#COVID19 Propaganda za Chanjo ya COVID-19: Askofu Gwajima apuuzwe
Gwajima ("Askofu" sio "Daktari")ni anti-Mrna vaccine au ni anti-vaxx in general?
 
Pumbavu kabisa, hapo ulipo umejaa makovu ya chanjo za surua, ndui, TB na polio u ulizochanjwa na mama yako kabla akili yako haijajaa matope.
Na yeye mwenyewe au wazazi wake wali sainishwa kwamba ikitokea matope ni juu yao
 
Mimi si mshabiki wa Askofu Gwajima. Lakini nakubaliana naye kwa ishu ya chanjo. Ni mtu mjinga pekee ndio anaweza kubali Chanjo.

Mungu hakosei kuhusu immunity aliyomuumba nayo mtu. Why chanjo now?
Na hizo chanjo nyingine, vipi au unadhani ipo hii tu.
 
Mimi nimesikia anauliza na kujijibu
1.nikichanja navaa barakoa?..ndio
2.nikichanja naweza kuambiza?...ndio
3.nikichanjwa naweza kuambukizwa?...ndio
4.sasa nachanjwa ili iweje?
Jamaa ni kichwa
 
Copy and paste
Kutoka fb

Wapendwa. Hii habari ya corona ni ngumu. Binafsi sina mashaka na wanasayansi na ndiomaana nilikwenda kupata chanjo siku ya kwanza. Mimi na familia yangu tumechanja. Mimi na mke pia watoto wetu wawili. Wale wa chini ya mmoja wa chini ya 18 atasubiri. Kabla ya kuchanjwa tulijiuliza na kusoma tafiti toka vyanzo vinavyoaminika kama reports za who, Muhas, Nyaraka za wizara ya afya nk. Na maswali yafuatayo:
1. Wazungu wanania ya kuangamiza wa afrika? Jibu: Hakuna ushahidi.

2. Serikali ya Tz imedhamilia kuangamiza watu wake? Jibu: hapana.

3. Je, kuna ushahidi wowote unaoonyesha wazungu waliwahi kuangamiza kizazi cha watu wen ye umri 50+? Jibu: Hapana ila ushahidi ni kwamba kwenye Biblia kama kuangamiza ni umri kuanzia miaka 0 - 2(rejea amri ya Herode na Farao).

4. Je, watz wa naogopa corona au chanjo ya corona? Jibu: chanjo.

5.Je, wa Tanzania ni waumini wa tafiti za kisayansi au maneno ya wahubiri na watabiri? Jibu: watz wa naamini kikombe cha babu wa Loliondo kuliko madaktari bingwa wa Muhimili au Mkapa.

5.Je, nafasi ya kufikiri kwa mtz(reasoning) ni % ngapi? Jibu:Hilo wanamwachia Mwamposa na Gwajima mfufua wafu.

Baada ya kujiridhisha na haya nimekubali kuwa sehemu ya watu wanaounga mkono chanjo na imani hii inachorewa mstari na ushahidi kwamba vituo vya tafiti duniani kwa sasa havihusishi Taifa moja bali wasomi toka kona zote za dunia.
 
Gwajima aheshimiwe na watu wote, tayari Ana cash kubindoni ya kununua treni ya umeme[emoji586].

Tena wananchi wote wa Kawe atawapeleka Marekani na kila mwananchi atamnunulia boat [emoji569] ya kisasa ya uvuvi
Kwani wale waliopo Birmingham (Marekani) wanasemaje?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
  • Kicheko
Reactions: Dua
Gwajima ameokoka "amempa Yesu maisha yake " na kwa imani ya Walio okoka Yesu naponya kila kitu pale unapo omba kwa imani.
HivyoGwajima amezungumza kwa imani na yupo sahihi kwakuwa Biblia yao inasema hivyo, kuwa na imani utapona.

Sema tu kosa la Gwajima ni YUPO PALE KWA WIZI WA KURA.

Vipi wananchi wa Kawe wameshafika Birmingham?
Vyuo vya uvuvi vimeshafunguliwa Kawe?
Na vipi?
Kama mtu aliiba kura wakati wizi ni dhambi je hawezi kuongea uongo?!
 
  • Kicheko
Reactions: Dua
Gwajima asikilizwe, ajibiwe kwa hoja, kumpuuza Gwajima ni Upuuzi.

Gwajima ana hoja nzito sana ajibiwe kitaalamu.
Unaweza kujibu hoja ya kwanini korona haikuja miaka 10 tanzania ndo ije saivi baada ya JPM kufa unaweza kujibu swali la hivyo kwa mtu mwenye PhD ya theology ..??
 
Mbona hamkusema kuwa Magufuli apuuzwe?
 
wakuu hope mko sawa,

baada ya Corona kuibuka kumekua na sintofahamu nchini na sintofahamu hii imeibuka mara baada ya watu fulani kututaka tuwapuuze wanasayansi kwani wanataka kutuangamiza kupitia ugonjwa huu na hivyo tutumie njia zetu za asili, ,


mabishano yaliyopo sasaivi ni kuhusu mtazamo wa chanjo ya korona je ni salama au sio salama je inafaa au haifai?

hapa kuna pande mbili upande wa wataalamu wa Afya ambao kwa sasa wanatuhimiza tupate chanjo na upande wa wengine wasio na elimu maalum ambao wanapinga chanjo,

nimejaribu kufuatilia tafiti za wale wanaopinga chanjo ili nione kama ninaweza kujifunza chochote ili nichukue maamuzi sahihi, moja ya watu waliokua wakipinga chanjo ni mpendwa wetu hayati dokta John joseph pombe magufuli shujaa, Mungu amlaze mahali pema!

Dkt JPM alipinga chanjo na kusema hazina nia njema kwetu na akaamua kufanya tafiti nyingine yeye kama yeye na akagundua kwamba Kirusi cha korona ni futa hivyo ukijifukiza kwa mvuke wa above 100° hilo futa linapasuka na ndio unakua umepona, maneno hayo aliyasema wakati akiongea na vyombo vya ulinzi na usalama nyumbani kwake chato,


hivyo kupitia utafiti wake huo akasisitiza sana tujifukize na tutumie dawa ya bupiji ambayo inaondoa kovid

mwingine ni Dkt Josephat gwajima yeye kupitia itafiti wake nguli akagundua sabuni za Amfifiro zinazuia korona hivyo tutumie sana sabuni za Amfifiro kupambana na korona, na pia aliomba kibali serikalini akaombee wagonjwa wote wa kovid watapona, tunaomba serikali impe kibali ili tupone na janga hili,



wakuu je, tutumie chanjo au tufuate njia za wataalamu wetu hawa waliofanya tafiti za kujitegemea?

bado tupo njia panda

 
Yoshua 10:21ndipo hao watu wote wakamrudia Yoshua maragoni huko Makeda salama; hakuna mtu awaye yote aliyetoa ulimi kinyume cha hao wana wa Israeli.

Mimegundua niliposoma Biblia kwamba Askofu Gwajima anakwenda kinyume na mafundisho ya Biblia.
Unaona jinsi ambavyo kwamba hakuna mtu aliongea maneno mabaya kuhusu Wana wa Israel.

Sasa kwa nini yeye anakwenda kinyume na maagizo ya serikali kuhusu corona?.
 
Yoshua 10:21ndipo hao watu wote wakamrudia Yoshua maragoni huko Makeda salama; hakuna mtu awaye yote aliyetoa ulimi kinyume cha hao wana wa Israeli.

Mimegundua niliposoma Biblia kwamba Askofu Gwajima anakwenda kinyume na mafundisho ya Biblia.
Unaona jinsi ambavyo kwamba hakuna mtu aliongea maneno mabaya kuhusu Wana wa Israel.

Sasa kwa nini yeye anakwenda kinyume na maagizo ya serikali kuhusu corona?.
gwajima anapendaga tu ajadiliwe, hakuna zaidi ya hapo
 
Mungu anasema anataka kuipa fundisho taasisi fulani. Sijui ni taasisi gani hiyo.
 
Back
Top Bottom