Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma ~ Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
Inahitaji akili ya mwendawazimu kumuamini Jumanne Muliro,mtu ambaye bila aibu amesema uongo kuwa Polisi haikuhusika kuwakamata viongozi na wanachama wa Chadema na kuwavunja miguu na mikono licha ya ushahidi wa wazi wa Polisi kufanya uhalifu huo.
 
Unaijua vita iliyo ndani ya pazia na maazimio ya kumharibia mama from within?
Siijui lakini kama ipo basi mama ni boya kupitiliza. Kwa nini? Yeye ndiye rais na anapaswa kujua kila kitu kinachoendelea nchini na hawa wote ''within'' kawaweka yeye. Au umesahau nchi yetu rais ni kama mungu mtu?
 
Mkuu sio kila kitu siasa na dini. Watu wanamaisha mengine nje ya vitu hivyo wiwili. Si sahihi kila kitu kiwe ni dini na siasa. Tatizo letu wengi tunapenda habari zinazozua taharuki sio kuwa objective. Katika dunia hii ielekeze akili yako iruhusu ukweli wowote sio uongo unaoutaka wewe
Sikatai watu wana maisha mengine...

Kwa maneno yako tungojee muliro na genge lake watakuja na taarifa gani...

Nitakuwepo hapa kukuuliza umeamini hiyo taarifa au la...
 
Inahitaji akili ya mwendawazimu kumuamini Jumanne Muliro,mtu ambaye bila aibu amesema uongo kuwa Polisi haikuhusika kuwakamata viongozi na wanachama wa Chadema na kuwavunja miguu na mikono licha ya ushahidi wa wazi wa Polisi kufanya uhalifu huo.
Uko sahihi kabisa. Siju ni kwa nini polisi hawatumii akili. Wanajiweka kwenye nafasi ya kutoaminika wenyewe. Sasa hivi hakuna anayewaamini tena.
 
MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma ~ Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
Polisi wako fasta leo 🤣🤣
 
Na huko kwenye Dini na kwenye mpira ndiyo kuna wajinga wengi wafuata mkumbo kisa Kiongozi wa Dini au mpira katoa tamko,hata kama hilo tamko ni la kijinga bado watalifuata!!
Ndo nchi yetu ilivyo mkuu ...
Mtanzania umtoe ndani akaandamane ni kazi mno ila sio kazi kwenye simba na yanga pamoja na dini...
 
MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma ~ Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
Msipomkamata Stev Nyerere na yule mwehu Mafuvu nitawashangaa sana.
 
Mkuu sio kila kitu siasa na dini. Watu wanamaisha mengine nje ya vitu hivyo wiwili. Si sahihi kila kitu kiwe ni dini na siasa. Tatizo letu wengi tunapenda habari zinazozua taharuki sio kuwa objective. Katika dunia hii ielekeze akili yako iruhusu ukweli wowote sio uongo unaoutaka wewe
Elezea kitu ambacho kipo nje ya siasa kwenye maisha yako. Ukiweza nitakuwa mjinga wa JF 2025!
 
Catholic inatisha mkuu... Unadhani ungekua ni wewe si tungeambiwa kifo ni kifo tu?😁
Hayo maeneo ya kuishi.mapdre huwa wanafanyiana umafia wenyewe kwa wenyewe.

Ona huyu padre kifo chake cha kutatanisha kwenye nyumba wanaishi Mapadre Dar es Salaam .Kesi ilipotelea hewani hadi leo

Back
Top Bottom