Kwakuwa Jeshi la Polisi limealika uwasilishwaji wa taarifa kuhusu kushambuliwa kwa risasi kwa Lissu,mimi
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa naanza safari ya kuzisaka taarifa. Natoka hapa Kibiti,Pwani kwenda Dodoma.
Risasi 32 si jambo la kawaida. Kwa uzoefu,historia na fani yangu naamini nitapata la kulipata na kuliwasilisha polisi. Nakwenda Dodoma kwa kazi maalum. Ikinipasa,nitakwenda Singida,Dar na kwingineko. Naanza na Dodoma
Wasiojulikana watajulikana tu. Tuwe na subira. Mpunga hufukiwa lakini wakati muafaka unapofika huchomoza. Hakuna siri ya milele
Smg ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)