Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Hahahaa hata Mwl nyerere hakumuona huyo?

..Katika ma-cj na ma-ag wote kabla ya magufuli hakuna hata mmoja aliyeteuliwa toka miongoni mwa wahadhiri wa udsm.

..sidhani kama hiyo inamaanisha kwamba wahadhiri waliokuwa kitivo cha sheria hawajui sheria au ni wabovu kitaaluma.
 
Unajua kwanini shivji hajawahi kupewa nafasi yeyote serikalini ya uongozi tangu baba wa taifa mpaka anastaafu utawala wa kikwete alikua mwalimu tu?
Ya nn? Waliokuwa wanapinga serikali waliondolewa kwa zengwe, huyu alikuwa ni uma puliza tu hamna kitu
 
Teuzi!
*Hivi IGA imesainiwa kati ya Tanzania na DP World au Tanzania na Dubai?

*Kama na Dubai ni yapi majukumu ya Dubai yaliyobainishwa katika IGA? na kama ni DP World ni kwanini tulisaini IGA na Kampuni?

*Prof anasema ni vyema mara baada ya hawa DP World ni vizur akatafutwa mwekezaji mwingine akapewa eneo nyingine! Je! Prof anajua kuwa Mkataba unahusu Bandari za Bahari na Maziwa nchini Tanzania?
 
New Chawa!
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

👉🏾 Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu...
 
Unajua kila anayetoa maoni anao upande aliochagua, kwa hiyo kila anayeunga mkono au kupinga inategemea amesimama katika upande upi, lakini katika yote hatuna sababu ya msingi ya kubinafsisha Bandari yetu kwa mkataba mbovu kiasi kile, kama uwekezaji bandarini umefanyika kwa kiasi kikubwa sana, tunapaswa kujua muwekezaji anakuja na nini cha ajabu, sio kupewa bure kabisa.
Unataka na proposal ya mwekezaji ya kile atafanya iwekwe kwenye hii IGA? Sasa TPA itakuwa ya nini kama Kila kitu kitaishia IGA? Tunajitia stress zisizo na mbona wakuu.
 
Sasa ukiambiwa una uelewa mdogo kwani ni kosa?
Usinichoshe. kosa au sii kosa, hapa sio mahakamani. Kila mmoja abaki na namna yake ya kuelewa hata profesa anaweza akawa na uelewa mdogo vilevile kama yule prof wa madini ambaye hakuamka vizuri
 
..Katika ma-cj na ma-ag wote kabla ya magufuli hakuna hata mmoja aliyeteuliwa toka miongoni mwa wahadhiri wa udsm.

..sidhani kama hiyo inamaanisha kwamba wahadhiri waliokuwa kitivo cha sheria hawajui sheria au ni wabovu kitaaluma.
Hahaaha. Unayo list ya wahadhiri walioteuliwa nafasi za uongozi tangu enzi ya baba wa taifa mpaka leo?
 
Hahaaha. Unayo list ya wahadhiri walioteuliwa nafasi za uongozi tangu enzi ya baba wa taifa mpaka leo?

..kabla ya Prof.Kilangi hakuna mwanasheria mkuu wa serikali aliyeteuliwa toka miongoni mwa wahadhiri wa udsm.

..pia kabla ya Prof.Ibrahim hakuna Jaji Mkuu aliyekuwa mhadhiri udsm akaenda mahakama kuu na kuteuliwa Jaji Mkuu.

..hoja yako kwamba Prof.Shivji sio mwanasheria mbobevu kwasababu hakuwahi kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu nadhani haina mashiko.

..pia nafasi za uongozi sio serikalini tu, au kupitia uteuzi wa Raisi.
 
Pro wa uchumi anabishana na pro wa sheria kuhusu dp world, kukaa kimya nayo hekima sio kila kitu lazima ujibu .
 
S

Tofauti ya Tibaijuka na Assad ni wazi kabisa ; Tibaijuka hoja zake amezielekeza kwenye contentious terms of the contract, Assad anaelezea faida zitakazopatikana kutokana na uwekezaji vitu ambavyo hakuna mtu anabishia!
Contentious terms of the contract Prof Tibaijuka hawezi kuzifasiri maana siyo taaluma yake, ndo maana unaona ameishia kuvurunda tu, amefasiri kwa Uelewa wake wa Kiingereza na amepotosha meeengi tu
Mimi Naona ungeandaliwa mdahalo ili mbivu na mbichi zitenganishwe
 
Huyu Assad aiseee!!

Alitimuliwa huyu profesa kiazi na Magufuri
watu tukamuonea huruma na IST yake.

Ila HAKIKA Magufuri alikuwa na kitu cha ziada mno
basi hatukumuelewa!

Magufuri alikuwa ameishaona humu hakuna cha uprofesa bali ni njaa tu na ubwege

Na wote aliowatosa akina Lugola, Makanba, Nape na wengine
hapo awali tulihisi anawaonea
Kumbe hawafai hata kuwa Balozi nyumba 10/10

Huyu Assad nae kwanza anatokea Zanzibar

coz it’s like wote sasa wametuzoea mno
Kuna kitu inabidi tu kifanywe
 
Unataka na proposal ya mwekezaji ya kile atafanya iwekwe kwenye hii IGA? Sasa TPA itakuwa ya nini kama Kila kitu kitaishia IGA? Tunajitia stress zisizo na mbona wakuu.
Kwani kuna nini cha ajabu? Ambacho wananchi hawapaswi kujua?
 
Yeye ndio hana uelewa.
Pale bandari wameigawa bure
Bora hata ingeuzwa Tujue tumepata kiasi gani.
Sasa hivi hela zimeishia kwa Samia na genge lake.
Wamegawa kwa mkataba usiokuwa na kikomo.
Na ardhi watatupora ili wampatie mwarabu.
Na bandari mpaka bubu.
Na zingine ni Beach za serikali wamegawa.
 
Back
Top Bottom