Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Mungu Mkubwaaaa, at last haki itatendeka, asante sana Mh. Rais wetu, Mama Samia, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu sana.

Hakika watanzania watapata matumaini makubwa sana sanaaa.. Rais Mama Samia ni kiongozi madhubuti, mpenda haki, asiyependa watanzania kuonewa, kunyanyaswa, kuteswa, kuuawa, etc hakika nimeamini Mama Samia ni Rais wa kipekee, Mama mwenye huruma. Kazi iendelee

Excellent, safiiiii...!!! 💚💚💚🔰🔰💛💛👏👏👏👏👏👏
 
Mbowe hausiki na hajawahi hata kugusa hayo madawa na kwa hili makonda atalipa. Mbowe alichafuliwa kwa makusudi kabisa.
Ila kwa majay na manji, NI KWELI Wala hawajasingiziwa.
Wewe nani alikwambia manji anatumia hayo madawa?,ulimuona au uliambiwa?
 
Kosa linaloitwa matumizi mabaya ya madaraka ni gumu kulitolea ushahidi mbele mahakama ya haki bila kuonyesha kuwa alitumia madaraka hayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Akitumia madaraka hayo kukutisha linaweza liswe kosa la jinai bila viongezi vingine.

Kivipi? Alivyopora nyumba ,magari ya wafanyabiashara nayo sio matumizi mabaya ya madaraka? je hivyo vitu haviwezi kuthibitishwa? Mbona hadi magari anayotembelea ziliwekwa documents za walioporwa? Na kuingilia contects za utangazaji nayo ngumu kuthibitisha? Vipi akitokea chizi mwingine akaingia na mitutu TBC taifa akalazimishwa atangazwe rais ina tofauti na alichofanya makonda kulazimisha maudhui yake yarushwe hewani?
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

View attachment 2010908
====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
wamuwekee money laundering akashikwe kalio gerezani kule. lazima watu wakaoge naye.
 
Ndio huyu mpaka leo hajalamba uteuzi.
na alikuwa anaamini angepata uteuzi wa uwaziri. kuna jamaa yangu mmoja yeye ni dalali alifuatwa na vijana wa makonda dodoma atafutiwe kiwanja, kipindi kile ndio amepigwa chini kura za maoni....wakapanda gari moja. unaambiwa alikuwa anabwabwaja kwenye gari lake hilo kuwa watu wanamdharau kwanini amekosa ubunge, wasubiri apate uteuzi toka kwa mwendazake ndipo watamkoma. na inaonekana mwendazake angekuwepo angempa uteuzi kweli. Mungu naye anajua ratiba zake, wanaomtegemea mwanadamu na moyoni wamemwacha Mungu Neno la Mungu linasema wamelaaniwa. na wale wenye kiburi siku moja Mungu huwa anawashusha hadi kuzimu.

hakuna mtu alikuwa na kibri kama huyu mwamba, ndiye mtu aliyekuwa anakula raha kuliko watu wote na alitangaza hadharani, alidharau masikini wasije mjini bila kuoga amesahau kuwa yeye pia aliwahi kupitia maisha ya ukondakta wa daladala na alikuwa hana hata sabuni ya kuogea, alisema mkoa wa dsm ni milk yake, alikuwa anauita "mkoa wangu". na alisema anayo mamlaka kuamua uingie dsm au la, mkoa ambao ameukuta hata kabla hajazaliwa au kuja mjini toka huko koromije ulikuwepo.

huyu hata asiposhitakiwa sasahivi, kuna siku atakuja kuingia kizimbani tu kwasababu jinai huwa haifi.

kwanza waanze na mali zake, majumba yake mwanza, sasahivi wanasema anakaa arusha kwenye nyumba yake pia, Dar es Salaam ana biashara alitumia mitaji ya kupora pesa kafungu amafamasi, alinyang'anya watu magari na pesa hadi zingine zilimzidia akawa akagawa kwa kina kaseja, kipa wa simba etc hadi wakamzushia kuwa anampenda. wanyang'anye mali zake zote za uovu sawasawa na wanavyonayang'anya mali za wahalifu wengine.

watu wajitokeze popote pale walioonewa wapeleke ushahidi.
 
Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.
Naona kila dalili huyo mwanasheria ni mpama tu, kuna mwavuli juu yake iwapo mvua itakuwa kubwa kumzidi
 
Kivipi? Alivyopora nyumba ,magari ya wafanyabiashara nayo sio matumizi mabaya ya madaraka? je hivyo vitu haviwezi kuthibitishwa? Mbona hadi magari anayotembelea ziliwekwa documents za walioporwa? Na kuingilia contects za utangazaji nayo ngumu kuthibitisha? Vipi akitokea chizi mwingine akaingia na mitutu TBC taifa akalazimishwa atangazwe rais ina tofauti na alichofanya makonda kulazimisha maudhui yake yarushwe hewani?
Specificity ndiyo inayotakiwa, siyo tu kusema alitumia madaraka vibaya kwa kusumbua watu. Kama kweli alitumia madaraka kupora mali za watu kwa faida yake binafsi kinyume cha sheria, basi sheria itachukua mkondo wake. Lakini siyo ule usumbufu aliokuwa akiwafanyia watu kwa kuwaweka ndani eti kwa vile wamechelewa mkutanoni, kwa mfano.
 
Ndugu kuna Watu nawajua walikuwa ni Waandamizi Kiushirikina na ni Tishio pia nchini na Serikalini ila kuna Watatu walitangulizwa Kimafia Udongoni na Leo wamekuwa ni Historia.

Aliyawadanganyeni kuwa Makonda ni Mshirikina, Tishio na Anaogopwa si tu Kawadharau bali kawaona pia ni Mazuzu kwani kama kweli yuko hivyo sasa ni kwanini anaishi kama Digidigi kwa kuhamahama Mikoa na sasa akipenda sana Kujificha?

Tena hakuna Mtu ambaye ni mwepesi Kuondolewa Kimedani ili akayaanze Maisha yake mapya Udongoni kama huyu Mpuuzi wenu sema tu kwa sasa Kumuondoa itakuwa ni Timing mbaya labda aondolewe kwa Mbinu za Warusi zinazohitaji Akili Kubwa na Mkakati ulio makini.

Nawalaumu tu SSIT kwa Kumlea huyu.
Huyo inaelekea alikuwa informer tu wa tiss, siyo carreer intelligence officer.
Na inaelekea hakuwa na mafunzo yoyote, katika utaalam wowote.

Kuingia Clouds, kama mshamba, tukio la Lissu Dodoma- ambayo ilikuwa operation ya kitoto, utekaji nyara kina Roma na Mo, zoote hazina utaalam.

Hawa ndio wameingizwa na kuitwa tiss , wakati si tiss waliofundishika bali wapambe wa wakubwa.

Tiss tunayoijua ni watu discreet, intelligent na proffessional.
 
Mungu Mkubwaaaa, at last haki itatendeka, asante sana Mh. Rais wetu, Mama Samia, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu sana.

Hakika watanzania watapata matumaini makubwa sana sanaaa.. Rais Mama Samia ni kiongozi madhubuti, mpenda haki, asiyependa watanzania kuonewa, kunyanyaswa, kuteswa, kuuawa, etc hakika nimeamini Mama Samia ni Rais wa kipekee, Mama mwenye huruma. Kazi iendelee

Excellent, safiiiii...!!! 💚💚💚🔰🔰💛💛👏👏👏👏👏👏
Punguza ujinga unajichora kwa chaki,anaemshtaki Makonda ni mtu binafsi serikali haiusiki.

Sasa Samia anakujaje? Sifa za kijinga.
 
Back
Top Bottom