Habari Wote.
Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.
Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.
Imetokewa na,
Ofisi ya Mawasiliano
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani. Lori iliacha njia na kuilalia gari ya Ngowi. Alitoka kwenye ajali akiwa majeruhi, amefariki akiwa hospitali
View attachment 2166709
Pia soma >
Dkt. Honest Ngowi aichambua sekta ya gesi na kukiri Serikali imejipanga