Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

Uko sahihi kabisa, anafanya siasa za publicity kwa kuteka wasiojielewa eti anafanya alichokuwa anafanya Magufuli. Lakini ukweli unafahamika huo umati ni wa kutengeneza kwa gharama kubwa, na ndio maana ilipofika uchaguzi wa 2019 & 2020 ilibidi wanajisi uchaguzi, maana walikuwa wanajua umati wao ni nguvu za Dola na Wala haukuwa na uhalisia.

Ni kweli kabisa afanyacho Makonda ni kujifanya anaieneza ccm, lakini kwa wakati huo anajisafisha kwa kufanya siasa za maigizo. Anajua ni kwa kiwango alifanya uhalifu, Sasa anapima ni kwa kiwango gani watu wamesahau. Cha ajabu Kila mahali anatoa maagizo ya jukwaaani, lakini hakuna uhakika wala mrejesho wa utekelezaji wake, zaidi ya kufurahisha genge.
 
Babu Sihasa.Anachokifanya ni Swahihi.CCM NI TAASISI.
 
Hatujasahau yaliyopita na jinai haifi.

Huyu mtu mwenye makando kando anaanzaje kuleta amsha amsha?

Anaamsha majambazi na wavamizi wa awamu ya tano labda waliookuwa wamepumzika sasa anawarudisha kazini.

Nani mwenye akili timamu aamshwe na siasa za kishamba kama za awamu ile ya maigizo?

Yani unamset mwamausalama Dumila anajidai anachoma mahindi halafu anapita Magufuli eti kiongozi wa wanyonge anakula mahindi ya kuchoma barabarani, mchoma mahindi igizo linafeli anaejiexpose kwa bastola kujichora ndio mnaturudisha huku mara leo kaingia na ngamia , mara lori la mchanga mumshauri basi aingie uchi next time.

You have stooped so low Pascal, this is not the type of content that should be coming from a person with intellectual rigour like you .

This kind of content as expected, should be coming from simpleton, trivial and slothful wannabe.

Do a thorough self and concrete. reappraisal it is not late.

 
Na waliomuweka hapo wanajua ni mropakaji, ila wamemuagiza afanye siasa kama za awamu ya Tano, wakiamini siasa zile zilipata uungwaji mkono, lakini hawakuwa tayari siasa nyingine kufanyika, na wakahakikisha vyombo vya habari vinahubiri watakacho. Ni kama vile unatengeneza uongo kisha inafikia mahali unauamini mwenyewe, kisa tu hutoi ruhusa ya wanaokwambia unasema uongo kuweka uongo wako hadharani!
 
Ngoja chadema waje waseme hy picha yao imepigwa kwenye angle ambayo haina watu wengi 😂
 

Msimtishie mwenezi muacheni achape kazi. Napendekeza mwenezi aanze kutandika bakora watendaji wote wazembe hata mawaziri akiona inafaa.
 
Ingekuwa ni kwenye mahakama za kimataifa Leo hii Makonda angekuwa ndani. Lakini kwa hizi mahakama zilizo na kesi ya kina Mdee mwaka wa nne huu na ushahidi wote upo, utakuwa mjinga kwenda kupoteza muda wako mahakamani kumshtaki muhalifu aliyetumika na kiongozi dhalimu wa awamu iliyopita.

Huwa nawaelewa sana wazungu kwenye mikataba ya raslimali zetu kuamua mashauri Yao yaamuliwe kwenye mahakama za kimataifa. Wangekosea watumie mahakama za humu nchini, leo hii wangekuwa kama wamasai wa Loliondo.

Makonda ameibuka upya sio kwamba tumesahau uovu wake, bali tunaonyesha kuwa Yale yaliyoitwa maridhiano ilikuwa ni utapeli ili mama atawale bila pressure ya wapinzani. Lakini kiukweli bila wahalifu ccm haiwezi kufanya siasa.
 
Mpeni nafasi mh makonda afanye kazi yake aliolekezwa na chama Cha mapinduzi na kupekuana pekuana katika hii nnchi hakuna aliye msafi hata mmoja wote tunamapungufu yetu.kama binadamu mwacheni afanye kwa niaba ya chama chake mh makondo mbele kwa mpaka kieleweke ccm haitaki mbamba mbamba piga kazi wakuelewa tu
 
Uko sahihi kabisa, anafanya siasa za publicity kwa kuteka wasiojielewa eti anafanya alichokuwa anafanya Magufuli.
Huyu bwana anachokifanya ni kutumia siasa chafu za wakati wa JPM, ni uongo mtupu .
JPM mwenyewe amekutwa na Bilioni majumbani , mtetezi wa Wanyonge kama alivyo huyu bwana
Lakini ukweli unafahamika huo umati ni wa kutengeneza kwa gharama kubwa, na ndio maana ilipofika uchaguzi wa 2019 & 2020 ilibidi wanajisi uchaguzi, maana walikuwa wanajua umati wao ni nguvu za Dola na Wala haukuwa na uhalisia.
Umati unaouona ni maagizo anayotoa kwa viongozi wa CCM Wilayani na vijijini . Hawa wanamuogopa sana kwasababu ana nguvu hata za kumkaanga Waziri mkuu hadharani. Juzi alikuwa mgeni rasmi daraja la Busisi na Waziri anatoa taarifa kwake! Hata waziri hajui anawajibika kwa nani kwasababu ya hofu.

Huku mitandaoni kajaza watu wanaanzisha thread za hovyo sana na hasa JF.
Utasoma nyuzi eti 'mwenezi anakunywa maji, sasa anakula chakula cha mihogo, mwenezi anaingia chooni '' yaani upuuzi mtupu . Anatumia mbinu zile zile akiwa RC na Clouds Fm.

Anachokifanya ni kusafisha taswira yake kutokana na uovu alioufanya enzi zile akiwa 'deputy president'
Hajaeleza kuhusu vyeti vyake kitaaluma
Hajaeleza Roma Mkatoliki alikuwa wapi na alijua nini kuhusu yeye
Hajaeleza, akiwa RC DSM vile viroba vya miili ya watu pale coco beach vilihusu nini

orodha ni ndefu, leo anataka kutueleza nini!
 
Mahakama ilikuwa 'msemaji wake' kwa kesi pale kinondoni. Yaani ilimtetea si kusikiliza kesi
Tume ya maadili haikufua dafu, waliufyata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…