Prof. Mukandala: Matokeo ya Rais yahojiwe Mahakamani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba, 2022

0FF9A0A8-C4BC-46A9-BFD0-8FEA9FDF05CF.jpeg

Mapendekezo 18 ya Ripoti yanasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala
  1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote, yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi.
  2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkala ya kushughulikia swala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili, msajili wa vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.
  3. Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote vyenye usajili kamili.
  4. Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.
  5. Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenyekiti) jaji mkuu wa Zanzibar (M/mwenyekiti), kamishna wa serkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Tanzania bara, mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ya Zbar, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na wajumbe 2 watakaoteuliwa na jaji mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria Zbar. Pia, angalau wajumbe wawili wa uteuzi wawe wanawake, sifa za kuwa mwenyekiti, makamu au mjumbe ziainishwe, nafasi za ujumbe zitangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi
  6. Matokeo ya Rais jahojiwe kwenye Mahakama ya juu
  7. Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, maadili, weledi, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao. Wasimamizi watakaokiuka taratibu wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  8. Tume ya taifa ya uchaguzi ipewe fedha kwa wakati ili iweze kutelekeza majukumu yake ipasavyo.
  9. Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote badaa ya uwepo wa sheria mbili kama sasa, maafisa wa uchaguzi watakao engua wagombea kushiriki uchaguzi bila kuzingatia sheria na weledi wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  10. Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe na kuongezwa.
  11. Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye kila chama cha siasa, na ujumuishi wa makundi maalumu, pia ushiriki wa jinsia moja kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%. Pia, utaratibu wa uwakilishi wa viti maalumu kwa wanawake uendelee, isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka 10 pekee.
  12. Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya
  13. Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe
  14. Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia na mpiga kura.
  15. Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi watambue kuwa vitendo vya rushwa havitavumiliwa wala kuonewa muhali. Katiba ya Chama cha Siasa iwe na adhabu ya kumuondoa katika Mchakato wa Uchaguzi Mgombea aliyedhaminiwa na chama akithibitika kuhusika na vitendo vya rushwa
  16. Kuanzishwe utaratibu wa mijadaa kila mwaka itakayohusisha viongozi wakubwa wa kitaifa na kisiasa ili kudumisha mshikamano, mahakama iwe ni mamlaka ya mwisho ya kuamua pindi maridhiano yanapokwama
  17. Wanahabari waunde chombo cha kusimamia wanahabari na vyombo vyao, vyombo vya umma vitoe muda sawa wa kutangaza habari za wagombea wa vyama vyote kwa usawa, uwepo mchakato wa wazi wa kuwajibisha vyombo vya habari badala ya kufungiwa pekee na mkurugenzi wa habari na mawasiliano
  18. Mchakato wa katiba mpya uendelee, hata hivyo mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ili kujadili maswala ya msingi kama muungano, mamkala ya Rais, madaraka ya serikali za mtaa, Rushwa, mfumo wa uchaguzi n.k. Pia, sheria ya mabadiliko ya katiba na sheria ya kura ya maoni zihuishwe pamoja na kuundwa kwa jopo la wataalamu ili kufanya mapitio ya katiba inayopendekezwa kwa kuzingatia hali ya sasa ya kiasiasa, kiuchumi na kijamii.
f312dd88-90bb-4e5e-a7c0-fa9de24b212a.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala, Makamu Mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho mara baada ya kupokea Ripoti yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.


Maneno ya Rais Samia Suhuhu Hassan
Kazi hii imechukua miezi 10, haikuwa rahisi. Pengine ningewaacha ingechukua zaidi ya muda huu, lakini mimi pia navutwa shati.

Wananchi waelewe kuwa maoni ya kikosi kazi sio amri kwa Serikali. Tutaitana tena tuangalie na hali halisi ndani ya serikali na hali halisi ya sheria zetu pia ili tuweze kuyafanyia kazi vizuri

Tumepokea, na kama mlivyoona ripoti yenu ina mambo kadhaa, sisi kwenye serikali inabidi tujipange vikosi kadhaa, na wengine kati yenu tutawaomba mje kwenye vikosi kazi hivyo tujadili.

Siyo kwamba leo tumepewa ripoti ya kikosi kazi, kesho tutaanza kutekeleza hapana. Tumepokea, na wananchi wasikie tumepokea na tutafanyia kazi.

Na nyie watu wa siasa mjichambue, ni kazi ya jaji mtungi na watu wake. Nakubailiana na hoja ya 40% ya wanawake kwenye vyama vya siasa.

Tumepokea marekebisho ndani ya vyama vya siasa na wenyewe wasiwe mahodari wa kuirekebisha serikali lakini na wenyewe ndani tutizame je wanavyokwenda mambo ya usawa wa kijinsia yapo, mambo ya matumizi mazuri ya fedha yapo na mwengine akipata chama cha siasa anasema ni chake, na siyo cha wanachama. Ni chake. Kujitathimini wenyewe ni jambo zuri.

Mgao wa ruzuku tutauangalia, hatuwezi kusema tutaongeza fedha zaidi sababu ni swala la kibajeti.

Matumizi ya teknolojia kwenye tume ya uchaguzi ni muhimu, ili teknolojia inayotumika iweze kutoa matarajio ambayo watu wanataka.

Tume ya uchaguzi tutalikalia kitako, ya serikali yatakwenda na ya ripoti nayo tutayaangalia.

Mijadala ya kisiasa kila mwaka iwepo, kaeni mjijadili, msijadili tu serikali, mjijadili na ninyi wenyewe. Mijadala heathy, hata serikali inaweza kuwezesha mijadala hii.

Wanawake mara nyingi nafasi muhimu wakigombea wanaambiwa kaa upande, au wanaambiwa njoo chukua hiyo gombea. Ukikuta wanawake kawekwa ni mwepesi mno, kapangwa kumsindikiza mtu. Kwa hili nakubaliana nao, ni pamoja na kuwasomesha wanawake, kuwatia moyo kwamba wanaweza.

Rushwa ni kidonda ndugu, hakuna hata chama kimoja kimenusurika hapa. Hakuna chama ambacho hakifanyi, nadhani ni tabia ambayo tunatakiwa kuibadilisha. Watu wajue, kuchaguliwa si mimi, ni chama. Hili la Rushwa, tujitazameni sote.

Maswala ya mikutano hakuna anayekataa, lakini lazima kuwe na jicho. Hatutaki kurudi tulikotoka, polisi wataanza tena kupiga watu. Tunaposema kwamba kanuni lazima tuzitazame siyo kwa nia mbaya, ni nia njema. Lazima tutazame kanuni na sheria ndipo turuhusu.
 
Kubwa wadau wote na wananchi wanahamu mno kujua , Lini mapendekezo yataanza kufanyiwa kazi.

Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania akiwezesha mabadiliko, hili jambo ataacha legacy iliyotukuka na kukumbukwa vizazi na vizazi kwa Karne nyingi zijazo.

Maana kwa Tanzania, katiba imempa rais madaraka yanayofanana kwa karibu kabisa ya mithili ya mfalme hivyo jambo lolote linamungukia yeye katika kulikubali iwe kuleta mabadiliko katika katiba, mfumo huru wa uchaguzi ulio wa haki, teuzi n.k n.k

TUONDOKANE NA TAASISI MOJA ILIYOJIKITA MIZIZI POTE, TAASISI HURU ZENYE USEMI ZATAKIWA
 
Huenda pazia la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa likaondolewa nini ?
Hili ni moja kati ya mambo ya kawaida ambayo kwa akili za kawaida za mwanadamu hayakutakiwa kuzungumziwa kabisa kwenye huu ulimwengu tuliopo.

Lakini kwasababu tumeamua kujirudisha nyuma kama taifa, ndio maana zaidi ya mwaka mzima tumekuwa tukipigia kelele jambo la kisheria liruhusiwe kufanyika!

Mimi nataka nione kama atatangaza kuanza huo mchakato wa Katiba Mpya, na hiyo Katiba yenyewe itakuwa ni ipi? Rasimu ya Warioba au ile Pendekezwa?

Kutoka hapo ndio tutajua hili taifa linaelekea wapi, kama ni kuendelea kuzunguka mbuyu kama kawaida yetu, au tutaamua kusonga mbele.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba, 2022



Ripoti inasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala

 
Hili ni moja kati ya mambo ya kawaida ambayo kwa akili za kawaida za mwanadamu hayakutakiwa kuzungumziwa kabisa kwenye huu ulimwengu tuliopo.

Lakini kwasababu tumeamua kujirudisha nyuma kama taifa, ndio maana zaidi ya mwaka mzima tumekuwa tukipigia kelele jambo la kisheria liruhusiwe kufanyika!

Mimi nataka nione kama atatangaza kuanza huo mchakato wa Katiba Mpya, na hiyo Katiba yenyewe itakuwa ni ipi? Rasimu ya Warioba au ile Pendekezwa?

Kutoka hapo ndio tutajua hili taifa linaelekea wapi, kama ni kuendelea kuzunguka mbuyu kama kawaida yetu, au tutaamua kusonga mbele.
hapo ndo kilipo kibarua.kwa kawaida viongozi wa kiafrika wanapenda kuwa watawala wa kiimla na hawataki mabadiliko yatokee wakati wao wako madarakani.ninachokiona mama anaweza kutumia delaying tactics mpaka uchaguzi wa 2025 utakapoisha au mpaka atakapokaribia kuondoka madarakani.tuombe Mungu ampe busara mama ajitoe ufahamu ili mchakato uendelee.
 
Kumbe Katiba mpya tunayochagizana lengo ni kuitoa ccm madarakani!!?
Hiyo sio lenga bali ni matokeo. Nakukumbusha tu kama katiba haitaitoa CCM basi ni kupoteza muda. Maana yake utakuwa na katiba bila serikali yenye utashi wa kuisimamia. CCM hata katiba iliyopo na ubovu wake hawaisimamii.
Prof.Assad aliwahi kusema Katiba mpya ni sawa ila kuisimamia ni jambo lingine
 
Mpaka sasa Prof. Rwekaza Mukandala anaongea mengi ya kubana zaidi vyama vya kisiasa badala ya kujikita katika suala la msingi la upatikanaji wa katiba mpya.

Toka maktaba :
Hadidu za rejea Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi


Msajili wa Vyama vya Siasa
https://www.orpp.go.tz › news › wa...
Wadau Waalikwa Kutoa Maoni Kikosi Kazi cha Rais

Maeneo mengine ni ushiriki wa wanawake na makundi maalumu katika siasa na demokrasia ya vyama vingi vya siasa, Elimu ya Uraia, Rushwa na
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba, 2022



Mapendekezo ya Ripoti yanasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala
  1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe, pia mikutano ya ndani ya vyama hivyo
  2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho
  3. Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote.
  4. Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri ya yeyote, na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa mahakamani
  5. Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Tanzania, akisaidiwa na jaji mkuu wa Zanzibar. Pia, nafasi itangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi
  6. Matokeo ya Rais jahojiwe Mahakamani
  7. Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria na maadili
  8. Tume ya taifa ya uchaguzi ipewe fedha kwa wakati
  9. Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote, maafisa wa uchaguzi wanaoengua wagombea bila sababu maalumu wawajibishwe
  10. Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe
  11. Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye sheria za vyama vya siasa, pia ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%
  12. Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya
  13. Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe
  14. Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia.
  15. Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi waelewe

Kama chaguzi zitaendelea kusimamiwa na DED ni kazi bure. Tume iwe na watendaji wake yenyewe kwenye ngazi zote kuanzia level ya Wilaya
 
Hivi huyo Jaji Mkuu wa kuongoza kamati ya kuteua wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, si mteule wa RaisI?

Na Rais si anatokana na chama cha siasa, chama kinachoshoriki huo uchaguzi?

Na hata matokeo ya uraisi yakihojiwa mahakamani, mahakama hizi zinaweza kutenda haki?

Hii ni janjajanya tu ya MA-CCM ila Mama ajue sisi sio wajinga .
 
Mpaka sasa Prof. Rwekaza Mukandala anaongea mengi ya kubana zaidi vyama vya kisiasa badala ya kujikita katika suala la msingi la upatikanaji wa katiba mpya.
Chama cha upinzani si kilisusia kushiriki kwenye kikosi kazi na kuviachia vyama mamluki? Hivyo usitegemee matokeo tofauti.
 
Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote.
Tumpongeze sana Profesa Mkandala kwa kazi nzuri pamoja na kikosi kazi chake kwa ujumla; ila kwenye "nukuu" hiyo hapo, Profesa anapelekea na mimi nianzishe Chama changu cha Siasa, nikamate hela ya Serikali kama itakuwa imejisahau kwa kiwango hicho.

Kwani ni sababu zipi zilizopelekea hiyo 10% ikawa haigawiwi sawa kwa vyama vyote vya Siasa? Nitaanzisha chama changu muda siyo mrefu
 
Chama cha upinzani si kilisusia kushiriki kwenye kikao kazi na kuviachia vyama mamluki? Usitegemee tofauti na hicho.

Hapo ndipo tunapoona mapungufu ya waTanzania, suala hili silo la rais wala chama cha upinzani au tabaka fulani la wananchi.

Suala hili ni la waTanzania wote haitakiwi majority wakae wamewaachia ulingoni wapo rais na wapinzani.
 
Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe, pia mikutano ya ndani ya vyama hivyo
Very WEAK statement....

Unapendekezaje kuwepo kitu ambacho tayari kisheria?!

Kikosi Kazi "Kinapendekeza Kuruhusiwa" au Kikosi Kazi "KINATAKA MIKUTANO ya hadhara iendelee" pasipo na masharti yoyote?
 
Back
Top Bottom