Profesa Ndalichako: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala

Profesa Ndalichako: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala

Dikteta Magufuli ameondolewa kwa nguvu

So kwako unaona Sawa mwanafunzi kupata mimba. Huyu Mtoto kumlea Mtoto mwenzake. Badala ya kutafuta mbinu za kuwasaidia wajitambue. Mnakimbilia short Kati. Mbona hawa wazungu hatuwaoni wakipata ujauzito mashuleni.
 
Moja ya masharti ya ule msaada toka WB, hapakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubali, nyie mnaopinga mjue serikali inahitaji zile pesa za WB bora muwe wapole tu.
Wanasiasa walivyowanafiki (wabunge)utasikia tena wanaipongeza serikali wakati kipindi kile cha meko, walikataa kabisa hadi wengi wakamuita zitto kuwa ni adui wa taifa!!anatakiwa kuuawa, baada ya WB, kugoma kutoa pesa!!
 
Hii si sawa kulingana na kizazi tulichonacho,km ni mpango uwe mpango haswa,vngnevyo hii issue itaharibu wanafunzi kwani inawafanya wasiwe na cha kupoteza,u boyfrend na u girlfrend utatamalaki mashuleni...
U boyfriend na u girlfriend havijawahi kupungua kwa sababu ya kuogopa mimba, haya mambo huwa yapo tu na mimba hutokea kama ajali kazini. Sema labda abortions zitapungua kwa kiasi fulani lakini lifestyle ya wanafunzi haitobadilika.
 
So kwako unaona Sawa mwanafunzi kupata mimba. Huyu Mtoto kumlea Mtoto mwenzake. Badala ya kutafuta mbinu za kuwasaidia wajitambue. Mnakimbilia short Kati. Mbona hawa wazungu hatuwaoni wakipata ujauzito mashuleni.
Wakiwa wanaabort unakuwaga wapi sasa
 
Wazee wa legacy watapinga sanaa[emoji3][emoji3].
Walakini tumeshuhudia mabinti wengi waliozaa utotoni na kuibuka kuwa wasomi wakubwa kabisa.
Fursa yao ilikatwa sijui kwa manufaa ya nani.
Wote tunajua wanafunzi wanavojihusisha na ngono huko mashuleni ila wale wanaokuwa na bahati mbaya hupata mimba na kushindwa kuendelea na masomo.
Unakuta kident kipanga kinamaliza shule salama kwasababu tu kinajua njia nyingi za kuepuka mimba.

Lakini tusisahau wanaobakwa au kurubuniwa na wanaume waroho wa ngono. Kwanini tulikosa moyo wa ubinadamu ? Kwanini hatukumfikiria huyu binti aliyebakwa na hatimae kupata ujauzito,,, nasisi eti tukamzawadia kumyima elimu????[emoji24]

Watoto hawa kuwanyima fursa ya elimu kwa kigezo cha mimba ni uonevu mkubwa.

Ila waliokulia mijeredi hawajawai kuappreciate maisha yenye uhuru
 
Moja ya masharti ya ule msaada toka WB, hapakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubali, nyie mnaopinga mjue serikali inahitaji zile pesa za WB bora muwe wapole tu.
Halafu watu wanasahu kuwa tumesaini protocol kuhusu haya maswala.
 
Soma vizuri maelezo ya Waziri.

Hawa watoto wahanga wa mimba za utotoni, wanaandaliwa utaratibu wa kuwawezesha kurudi masomoni baada ya kuzaa. Mpaka tuone huo utaratibu, ndiyo tunaweza kujua faida na hasara zake.

Kilicho muhimu, ni kuwa baada ua hao watoto kupatwa na janga la mimba, wanapata elimu.
Kupata elimu ni haki ya mtoto, lakini mpaka sasa serikali haina shule za kutosha kusomesha wote, wengi hukosa nafasi kuendelea na masomo kwa kukosa nafasi. Aliepata nafasi na akaamua kuingia kwenye uzazi ameona elimu kwake haifai, uamuzi wake uheshimiwe, nafasi yake wapo wanaoihitaji. Hata kufanya kazi ni haki ya raia, akikiuka sheria za kazi anafukuzwa. Hakuna kanuni na sheria kwa mwanafunzi? Kuzitekeleza si kukiuka haki yake.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Magufuli ndo aliharibu Mambo,mwanafunzi akiwa mjamzito ana haki kupata elimu Kama wale ambao sio wajawazito!ELIMU NI HAKI YA KILA MTU!

Ila Sheria zimuangalie kwa hurumamwanaume anayepiga mimba,miaka 30😲😲😲,mama wa mtoto akiendelea kula Bata uraiani na vidume vingine😔😔😔
 
Ni nchi ya ajabu sana maana kama principal Act inatamka wazi kuwa kumpatia ujauzito mwanafunzi ni kosa jinai inakuwaje waziri mwenye dhamana anaruhusu impliedly?

Kifungu cha 60A(3) cha sheria ya elimu hapa nchini kimetamka wazi kuwa ni kosa la jinai kumpa mwanafunzi mimb na adhabu yake ni miaka 30. Sasa waziri untamka hadarani kuwa unaandaa mpango kamabe ili watoto wataopata mimba kuendelea na masomo kwa njia mbadala una maana gani? Kuwa wawe wanapata mimba makusudi ili baadae wafanye mitihani na kuendelea?

Kukosa hekima na busara ya kutegegelea misaada midogo midogo toka kwa wazungu ndio sababu ya kutosimamia sheria?

Leo hii pamoja na sheria kuwa kali lakini mimba za utotoni ni tatizo,je ulivyowapa hii ruhusa si nusu ya wanafunzi wa kike watapata ujauzito wakijua wataendelae kusoma.

Tusiendekeze njaa kwa misaada ambayo haina tija. Kuruhusu mimba za utotoni kisa utajengewa choo huku mabil yakitafunwa na wajanja wachache.
 
Ujinga ujinga tu kusomesha wajawazito na wazazi,ilipokuwepo sheria ya kuwafukuza shule,kwanza wazazi walikuwa makini kuwalinda binti zao,wanajua usumbufu watakaoupata binti akigundulika mjamzito!!kwa utaratibu huu ni sawa na kuruhusu ngono kwa wanafunzi ajali ikitokea njia mbadala ya kuendelea na masomo ipo stupid [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
 
Back
Top Bottom