hivi kweli kamanda wa Police mwenye nyezo na zana zote za kazi anakuja na hoja nyepesi namna hii!!!!... Nijuavyo mimi Police amefunzwa kukariri Kwa wepesi na haraka zaidi na sio kukariri sura na rangi za magari bali kithibito ambacho Ni namba za usajili.

Nina Swali Kwa RPC alijuaje gari Ni Nissan Nyeupe akashindwa kujua namba za usajili ambazo ziko mbele na nyuma???

Swali la pili; Jana tuliambiwa muda mfupi tu baada ya tukio kuliwekwa vizuizi katika viunga vyote vya Dodoma, Ni vipi hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya kukamatwa Nissani yoyote Nyeupe ili zifanyiwe uchunguzi???

Narudia tena kwa hili, Serikali iache sarakasi zote ije na majibu na hoja za msingi. Hizi siasa as kina Mwigulu na Mwenyekiti kutoa pole kupitia mitandao ya kijamii hazina mashiko Kwa tukio kama hili.

Tatu kamanda Sirro ulituhumiwa kutuma vijana kumfwatilia Lisu na wewe japo Ni mwanasiasa lakini Kwa hili siasa hairuhusiwi tunaomba majibu maana hata walitaka kumuua Mungu akakataa walimfwatilia kutoka Bungeni hadi walipomshambulia.

Nne Mwenyekiti wa chama; kauli yako ya walete huku mtaani niwashughulikie nayo naomba uitoleee ufafanuzi ulikua unamaanisha nini?? Au maana Ni hii tuliyoiona jana??? Hapa msitufumbe Kwa chochote njooni na lakini kamili.
 
Labda walioona kwa mbali inaishia ishia,
Na pengine hata walimuhoji dereva wa Lissu akawajibu hivyo.
Pia si rahisi kuwe hakuna hata mpita njia mmoja japo wa mbali tu
 
Kwakuwa Jeshi la Polisi limealika uwasilishwaji wa taarifa kuhusu kushambuliwa kwa risasi kwa Lissu,mimi VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa naanza safari ya kuzisaka taarifa. Natoka hapa Kibiti,Pwani kwenda Dodoma.

Risasi 32 si jambo la kawaida. Kwa uzoefu,historia na fani yangu naamini nitapata la kulipata na kuliwasilisha polisi. Nakwenda Dodoma kwa kazi maalum. Ikinipasa,nitakwenda Singida,Dar na kwingineko. Naanza na Dodoma

Wasiojulikana watajulikana tu. Tuwe na subira. Mpunga hufukiwa lakini wakati muafaka unapofika huchomoza. Hakuna siri ya milele

Smg ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
 
Mzee Tupatupa unaanza safari ya kuwasaka "watu wasiojulikana" waliofyatua risasi na kutokomea "kusikojulikana" kwa gari ambayo namba zake "hazijajulikana"?Chunga na wewe usijeishia "kusikojulikana"!
 
Back
Top Bottom