Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Jiulize alikua marekani muda mrefu halafu kaja jana wanasema ameteua, tena majina yametoka bado akiwa uwanja wa ndege anashangilia kurudi kwake.

Mbaya zaidi wanasema aliteua alhamisi siku ambayo alikua anahutubia UN.

Yule wanampa tu anasaini basi.

Mtu akisema Urais ni taasisi huwa unaelewaje mkuu ?
 
Kama kweli kilichoelezwa na mtoa mada, basi tambua kuwa kuna mgongano wa kimaslahi hapo. Mwanzilishi wa Rex Attorneys inayoishitaki Tanesco kwa niaba ya makampuni mengine akawe Board member wa Tanesco? Huitaji shahada kujua nini kinaendelea.

Refer; Waziri wa Uchukuzi anayeisimamia ATC kuwa Board member na shareholder wa Precision Air, nini kilitokea?
 
Huyu bibi huwa hata hausiki kwenye teuzi, yeye kazi yake ni kusaini tu, nadhani ingekuwa vyema angejiuzulu kabisa maana hakuna kitu cha maana anafanya
Wengi ya watu wanaoingia kwenye teuzi sasa ni watu wa kipindi cha Kikwetena wengi wana makandokando kibao. Makucha halisi yanaanza kuchomoza sasa na ufisadi unarudi upya.
 
Nimekupata
 
Ukifuatilia kwenye mitaa ya Twitter huyo Prof wamempiga spana vizuri wakitoa na mifano hai ya S.O.Es zinazoendeshwa kibiashara zinavyofanya vizuri kwa huduma na biashara
Haiwezi kutokea hapa, kwanza ibinafsishe ndo iendeshwe kibiashara, kinyume na hapo, ni utaratibu tu wa kuwapiga waTz.

Hakuna shirika litakalomilikiwa kwa 100% na serikali lenye machineries kubwa kubwa likaweza kujiendesha kibiashara, HAKUNA.
 
Utawala wa Trump ulijaa ufisadi ndio maana hakuchaguliwa tena mara ya pili na bunge lilimu impeach.

Wananchi walio wengi wakiamua kumchagua yoyote kupitia uchaguzi huru kuwa Rais wao hakuna tatizo, hata akiwa na "faili Mirembe".
Sawa kiongozi!
 
Kwani kuna sheria yeyote inayowabana Private Sector players kutokushiriki kwenye Bodies za Umma?
Pengine ni these very players can bring about changes that are desperately required to improve the situations?
One may or can ask, who is Prof Shivji as a private citizen to ask the Government?
 
Hii ni very weak point,wataalanu wa biashara ni muhimu sana kuwndesha asasi za umma kwani wanaingiza utaalamu mkubwa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Tanesco haiwezi kuendeshwa kibiashara ata siku moja.Hili ni shirika la serikali, labda liuzwe ndo liendeshwe kiabiashara. Yaani akili za kuambiwa wewe mwezi wa kwanza uchanganye na za kwako. Labda kama team mwezi wa kwanza wanataka kununua shares tu wamiliki Tanesco. Waseme tu hii mbinu ya Tanesco kuendeshwa kibiashara ndo wanatumia kufikia malengo ya kuuza shirika. Baada ya hapo ni SGR , ....na wa mwisho kuuzwa ni Mtanzania. Yale yale ya awamu ya nne
 
Kama mkurugenz mkuu alikua ni engineer na shirika lilipata hasara basi ni vizuri tukajaribu pia kuweka na wafanyabiashara tuone hali itakuaje..
Weka yoyote yule, kama bado ni 100% owned by Gov, watakachofanya hao wafanyabiashara ni kuanzisha au kukuza biashara zao kupitia shirika hilo na HILO ndo lengo mpaka sasa, KUPIGA. Serikalini hakuna discipline na kuchukuliana hatua, ukiiba hapa unahamishiwa kule.
 
Sikuwahi na Sitowahi mkubali JPM hata Mama azingue vipi!! Sera zake zilikua zinaenda kuzika uchumi wa TZ by 2025!
Hata Mnyika aliwahi kumtusi sana JK ila juzi juzi tu hapa alikuwa anamwita JK jembe
 
Mkuu chain inaanzia juu kabisa
Nadhani unakumbuka kipindi Cha Dowans, Maajar anaishauri Tanesco kuvunja mkataba na Dowans huku akiwa sehemu ya dowans. Unafikiri waziri na raisi hawakuwepo?
Ndio maana nikahoji mbona hata mawaziri ni share holders wa baadhi ya kampuni huko private sector ila hawazuiwi kuwa mawaziri/wabunge??

Ndio maana nimeuliza ni wakati gani unachora mstari wa private sector na public sector ilihali waliopo public sector zaidi ya 50% wanamiliki biashara/investments/hisa huku uraiani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…