Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

Kitendo cha kushambuliwa kwa Padri Dkt. Charles Kitima katika makazi yake, kama inavyoripotiwa, ni tendo la kishenzi linalohitaji kulaaniwa na kila mtu anayeipenda amani na utulivu wa Taifa letu la Tanzania. Hili sio suala la uhalifu wa kawaida, bali ni kitendo chenye nia mbaya ambacho kinaweza kuathiri umoja na mshikamano wa jamii yetu.
Naiomba Jeshi la Polisi la Tanzania (@tanpol) kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka, na kutoa taarifa kwa umma kwa wakati ufaao. Natarajia kwamba wahusika wote waliotekeleza kitendo hiki watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Kitendo hiki ni cha aibu, kinyama, na kinaweza kusababisha athari mbaya kwa maendeleo ya amani na ustawi wa Taifa letu.
Pia, namtakia Padri Dkt. Charles Kitima apone haraka na Mungu ampe nguvu pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Tujenge Taifa la amani, upendo, na haki kwa wote.
 
🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 

Kwenye matukio nyeti kabisa Kama hili la kushambuliwa huyo Padre Kitima, Jeshi la Polisi kabla ya kutoa taarifa yake kwa umma basi liwe linakaa vikao vyao vya Ndani na kuitathmini kwa kina kabisa hiyo taarifa yao wanayotarajia kuitoa kwa umma. Wasiwe na utaratibu wa kukurupuka na kisha kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikiibua utata mwingi zaidi na kuibua maswali mengi zaidi yasiyokuwa na majibu kama taarifa yao hii waliyotoa.
 
Halafu usiku saa nne na Robo .Padre anakuwa bado yuko bar analewa? Sio muda wa kuwa chumbani kwakehuo?

Na Raia kutoka nje wanakuwa ndani ya hiyo bar nao wakilewa? Muda huo?

Kuna maswali.mengi kuliko majibu
Na hii template mlishirikiana kuitengeneza kabla ya tukio...

Watanzania sio ng'ombe we don't buy your stupidity...nyama ya binadamu tamu mtaanza kulana wenyewe soon
 
Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.
Haliwezi kuwa igizo kama la yule mkenya aliyedaiwa kwenda kuomba toba kwa Mchg Lwakatare!
 
Polisi hawawezi kujichunguza wenyewe. Ila wajue ndiyo wanazidi kumharibia huyo mgombea wao.
 
Haahaa lengo ni kuzima...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…