Hata mimi nimewahi kushirikiana naye kuandika paper kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara. Alikuwa ni kijana wa shughuli nyingi.
Niseme tu kwa wale ambao wanasafiri mara nyingi wanatakiwa kuzingatia mambo matatu:
1.Kila safari ni mpya, usitumie uzoefu wako wa barabara husika.
2.Unayeendeshwa, una haki ya kumdhibiti dereva wako kuhusu mwendo na kufuata sheria; pia kumwangalia dereva mwanzoni kabisa kama yuko hali nzuri hata unavyomwangalia, kachoka au vipi?
3. Katika ratiba ya siku husika, jipe muda wa kutosha wa safari; hakuna haraka inayokufanya usifuate sheria na kanuni za barabara.
Mimi nimefuata sheria hizo tatu nimeishi; mara 2 nimewahi gundua dereva anasinzia anapoendesha! Nikamsimamisha.
Baada ya hadhari hizo, ulinzi mwingine mwachie Mungu.
Pole Prof. pole familia, jumuiya ya Chuo na Watanzania; tumemkosa mtu mwema na dereva wake. RIP.