Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
hamna hoja hapa, mto mada umedhihirisha wazi kabisa, kwa kuegemea upande moja, we una uhakika gani, kama kabebeshwa, em tuanzie hapa kwanza,.(sitetei upande wa wowote)

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mtu afanye vurugu aachiwe sababu tu ya kuogopa wawekezaji? Huo ni upuuzi
Kwa Tanzania ukiwa mhalifu jifiche kwenye dini au siasa utatetewa kwa nguvu zote. Kuwa mchungaji, sheikh au mwanasiasa siyo kwamba huwezi kufanya uhalifu.
 
Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
Nakubaliana kuwa yupo sehemu.anayostahili. wapigania haki wote jela ndo makazi yao
 
Hakika dadangu....

Yaani dada Sky Eclat anataka tupuuze maneno yale makali toka kijana mwenzetu Mdude....huku mh.Mwenyekiti wake akishindwa KUMKATISHA....

Waswahili wananena "ukimuona mbwa juu ya bati ,ujue amepandishwa"

#KaziIendelee

Umenena kaka

Na wahenga wanasema "ukimchekea mbwa atakufuata hadi msikitini"
 
Kwa Tanzania ukiwa mhalifu jifiche kwenye dini au siasa utatetewa kwa nguvu zote. Kuwa mchungaji, sheikh au mwanasiasa siyo kwamba huwezi kufanya uhalifu.
Majambazi na watakatishaji fedha za madawa ya kulevya wamejificha huko mkuu, akina Mwingira, Gwajima, Lwakatare (Marehemu), Mbowe, Makonda na majizi ya aina hiyo, ni untouchables, ukiwagusa tu utashambuliwa na wafuasi wao vibaya mnoo
 
Hao wasio na akili ndio wanakuongoza toka 1961 mpaka leo bado wanakunyoosha na kizazi chako chote, sasa jiulize nani hana akili wewe 'mwenye akili' kuongozwa muda wote huo na asiye na akili au asiye na akii...
Hawajawahi kuniongoza mimi wala kuongoza mtu yeyote.Kuongoza ni kufanya watu/nchi kufikia malengo.

Hakuna malengo wala goals ambazo CCM imeachieve ndiyo maana hadi leo hata baada ya zaidi ya miaka hamsini ya uhuru bado Taifa linahangaika na vitu vidogo sana kama vile huduma za maji,afya na elimu.
 
Kwa Tanzania ukiwa mhalifu jifiche kwenye dini au siasa utatetewa kwa nguvu zote. Kuwa mchungaji, sheikh au mwanasiasa siyo kwamba huwezi kufanya uhalifu.
Sijasema kuwa ukiwa mwanasiasa, huwezi kufanya Makosa, mbona Sabaya yupo selo akikabiliana na kesi yake?

Tunachokataa ni Jeshi la Polisi, kubambika kesi kwa mwanasiasa, ambaye anaonekana ni "mwiba" kwa watawala, kama ambavyo ameonyesha Mbowe, kwa kupigania Katiba ya nchi

Tunalitaka Jeshi la Polisi litumie weledi katika kutekeleza majukumu yake
 
Akili ya kipumbavu Sana, kwamba tumuache mtu afanye anavyotaka yy na kutishia hadi viongozi kwa kuogopa eti wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza,Tanzania ni nchi huru na Ina Rais anaye iongoza na watu wote tunatakiwa kutii mamlaka ya nchi,
Sasa hutii chochote, unajiamulia tu kwa kudharau kuwa kiongozi ni mwanamke, Tena unamlazimisha kabisa eti ukae nae uongee nae,na unasema waziwazi kuwa utafanya chochote,unaenda mbali zaidi kumwambia uta mnyolea wembe ulio mnyolea mtangulizi wake, na mtangulizi wake Kesha kufa, unategemea mama akuache t?
Point yangu hapo nikwamba tutii mamlaka husika, hakuna aliye juu ya Rais, wala Wazungu hawawezi kutuingilia,
Mkuu mwendazake alikuwa na akili kama zako na nyie mkamponza na kumtia kiburi, yuko wapi sasa? Sasa mpotoshe mama pia
 
Nchi za MAGHARIBI na UGAIDI....

Unapotaja tu ugaidi ,Magaidi ,gaidi ujue nchi za MAGHARIBI hushtuka mno......nimeshangaa eti unasema kuwa NCHI HIZO ZITAKUWA NA HURUMA na wahusika wa vitendo hivyo......

Hivi ni lini nchi hizo zimeanza kuwa na HURUMA NA KUGUSWA NA WANAOHUSIKA NA HAYO MAMBO?!!!

Kwao ukituhumiwa ugaidi basi ujue utatambulika sio gaidi mpaka pale MAHAKAMA ikithibitisha hayo......

Kutuhumiwa si KUHUKUMIWA....

Tusubiri mahakama ifanye kazi yake.....

Nasubiri mahakama ifanye kazi yake zaidi ya humu mitandaoni KUHUKUMU kuwa ANA/HANA HATIA......

#MahakamaNiMuhimiliWaNchi
#KaziIendelee
mahakama za ccm
 
"Mama anauoiga mwingi, anawakaanga Sukuma gang"
 
Ivi hii dhana ya kwamba wanasiasa wa upinzan hawakosei au hawana makosa?
Kwamfano ushahidi ukaonesha amehusika kwenye ugaidi mtakubali? Acheni sheria ifuatwe kama kweli hana makosa akaithibitishie mahakama hivyo vyombo vya habari vya kimataifa havitasaidia chochote zaid ya propaganda tu mana ndo wanachokipenda
Mliwahi mpotosha mwendakuzimu sasa mnataka mpotosha mama pia
 
Kafanya vurugu gani? Au na wew ndiyo walewale, ebu zitaje hizo vurugu mkuu
Rais, ambaye ni amiri jeshi mkuu, kasema subirini kwanza mambo ya katiba mpya, yeye anaanzisha makongamano (ni uasi huo). RC na DC wanasema ili kudhibiti corona tupunguze mikusanyiko isiyo ya lazima, ya lazima iombewe kibali, yeye anawaita wajinga. Huoni kama hizo ni chokochoko?
 
Rais, ambaye ni amiri jeshi mkuu, kasema subirini kwanza mambo ya katiba mpya, yeye anaanzisha makongamano (ni uasi huo). RC na DC wanasema ili kudhibiti corona tupunguze mikusanyiko isiyo ya lazima, ya lazima iombewe kibali, yeye anawaita wajinga. Huoni kama hizo ni chokochoko?
Mbona wapenzi wa soka wanasongamana kwenye viwanja vya mpira?

Unataka kutuambia kuwa kwenye hatari ya corona ni kwenye makongamano ya Katiba ya chama cha Chadema pekee??
 
Back
Top Bottom