Wewe nani alikwambia manji anatumia hayo madawa?,ulimuona au uliambiwa?Mbowe hausiki na hajawahi hata kugusa hayo madawa na kwa hili makonda atalipa. Mbowe alichafuliwa kwa makusudi kabisa.
Ila kwa majay na manji, NI KWELI Wala hawajasingiziwa.
Kosa linaloitwa matumizi mabaya ya madaraka ni gumu kulitolea ushahidi mbele mahakama ya haki bila kuonyesha kuwa alitumia madaraka hayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.
Akitumia madaraka hayo kukutisha linaweza liswe kosa la jinai bila viongezi vingine.
wamuwekee money laundering akashikwe kalio gerezani kule. lazima watu wakaoge naye.Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.
View attachment 2010908
====
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.
Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.
Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.
Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.
Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
na alikuwa anaamini angepata uteuzi wa uwaziri. kuna jamaa yangu mmoja yeye ni dalali alifuatwa na vijana wa makonda dodoma atafutiwe kiwanja, kipindi kile ndio amepigwa chini kura za maoni....wakapanda gari moja. unaambiwa alikuwa anabwabwaja kwenye gari lake hilo kuwa watu wanamdharau kwanini amekosa ubunge, wasubiri apate uteuzi toka kwa mwendazake ndipo watamkoma. na inaonekana mwendazake angekuwepo angempa uteuzi kweli. Mungu naye anajua ratiba zake, wanaomtegemea mwanadamu na moyoni wamemwacha Mungu Neno la Mungu linasema wamelaaniwa. na wale wenye kiburi siku moja Mungu huwa anawashusha hadi kuzimu.Ndio huyu mpaka leo hajalamba uteuzi.
Hehe, sawa bwana DPPHawezi kushtakiwa kwasababu hakuna jinai ambayo aliitenda zaidi ya utumishi uliotukuka!
Naona kila dalili huyo mwanasheria ni mpama tu, kuna mwavuli juu yake iwapo mvua itakuwa kubwa kumzidiTaarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.
Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.
Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.
Heee kumbe ndivyo unavyoonekana mkuu Mmawia ?Nakuona ukiwa kwenye majukumu yako ya kila siku ili mradi mkono uende kinywani. View attachment 2011290
Specificity ndiyo inayotakiwa, siyo tu kusema alitumia madaraka vibaya kwa kusumbua watu. Kama kweli alitumia madaraka kupora mali za watu kwa faida yake binafsi kinyume cha sheria, basi sheria itachukua mkondo wake. Lakini siyo ule usumbufu aliokuwa akiwafanyia watu kwa kuwaweka ndani eti kwa vile wamechelewa mkutanoni, kwa mfano.Kivipi? Alivyopora nyumba ,magari ya wafanyabiashara nayo sio matumizi mabaya ya madaraka? je hivyo vitu haviwezi kuthibitishwa? Mbona hadi magari anayotembelea ziliwekwa documents za walioporwa? Na kuingilia contects za utangazaji nayo ngumu kuthibitisha? Vipi akitokea chizi mwingine akaingia na mitutu TBC taifa akalazimishwa atangazwe rais ina tofauti na alichofanya makonda kulazimisha maudhui yake yarushwe hewani?
Huyo inaelekea alikuwa informer tu wa tiss, siyo carreer intelligence officer.Ndugu kuna Watu nawajua walikuwa ni Waandamizi Kiushirikina na ni Tishio pia nchini na Serikalini ila kuna Watatu walitangulizwa Kimafia Udongoni na Leo wamekuwa ni Historia.
Aliyawadanganyeni kuwa Makonda ni Mshirikina, Tishio na Anaogopwa si tu Kawadharau bali kawaona pia ni Mazuzu kwani kama kweli yuko hivyo sasa ni kwanini anaishi kama Digidigi kwa kuhamahama Mikoa na sasa akipenda sana Kujificha?
Tena hakuna Mtu ambaye ni mwepesi Kuondolewa Kimedani ili akayaanze Maisha yake mapya Udongoni kama huyu Mpuuzi wenu sema tu kwa sasa Kumuondoa itakuwa ni Timing mbaya labda aondolewe kwa Mbinu za Warusi zinazohitaji Akili Kubwa na Mkakati ulio makini.
Nawalaumu tu SSIT kwa Kumlea huyu.
Punguza ujinga unajichora kwa chaki,anaemshtaki Makonda ni mtu binafsi serikali haiusiki.Mungu Mkubwaaaa, at last haki itatendeka, asante sana Mh. Rais wetu, Mama Samia, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu sana.
Hakika watanzania watapata matumaini makubwa sana sanaaa.. Rais Mama Samia ni kiongozi madhubuti, mpenda haki, asiyependa watanzania kuonewa, kunyanyaswa, kuteswa, kuuawa, etc hakika nimeamini Mama Samia ni Rais wa kipekee, Mama mwenye huruma. Kazi iendelee
Excellent, safiiiii...!!! ππππ°π°ππππππππ
Sawa tunza hii comment yakoBashite yupo busy kila jumapili kwenye shamba lake kigamboni akiejoy upepo, mtatapatapa sana na udaku wenu.
ananishi wapi mzee?Hivi pale anapoishi makonda mfanyakazi wa serikali atachukua miaka mingapi kukusanya pesa ya kupanunua na kufanya ukarabati mkubwa kama ule?
[emoji1787][emoji1787]Naibu raisi mstaafu
[emoji1787][emoji1787]Wasisahau na makosa ya kughushi vyeti.