TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

Hata mimi nimewahi kushirikiana naye kuandika paper kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara. Alikuwa ni kijana wa shughuli nyingi.
Niseme tu kwa wale ambao wanasafiri mara nyingi wanatakiwa kuzingatia mambo matatu:
1.Kila safari ni mpya, usitumie uzoefu wako wa barabara husika.
2.Unayeendeshwa, una haki ya kumdhibiti dereva wako kuhusu mwendo na kufuata sheria; pia kumwangalia dereva mwanzoni kabisa kama yuko hali nzuri hata unavyomwangalia, kachoka au vipi?
3. Katika ratiba ya siku husika, jipe muda wa kutosha wa safari; hakuna haraka inayokufanya usifuate sheria na kanuni za barabara.
Mimi nimefuata sheria hizo tatu nimeishi; mara 2 nimewahi gundua dereva anasinzia anapoendesha! Nikamsimamisha.
Baada ya hadhari hizo, ulinzi mwingine mwachie Mungu.
Pole Prof. pole familia, jumuiya ya Chuo na Watanzania; tumemkosa mtu mwema na dereva wake. RIP.
Ni Kweli kabisa unaeza kuzingatia hayoo, lkn likatokea jitu lingine huko kama hilo Lori kaacha njia kakufuata upande wa pili!lkn ww unakua lbd ktk mwendo wako mzuri tuu na umakini sana lkn ghafla mtu anahama kwake!!naona ulinzi wote tumuachie MUNGU tuu
 
Nchi yetu imepoteza profesa wa mfano wa kuigwa, alikuwa na mguso mpana ktk jamii kwa kupitia fani aliyosoma.

CLINIC YA UJASIRIAMALI YA Prof. NGOWI EPISODE 3
Prof. Ngowi amshauri kijana muuza maji huko katika mji wa Somanga Kilwa, mkoani Lindi, kuhakikisha anatumia kipato anachokipata kuwekeza kwenye miradi ambayo hata umri ukienda na nguvu zikiisha ataweza kuifanya bila kutumia nguvu. Source : ngowi tv
Hakuwa mchoyo kusambaza elimu aliyoipata, alikuwa anatumia media platform zote kuifikia jamii nje ya Mzumbe University Morogoro Tanzania.

Hakika profesa Honest Ngowi namlinganisha na maprofesa wa nchi zilizoendelea ambao walijitoa elimu yaliojifunza iwafikie wengi.

Ukiingia mfano ktk mtandao wa YouTube ni ngumu kuwaona maprofesa wa kiTanzania wakisambaza elimu huria hata kwa kile kiwango cha maprofesa wa waliopo Kenya, South Africa au Nigeria wanavyofanya.

Maprofesa wa nchini Tanzania wanajificha ktk "vilinge" vya madarasa au lecture rooms za vyuo vikuu utafikiri wasomi hawa ni mithili ya "waganga wa kienyeji" wasiotaka jamii kunufaika na ujuzi wao kwa kuwa mbali ktk vilinge vyao vyenye kutisha vya kazi ya uganga wa kienyeji.

Tangulia profesa mzalendo uliyeamini kuwa usomi siyo kutundika vyeti ktk kuta za majengo, nyumba na ofisi bali ulifuata wito kuwa elimu inapaswa kuigusa jamii pana hata iliyo nje ya majengo ya vyuo vya elimu ya juu ili kuleta mguso mpana na maendeleo ya watu endelevu popote walipo.

RIP Prof. Honest Ngowi .
 
Rudia kusoma uzi upya, tena kuwa makini sana maana watu kama ninyi ndiyo hupelekea kusaini mikataba mibovu sababu ya uvivu tu wa kusoma kwa kina habari husika.
Inna Lilah Waina lllah Raj'un Mzumbe University wamepoteza jembe Prof' Ngowi alikua tofauti sana na Maprof wengine alikua hana makuu kwa mtu yoyote mwenye elimu na asiye na elimu
 
Very sad ,nilikuwa namuonaga Kwa itv ila Leo habari yake inasikitisha ,Mwenyezi Mungu awapumzishe Kwa aman,polen Kwa familia
 
Hata mimi nimewahi kushirikiana naye kuandika paper kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara. Alikuwa ni kijana wa shughuli nyingi.
Niseme tu kwa wale ambao wanasafiri mara nyingi wanatakiwa kuzingatia mambo matatu...
Dereva,ana husikaje hapo?
 
Hii ni habari mbaya,Pole kwa Familia yote na Tanzania kwa ujumla,alikuwa mwanataaluma mzuri.
RIP
 
Inasemekana gari yake imedondokewa na gari iliyobeba kontena Morogoro

Mara nyingi Prof amekuwa mchambuzi wa uchumi Tanzania kwenye vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom