TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

Nimesikitika sana. Huyu prof alikuwa very active. Tumepoteza msomi mahiri kabisa.
 
Duh,kumbe ndo ajali hiyo ,kuanzia madafu mpaka mlandizi kulikua na bonge la folebi,tukachepukia old morogoro road,.Apumzike mahala pema
 
R.I.P

Hii barabara isipotanuliwa na kuweka dual carriage way tutaisha sana kwa kweli lawama tutawapa sana madereva lakini ukweli tuuseme barabara hii ni bado ya kizamani hailingani na matumizi ya idadi ya magari iliyopo sasa.

Wanasiasa hebu tumieni hicho kiwango cha posho zenu kuokoa maisha ya watu kwa ajali ambazo huenda zingeepukika.

Hivi nchi mnazoenda kutembelea hamjifunzi tu kitu cha kufanya?

Oneni aibu kwa kuchelewa kujenga dual carriage way ya dar to morogoro tunazidiwa na nchi kama Zambia kweli?

Hadi iue wanasiasa wao wawili watatu hivi ndio wataamka na kufikiria
 
Dah! Mwalimu wangu ulikua zaidi ya ndugu kweli kazi yake Mola haina makosa
Kwa mara ya kwanza kuonana naye ilikuwa wiki juzi pale Mzumbe University Dar Es Salaam Campus, tokana na physical appearance psychology alikuwa ni mtu mwenye hekima sana.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe milele amina [emoji26]
 
Nimesikitika sana. Huyu prof alikuwa very active. Tumepoteza msomi mahiri kabisa.
Hata mimi nimewahi kushirikiana naye kuandika paper kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara. Alikuwa ni kijana wa shughuli nyingi.
Niseme tu kwa wale ambao wanasafiri mara nyingi wanatakiwa kuzingatia mambo matatu:
1.Kila safari ni mpya, usitumie uzoefu wako wa barabara husika.
2.Unayeendeshwa, una haki ya kumdhibiti dereva wako kuhusu mwendo na kufuata sheria; pia kumwangalia dereva mwanzoni kabisa kama yuko hali nzuri hata unavyomwangalia, kachoka au vipi?
3. Katika ratiba ya siku husika, jipe muda wa kutosha wa safari; hakuna haraka inayokufanya usifuate sheria na kanuni za barabara.
Mimi nimefuata sheria hizo tatu nimeishi; mara 2 nimewahi gundua dereva anasinzia anapoendesha! Nikamsimamisha.
Baada ya hadhari hizo, ulinzi mwingine mwachie Mungu.
Pole Prof. pole familia, jumuiya ya Chuo na Watanzania; tumemkosa mtu mwema na dereva wake. RIP.
 
Back
Top Bottom