Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Hakuna sehemu IGA imeandika wakifanya vizuri watapewa hayo maeneo mengine au hata mimi kuandika hivyo; hayo umeyatoa kichwani kwako tu...
Wapi kwenye mkataba huo wamesema/wameandika wakishindwa kufikia hayo malengo basi watavunja huo mkataba?
 
Actually mahali tulipofikia kwenye huu mjadala,maoni yake ni yalitegemewa kuwa haya hivyo siyo habari sana.

Wenye sugu kwenye komwe na wakata suruali huwa hawafurukuti kwa mwarabu,ni mwenzao hasa.

Kule USA mjadala wa DP World "kuuziwa" bandari zao sita ulipopamba moto 2006,House appropriations committee ilipiga kura na wajumbe 2 pekee wakawa upande wa DP huku 62 wakamkaa.

NB:Rais Bush alikuwa upande wa DP World kwa hoja ya UAE ni mshirika wetu muhimu Mashariki ya Kati.

Huku kwetu kwa huu uchawa na udini sioni watu wakitumia utashi wao hata mkipigisha watu kura.

BOTTOM LINE: Mpaka siku tutakapokuwa na sheria ya kunyonga hii kinga dhidi ya mashtaka kwa viongozi ndiyo kiburi chote kimeanzia hapo.
 
Hakuna sehemu IGA imeandika wakifanya vizuri watapewa hayo maeneo mengine au hata mimi kuandika hivyo; hayo umeyatoa kichwani kwako tu...
Huu mkataba unapigiwa debe sana sana kwani kuna nini jamen? Mbona sio kawaida ya serikali kufanya hivi?
 
Watanganyika hawana shida na muekezaji TATIZO ni vipengele hatarishi ndani ya mkataba. Rekebisheni mkataba mchape kazi
 
Huu mkataba unapigiwa debe sana sana kwani kuna nini jamen? Mbona sio kawaida ya serikali kufanya hivi?
Una faida kubwa sana kwa Tanzania, hata mimi nilikuwa against it maana sikuona tija ukizingatia serikali ilikuwa imeongeza kina cha kupokea meli kubwa na washaanza kununua baadhi ya cranes; so nikaona hawa waarabu wanakuja kufanya nini zaidi ya kuvuna tu kwa jasho la watanzania.

Hila nilipoona mkataba, kusoma taratibu na maeneo ya uwekezaji nikawavulia kofia waarabu. Strategically wamefikiria mbele sana in terms of smooth flow ya logistic za ndani with the anticipation of future cargo volumes increase.

Jamaa wameonyesha wao sio tia maji tia maji kabisa kwenye hiyo industry in terms of strategic planning.
 
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

👉🏾 Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu...
Ni lini mhasibu akafanya mikataba?Tuwaheshimu wana sheria huyu ni muhasimu na ndiyo maana watu walimuomba mwanasheria mkuu aelezee!

Pili kama anayosema ni kweli basi mkataba kama wa DP world ndiyo tungeuona nchi nyingine! tatizo mikataba mingine ya nchi kwa wataalamu walioangalia haina haya madudu
 
Mwabukusi said" this is a binding contract kwamba IGA ndio foundation ya mikataba midogomidogo itakayosainiwa baadae na serikali ikiwa kama umezingua kwenye IGA hautaweza kurekebisha kitu" mwsho
 
Mwabukusi said" this is a binding contract kwamba IGA ndio foundation ya mikataba midogomidogo itakayosainiwa baadae na serikali ikiwa kama umezingua kwenye IGA hautaweza kurekebisha kitu" mwsho
Sio IGA tu sheria yoyote inayopitishwa na bunge hata za ndani baadhi ya vipengele vyake ni sehemu ya mkataba (wanaita ‘implied terms by law).

But laws don’t cover all contract terms and clauses, some are expressed especially considerations; they occur after direct negotiations na hayo bado kwa sababu ni mambo ya project agreements; hao watu wanapotosha tu umma.
 
Hivi chama kilichotuingiza kingi kwenye makinikia si hawa hawa mbwa wa ccm! Lisu,akasemaje vile? Ni professorial rubbish! Wakaja juu, juzi ukweli umejurikana.

Namkubali sana Prof, lakini sina Imani na ccm, hawajawahi, kuwa, na, jema,
Walioongelea swala la bandari ni wanasheria, tena nguli, huyu Assad ni mchumi tu, ukiona mkataba unakuwa na tafsiri nyingi, ambiguities kibao, jua kuna shida.

Sasa Prof atuambie, kama huu mkataba ni mtamu na hauna shida kabisa, umeandikwa na maraika, kwanini ccm waliukimbiza bungeni, kwanza ulidhiwe, harafu ndio tutoe maoni tena kwa siku moja!

Na utamu wote wa huu mkataba, kwanini Zenj, hawataki hata kuusikia?

Mzee Assad, alisema mengi mabovu tena ya ukweli kuhusu utawala wa, Shetani Maghu, lakini kwa samia, amekaa kimya sana, au Haoni kitu kibaya?
 
Nilikuwa namsubili kwa hamu iliathibitishe

Inaweza kabda ujazaliwa mwenzio anafundisha sheria
Hajui chochote kuhusu Sheria jina lisikutishe. Kasome vitabu vyake ni philosophy tupu hana lolote
 
Elewa kwamba teuzi nyingi kabla ya kuteuliwa ujulishwa kuona kama utaridhia. Shivji ni miongoni mwa watu walio taka kujikita kwenye fani yake tu. Yeye anajua ukikutana nae atakuelezea....
Wewe umejuaje kama alijulishwa kupata uteuzi akakataa?
 
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

👉🏾 Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu...
Kwa hiyo yeye anauelewa?
 
Sio IGA tu sheria yoyote inayopitishwa na bunge hata za ndani baadhi ya vipengele vyake ni sehemu ya mkataba (wanaita ‘implied terms by law). But laws don’t cover all contract terms and clauses, some are expressed especially considerations; they occur after direct negotiations na hayo bado kwa sababu ni mambo ya project agreements; hao watu wanapotosha tu umma.
Hizo project agreements foundation zake si ndo IGA?? yan wakiwa wanatengeneza hizo agreements kwenye hyo mikataba midogomidogo si wanaangalia IGA Inasemaje??
 
Elewa kwamba teuzi nyingi kabla ya kuteuliwa ujulishwa kuona kama utaridhia. Shivji ni miongoni mwa watu walio taka kujikita kwenye fani yake tu....
Biblia yenyewe imeandikwa kiswahili lakini wengi wetu hatuielewi, itakuwa mkataba wa DP world uliojaa jargons za sheria ya mikataba?
 
Sio IGA tu sheria yoyote inayopitishwa na bunge hata za ndani baadhi ya vipengele vyake ni sehemu ya mkataba (wanaita ‘implied terms by law). But laws don’t cover all contract terms and clauses, some are expressed especially considerations; they occur after direct negotiations na hayo bado kwa sababu ni mambo ya project agreements; hao watu wanapotosha tu umma.
Bro mm sio mjuzi wa sheria lakn kwa nilivyowaelewa wanasheria ni kwamba IGA ni msingi wa kwenda kufanya project agreements na ikiwa IGA imekaa vibaya lazma uliwe.

Ndiomaana wanasheria nguli wanasema huu mkataba umekaa kitumwa coz yalipo kwenye IGA huwez kuyabadili ukiwa unatengeneza hzo pj agremnts
 
Actually mahali tulipofikia kwenye huu mjadala,maoni yake ni yalitegemewa kuwa haya hivyo siyo habari sana.

Wenye sugu kwenye komwe na wakata suruali huwa hawafurukuti kwa mwarabu,ni mwenzao hasa...
GO PROF ASSAD GOO GOOOO

1691590929432.png
 
Hizo project agreements foundation zake si ndo IGA?? yan wakiwa wanatengeneza hizo agreements kwenye hyo mikataba midogomidogo si wanaangalia IGA??
Hata sheria ya kazi ina haki za mwajiri na mwajiriwa, unapoandaa mkataba wa kazi ndani ya Tanzania lazima uweke hizo terms zilizotajwa ndani ya sheria (hata usipoziweka mahakama inazitambua).

Lakini unapopata kazi kwenye mkataba kuna terms zingine ambazo hazipo kwenye sheria mfano masaa ya kazi, mshahara, performance bonuses, termination processes za mkataba wa kazi, muda wa mkataba wako (permanent or temporary). Hayo ni expressed au negotiated kati ya mwajiri na mwajiriwa lakini hayapo kwenye sheria, mnajadiliana kwanza halafu na yenyewe yanaongezwa kwenye mkataba.

Same IGA ina cover sehemu ya terms za mikataba ya baadae na hata isipowekwa kwenye project agreements ni terms tayari kwa sababu IGA ni sheria; that’s the whole point of parliamentary ratification.

Kwa hivyo IGA kama ilivyo sheria ya kazi haina terms zote na ndio tumeelezwa mengine kama ya muda, performance measurement agreements, etc with consideration yatakuwa kwenye ‘project agreements’ baada ya kukaa chini kupigiana mahesabu na hatua hizo bado.

Kwa kifupi sheria zote za administrative law zinazopitishwa na bunge ni implied terms kwa mikataba inayohusu hizo sector. Sio IGA tu.
 
Basi
Magufuri mengi sana tunaamini yalikuwa sababu ya kusogezwa kwa Baba
Huenda hata huu mkataba tu waliona hawezi kutoboa mbele zake ila tu asogezwe kwa Baba Muumba!

Fikiria Mwinyi aliuza Ngorongoro enzi hizo
Eti Leo ndiyo mkataba unatekelezwa!!!!!

Natamani tuamke Kesho baadhi ya watu nao wametangulia kwa Baba hasa ile Top Juu yote
 
Bro mm sio mjuzi wa sheria lakn kwa nilivyowaelewa wanasheria ni kwamba IGA ni msingi wa kwenda kufanya project agreements na ikiwa IGA imekaa vibaya lazma uliwe. Ndiomaana wanasheria nguli wanasema huu mkataba umekaa kitumwa coz yalipo kwenye IGA huwez kuyabadili ukiwa unatengeneza hzo pj agremnts
IGA ime cover basic terms tu za kulinda uwekezaji (ambazo ni complete terms) na kuna maelezo ya taratibu ya kuingia mikataba ya baadae. Maelezo ambayo yanahitaji makubaliano mengine hizo ndio zitakuwa expressed terms zenye kuongelea issue za consideration, huko bado.

Hao watu wanapiga porojo tu, kutisha jamii na kutunga uongo; mengine wanayoongea hayapo kwenye IGA wala hakuna hayo madhara as yet.

Uwezi kuwa na mkataba wa biashara kama aulezi A anatoa nini na B anarudisha nini in measurable gain wanaita ‘consideration’ kwenye mkataba. IGA aina hayo maelezo na auwezi mshitaki mtu mahakama yoyote duniani bila ya hizo information ndio maana hiyo IGA sio commercial contract kwa hapo ilipo.
 
Back
Top Bottom