Uchaguzi 2020 Polisi waondoa kizuizi alichowekewa Tundu Lissu Kiluvya. Asema anaendelea na safari yake

Halafu kuna mtu kesho ataongea kudai kuwa police wametumia busara kuachia Lissu aendelee na safari yake. Sijui Hawa Jamaa huwa wanakoseaa wapi mpaka wanashindwa kutumia busara mwanzo.
Komaa Lissu Komaa Sana na leo wameaibika tena. Ile mitutu ya leo wameoneaha woga mkubwa sana.

TL we ni nomaa sana.

Polisi nao wanahitaji Mtenda haki na mzingatia utawala bora kama TL. Polisi wanateseka bure bila sababu yoyote kwa maagizo ya wahuni fulani tu kutoka juu.
 
Pole zake watz siyo wa mchezo mchezo leo wamemwache pale Kiluvya pekee yake na kikundi chake masaa zaidi ya 9 amepigwa na jua na mbu. Nafikiri atakuwa amewatambua vizuri na bado tarehe 28/10/2020.

Waliomzuia ndiyo wamepata aibu jeshi la polisi liache kujifedhehesha kiasi hicho hadi wanakosa sababu na kuamua kuondoka hivi hawaoni kuwa wanakosa weledi wa kazi yao. Hakuna polisi duniani anayemzuia mtu bila ya sababu hadi anaamuwa kumuachia mtu aliyekuwa amemzuia
 
Wananchi walikuwa wameanza kusogea kwa wingi eneo la tukio

View attachment 1592448

View attachment 1592451
Kesho tena akileta ujinga wanambana anakaa mpaka jioni

Daresalam kuna wapiga kura milioni kama 3 sasa nyie hapo manategemea ngapi?
Kanda ya ziwa usitegemee wao hupenda shangwe ila ukiondoka wanaenda na mambo yao
Kwa utashi wako ujinga gani alileta na unefutika saa ngapi hadi aachiwe?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Point tatu kachukua Mh. Lissu kiulainiii.
 
Ha
Upinzani wa bongo|Tanzania bwana!.

Ukiachiwa huru|ukipewa haki yako uongozi unakua umelegea..Haha.

Sawa,Endeleeni kuvunja sheria tu kwa kutafuta political violence.

Itafika mahali itabidi kila mtu mwenye madaraka atimize wajibu wake ipasavyo.

Haki siyo barashishi aise haki inatakwa siyo ombi aise
 
Kuanzia saa nane mpaka usiku? Nafikiri kama akili zake zinafanya kazi,atakuwa amegundua kuwa swala la kuwaingiza watz barabarani haliwezi kuwa jepesi kama alivyokuwa analichukulia.
Wewe ulikuwa unafikiria nini kwani? Mbona wamemruhusu sasa? Kinacho matter ni ruhusa na sio muda alio ruhusiwa utopolo wewe
 
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ni muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini Tanzania. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa na mkosaji kujiadhibu mwenyewe, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. Uliona wapi nyani anajizuia kula mahindi ya mkulima? Nyani wamezoea kula mahindi ya mkulima kiasi kwamba mkulima akiwafukuza au kuwaua wasimalize mahindi yake, watamuona kama anawaonea bure! Wanadhani kula mahindi wasiyoyalima ni haki yao ya msingi au ya kuzaliwa.

Jinsi ambavyo wanakula mahindi ya mkulima, vivyo hivyo CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya chama cha mapinduzi ilipotufikisha.

Na kama ambavyo ili mkulima ajiepusha na nyani anapaswa kuwaua au kuwafukuzilia mbali nyani, vivyo hivyo kwa chama cha mafisadi na serikali yake, ili kuepukana na ufisadi wao, hatuna budi kuwapiga chini mwaka huu wa 2020. Hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang’oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang’oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.

Ndugu watanzania tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na kupe hawa wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hupenda kuchakura mwenyewe vichakani kutafuta chakula bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wajitafutie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa. Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona humtakii mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.

Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa wanakiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2015. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hiyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (maCCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo waaliyoyaleta MABEBERU wa kikoloni.

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 22 alizoziacha Mkapa hadi Tsh trillion 55 sawa na ukuaji wa 150%! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi maisha bora tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukampigie kura Mgombea wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hii ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020!
 
Sasa nikiona bavicha yeyote anataoa mkwara humu wakati Lisu kashikiliwa na polisi masaa 8 njiani mpaka wameamua kumuachia kwa hiyari yao wenyewe, hakika ntamuona bavicha huyo ni kopo kabisa.
Ulitaka wawashambulie Askari!?
Nenda ukasome historia za akina Mahatma Gandhi na Martin Luther, utajipatia ufahamu!
 
Aiseee police ndo wanamuua magufuli sasa an jamaa kafungiwa na bado anatake headline kama kawaid
Tuvushe mwamba
Ushauri was Bure,awatafute wanaomhujumu,aanze na wale wote wanaompa ushauri,unaomletea ugumu kufikia malengo,kampeni inakuwa ngumu kids wazalendo maslahi.
 
Hapo awali

06 October 2020
Pwani , Tanzania

RPC mkoa wa Pwani azungumza

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani aliahidi polisi kukaa na Tundu Lissu barabarani Kiluvya, Kibaha mkoani Pwani hata kwa siku 14 kutekeleza amri toka juu
 
Upinzani wa bongo|Tanzania bwana!.

Ukiachiwa huru|ukipewa haki yako uongozi unakua umelegea..Haha.

Sawa,Endeleeni kuvunja sheria tu kwa kutafuta political violence.

Itafika mahali itabidi kila mtu mwenye madaraka atimize wajibu wake ipasavyo.
Amevunja sheria?
 
You nailed it mkuu[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ni muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini Tanzania. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa na mkosaji kujiadhibu mwenyewe, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. Uliona wapi nyani anajizuia kula mahindi ya mkulima? Nyani wamezoea kula mahindi ya mkulima kiasi kwamba mkulima akiwafukuza au kuwaua wasimalize mahindi yake, watamuona kama anawaonea bure! Wanadhani kula mahindi wasiyoyalima ni haki yao ya msingi au ya kuzaliwa.

Jinsi ambavyo wanakula mahindi ya mkulima, vivyo hivyo CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya chama cha mapinduzi ilipotufikisha.

Na kama ambavyo ili mkulima ajiepusha na nyani anapaswa kuwaua au kuwafukuzilia mbali nyani, vivyo hivyo kwa chama cha mafisadi na serikali yake, ili kuepukana na ufisadi wao, hatuna budi kuwapiga chini mwaka huu wa 2020. Hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang’oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang’oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.

Ndugu watanzania tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na kupe hawa wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hupenda kuchakura mwenyewe vichakani kutafuta chakula bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wajitafutie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa. Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona humtakii mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.

Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa wanakiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2015. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hiyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (maCCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo waaliyoyaleta MABEBERU wa kikoloni.

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 22 alizoziacha Mkapa hadi Tsh trillion 55 sawa na ukuaji wa 150%! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi maisha bora tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukampigie kura Mgombea wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hii ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020!
 
Baada ya mapema leo polisi kuzuia msafara wa Tundu Lissu eneo la Kiluvya, hatimae wameondoka na kuacha uendelee na safari na Lissu amesema ataendelea na safari yake kama ilivyopangwa na atakutana na wanachama usiku huu. Baada ya polisi kuondoka, Lissu ameongea yafuatayo.

LISSU: Nasikia hata siku moja imewashinda na wameondoka, sasa kwa sababu walikuwa wametuzuia na lengo letu lilikuwa kwenda kukutana na wanachama wetu Mlandizi, sasa tunaelekea Mlandizi, lazima twende Mlandizi na tumemwambia mheshimiwa mbunge wetu, Kinabo awaambie watu wake ambao walikuwa wanatusubiri tangu asubuhi kwamba, sasa tunaelekea Mlandizi kukutana na wanachama wetu.

Sheria haisemi kwamba, kama ilivyo sheria ya uchaguzi, haisemi mikutano ya wanachama nayo lazima ianze saa kumi na mbili mpaka saa kumi na mbili, tutafanya usiku na wanachama wetu.

Naomba niseme mambo mawili, la kwanza ni kumshukuru sana baba askofu Mwemakula kwa kuja kutuunga mkono hapa, Askofu Mwamakula amejidhihirisha katika kipindi hiki kigumu katika historia ya nchi yetu kwamba ni kiongozi wa kiroho kwelikweli, kiongozi ambae yuko tayari kusimamia ukweli wa imani yake. Sasa askofu Mwamakula ni Desmond Tutu wa kwetu, tunahitaji viongozi wa kiroho ambao hawana hofu ya hizi mamlaka za kutisha tisha za utawala wa aina hii.

Tumekaa hapa tangu saa tano asubuhi, kuna watu wanafikiri tumepotezewa muda, hatujapotezewa muda. Unapopigania haki, ukweli lazima uwe tayari kupigania masuala ya msingi. Kama huruhusiwi kuonana na wanachama wako kwenye kikao cha ndani, anaambiwa uombe kibali cha mapolisi, kama hiyo huwezi kusimamia utasimamia kitu gani?

Kwa hiyo tulikuwa tuna haki ya kwenda tunapotaka ili mradi hatuvunji sheria, tusije tuka-negotiate kwenye masuala ya principle.

PIA SOMA,
CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wa CHADEMA Tundu Lissu ukielekea Kibaha

RPC Pwani Wankyo Nyigesa: Tutakesha na Tundu Lissu, ndiyo kazi yetu

Askofu Mwamakula aenda alipozuiliwa Lissu kumtia nguvu
Ila Tundu Lissu ana spirit ya kipekee sana, sioni mwanasiasa kama wa kuvumilia kukalishwa hapo barabarani kwa kutwa nzima.
He is extraordinary
Lissu ameshinda!!! CDM tumeshinda!! Nuru imeshinda giza!! Jeshi la polisi wameamua kunyoosha mikono juu!! Wameamua kuondoka eneo la tukio muda huu!! Wameona mziki wa Lissu wataishia kukaa hapa mpaka tarehe kumi
!! Wamesepaaa!! Sasa ni Mwendo wa kwenda tunakotaka!
 
Back
Top Bottom