wakuu hope mko sawa,
baada ya Corona kuibuka kumekua na sintofahamu nchini na sintofahamu hii imeibuka mara baada ya watu fulani kututaka tuwapuuze wanasayansi kwani wanataka kutuangamiza kupitia ugonjwa huu na hivyo tutumie njia zetu za asili, ,
mabishano yaliyopo sasaivi ni kuhusu mtazamo wa chanjo ya korona je ni salama au sio salama je inafaa au haifai?
hapa kuna pande mbili upande wa wataalamu wa Afya ambao kwa sasa wanatuhimiza tupate chanjo na upande wa wengine wasio na elimu maalum ambao wanapinga chanjo,
nimejaribu kufuatilia tafiti za wale wanaopinga chanjo ili nione kama ninaweza kujifunza chochote ili nichukue maamuzi sahihi, moja ya watu waliokua wakipinga chanjo ni mpendwa wetu hayati dokta John joseph pombe magufuli shujaa, Mungu amlaze mahali pema!
Dkt JPM alipinga chanjo na kusema hazina nia njema kwetu na akaamua kufanya tafiti nyingine yeye kama yeye na akagundua kwamba Kirusi cha korona ni futa hivyo ukijifukiza kwa mvuke wa above 100° hilo futa linapasuka na ndio unakua umepona, maneno hayo aliyasema wakati akiongea na vyombo vya ulinzi na usalama nyumbani kwake chato,
hivyo kupitia utafiti wake huo akasisitiza sana tujifukize na tutumie dawa ya bupiji ambayo inaondoa kovid
mwingine ni Dkt Josephat gwajima yeye kupitia itafiti wake nguli akagundua sabuni za Amfifiro zinazuia korona hivyo tutumie sana sabuni za Amfifiro kupambana na korona, na pia aliomba kibali serikalini akaombee wagonjwa wote wa kovid watapona, tunaomba serikali impe kibali ili tupone na janga hili,
wakuu je, tutumie chanjo au tufuate njia za wataalamu wetu hawa waliofanya tafiti za kujitegemea?
bado tupo njia panda