Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Moja ya jumbe ya maandamano ni kuachiliwa kina heche nafikiri limefanyiwa kazi, bado Lisu
 
Lissu wana muachia lini ?
Hata wamshikilie maisha yake yote, sisi hatuangalii Lissu wala chama chochote. Msimamo wetu kama wananchi uko palepale. Katiba mpya, uwajibikaji, no more kutekana na kuuana, na tunataka uchaguzi urudiwe tuweze kuchagua viongozi tunaowataka. Hatuna mwanasiasa. Sisi wenyewe tuna akili. Sasa wao wakazane kuwanunua wanasiasa, wakidhani wanasolve kitu. 9.12.2025
 
Nyinyi CHADEMA mkae mkijua hili ni beef letu sisi wananchi na serikali msiingilie kabisa hayo maridhiano sisi hayatuhusu.Sisi tunataka Samia ajiuzulu kwanza
Ma ccm yanafanya kusudi kutupunguza nguvu.. hao chadema wakikubali maridhiano wote m&*% yao.. mimi binafsi sitaki kusikia chochote zaid ya kila aliehusika awajibishwe
 
Fanyeni fujo, wizi na kuharibu vitu Kisha lawama pelekeni kwa Raisi kama yeye ndie aliefanya wapumbavu wakubwa . Ujinga wenu unasababisha ugumu wa usafiri na kupanda vitu bei.
#free and fair election ndio tiba
 
Joto bado ni kali sana, wanavutavuta kamuda kupoe kwanza ndio watamuachia ila haitazidi Christmas. Lissu akitoka leo mchakamchaka unaweza anza upya kabisa
Sasa mbona hili joto halioneshi dalili ya kupoa.

Kwasababu njia pekee ya kufanya raia wapoe ni kuona uongozi huu unajiuzulu na wahusika wakichukuliwa hatua ikiwemo ICC
 
Kumbe siku hizi kuna dhamana kwenye makosa ya uhaini?
 
Anaandika Gobless E. J. Lema kwenye X-Twiiter account yakeπŸ‘‡πŸ‘‡
 
Kwa hiyo watuhumiwa wa uhaini na ugaidi wamepewa dhamana?

Au walikuwa wanapima upepo tu?
 
R.I.P Tanzanian who died in 29 october.we tried so much but our efforts were in vain.But we are GEN-Z we want change in our country.we will not give up or surrender the revolution has already started and it has to be completed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…