The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
View: https://youtu.be/Isx1OohuSwE?si=h2rmCO7VUQwe_PWb
➡️Huu ni unabii mwingine kumhusu Tundu Lissu kutoka kwa nabii aitwaye "Prophet Denis wa Tanzania...."
➡️ Nimemsikiliza na kumtazama hadi mwisho ktk video clip hiyo. Nimemwelewa na kumuamini kwa kiasi kikubwa..
➡️Anasema kuwa, Mungu ameweka kusudi lake ndani yake juu ya nchi na taifa hili la Tanganyika. Na kusudi hili Mungu atalitimiza kupitia kwake. Kifo kimezuiliwa kabisa kwake hadi kusudi hilo litimie
➡️Anaendelea kusema kuwa, si kwamba hakuna watu wengine ambao Mungu angeweza kuwatumia. Ila kwa sasa ni wakati wa Tundu Lissu...
➡️ Anasema pia kuwa, inawezekana hata yeye Tundu Lissu hajui ni kwanini anafanya baadhi ya mambo na yanafanikiwa. Ni kwa sababu kila analofanya lina nguvu (msukumo wa Mungu) na litafanikiwa..
➡️Amemaliza kwa kusema, maisha yake si marefu sana. Mara atakapokuwa ametimiza kusudi la Mungu, hapo MUNGU ataruhusu kuondoka (kufa) kwake...
➡️Kwa Sasa hakuna wa kuzuia jambo lolote atakalopanga kulifanya lenye mwelekeo wa KUTIMIZA KUSUDI HILI LA MUNGU NDANI YAKE juu ya nchi na taifa hili kwa sababu SI YEYE BALI NI MUNGU YEHOVA NDANI YAKE ANATENDA KAZI...!
##Sasa jiulize swali hili:
Kwamba, kuna binadamu au shetani gani awezaye kuzuia mipango na makusudi ya Mungu? Je, Mungu akiamua jambo fulani liwe, haliwezi kuwa...?
##Chawa wa CCM na mama Samia karibuni kwa maoni yenu..