Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi.
Binafsi sijui hizo takwimu amezipata wapi za kua vichaa tu ndio wananunua ndege kwa pesa tasilimu ama cash.
Utafiti unaojulikana Duniani kote uliofanywa na Chase & Associate unaonyesha kua ndege zote za biashara 73% hununuliwa kwa cash ama wanaita outright purchase. Je, wote hao 73% ni vichaa? Ama profesa ndie ana akili kuwazidi?
Profesa anataka kuaminisha umma kua njia pekee na ya lazima ya kununua ndege ni kwa mkopo, kwa cash unakua kichaa, hivi huyu jamaa ana akili kweli?
Profesa ameongea kama mtu ambae hakwenda shule, profesa analazimisha mtazamo wake ndio uwe mtazamo wa watu wote.
Nilikua namkubali profesa lakini hii la ku-personalize tofauti zake na Magufuli na kumshambulia marehemu kua ni kichaa tena kwa mtazamo wake binafsi imesababisha nimemuondoa akili profesa Assad.