#COVID19 Propaganda za Chanjo ya COVID-19: Askofu Gwajima apuuzwe
Mkuu naweza kukubaliana na wewe, lakini kwenye mstari wa mwisho hapana. Kweli Mungu katuumba na immunity, lakini kama unadhani immunity tuliyoumbwa nayo inatosha, Je kwa nini tunaugua na wewe mwenzetu hujawahi kabisa kuchanjwa? Nadhani tusitumie kigezo cha immunity tuliyoumbwa nayo kutosha bali tubaki na hoja ya chanjo ya corona
Swali moja tu...je,hujawahi kuchanjwa tangu uzaliwe?
Jibu kaa nalo tu. Silihitaji.
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha...
Serikali inajiridhisha kwa kutumia nini? Hawa madakitari wetu wanafanya nini kama chanjo tunatoa nje? Baadhi ya magonjwa unaambiwa uende India, UK na kwingineko,sasa tuna madakitari gani? Tuna engineers hapa nchini lakini kutwa kucha barabara zetu zinachongwa na wachina.

J Gwajima yuko sahihi kabisa
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha...
Inawezekana kumpuuza gwajima ikawezekana lakini itapendeza zaidi hoja na maswali yake pia yangejibiwa ili watanzania wanaoamini hoja zake waelewe vizuri
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha...
Hatumpuuzi sasa, kwenye swala la corona kila mmoja ni mtalaam, sote tumejifunza corona.
 
Kuna wale wahubiri Mapendo na Kuombeana uzima.... ila pale wanapowaambia watu kwamba Chanjo zitawaua na kuendesha harakati za kutisha wale waliochanja tuwaelewe vipi?, Kwamba ni Wauwaji wa Kutumia Hofu au?

Je Hawajui kwa kufanya kwao hivyo wanaweza kuwauwa waliochanja kwa hofu?

Tuwaelewe vipi Hawa watu ? Badala ya kuleta amani wanaleta taharuki. Kwahio ndugu kama hio ni tabia yako kabla ya kutisha watu (kwa mujibu wa imani yako ukidhani unawaokoa watu) unaweza kuwa unawamaliza kwa hofu.
 
Chakushangaza wanadhani Dunia hii ni ya wakrito tu, mbona wenye imani zingine hawatutishi namna hiyo! Ninachoamini Mimi corona ni vita ya kiuchumi na wala si imani za 666!
 
Hawajatisha watu, ila wanaeleza wasiwasi wao, maana ni ukweli usiopingika hakuna daktari au virologist anayewaze kujua short term and long term side effects za chanjo ya Corona.

Wewe Kama umelikoroga tayari endelea kulinywa
 
Hakuna mwenyewe uhakika uko mbele kitakuja kutokea nini juu ya chanjo.

Screenshot_20210804-093123_Instagram.jpg
 
Askofu Gwajima amekua akitusisitiza tukatae chanjo ya Mzungu, kwa maana yeye anautafiti wa kutosha kuwa ina madhara,

sasa basi tunaomba atuonyeshe chanjo yake yeye kama mwanasayansi nguli atupatie chanjo yake inayoaminika ili tuitumie, maana anaposema tukatae chanjo halafu tubaki hivyo hivyo anataka tuemdelee kufa au?

gwajima wenye magonjwa sugu na wazee wamekuelewa sasa tunasubiri utuletee chanjo ili tunusulike maana unaonekana wewe ndiye mwenye akili sana kuliko wanasayansi wote duniani,

tisaidie kwa hilo
 
Uzuri mmoja!hata kama akitemwa sio mtu wa njaa, atapata mda zaidi wa kuwajenga waumini wake kiimani.
 
Enyi wana Kawe wenzangu huyu askofu Gwajima anatupeleka wapi naina kama anatupoteza?

Tuchanje au tusichanje?!

Hiyari yako inaanzia kwenye hiyari ya mwenzako vinginevyo ni lazima!

Mungu ni mwema wakati wote.
 
Anasema tusichanje anataka tumuombe Mungu, wakati yule bosi wa maombi alishaondoka na Gwajima bado hajamfufua mpaka leo, mimi namuona Gwajima kama kichaa fulani na wafuasi wake ndio wakuhurumiwa kabisa.
 
Gwajima mwenyewe ana bodyguards wa kutosha ili kuhakikisha usalama wake.
Mtu kama huyo usimuamini
 
Unaomba ushauri wa kuwekeza kwenye dhahabu kwa muuza nyama ?

Kwa Ushauri, Ushauri wa Dhahabu omba kwa Muuza Dhahabu na wa Kuhusu Nyama omba kwa Muuza Butcher...
 
Kwanza nilitamani sana huyu mtu anayejiita Askofu akamatwe na vyombo vya dola kisha ahojiwe kuhusu tabia yake ya kwenda kanisani na kwenda kuwadanganya Watanzani kua chanjo si salama wakati anajua kabisa kua kila chanjo inayotolewa na serikali imejiridhisha...
Gwajima asikilizwe, ajibiwe kwa hoja, kumpuuza Gwajima ni Upuuzi.

Gwajima ana hoja nzito sana ajibiwe kitaalamu.
 
Back
Top Bottom