Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Huyu akipelekwa ubaoni hachomoki especially hilo kosa la matumizi mabaya ya madaraka watamdaka mapema mno maana alikuwa anasumbua watu then mwishoni hakuna kinachotokea zaidi ya kuwapakazia watu Mambo ambayo amekosa ushahidi.
Makonda ana ukaribu wa kipekee na huyo Mzanzibari, hawezi kushtakiwa
 
Kwani Mbowe hayo makosa amefanya mkuu,?? Ila huyu si amefanya na wote tumeona???
Huyu ashitakiwe tu mahakama iamue,
Na Mbowe pia haki atapata na atatoka am praying for.
 
Hatimae. Kwanza lile la kuvamia clouds media hachomoki. Ninawaonea huruma wale aliongozana nao. Gwajima alisema kweli. Hatimae amemfuta kwenye ulimwengu wa siasa.
Na Gwajima naye ni msanii tu
 
Hii kolabo ndo itakuwa kali sana...anaenda kukutana na Mbowe huko. Sijui atamsalimia au kauzukauzu tu......
 
Huyu akipelekwa ubaoni hachomoki especially hilo kosa la matumizi mabaya ya madaraka watamdaka mapema mno maana alikuwa anasumbua watu then mwishoni hakuna kinachotokea zaidi ya kuwapakazia watu Mambo ambayo amekosa ushahidi.
Sasa huo ndio ushahidi ,ndio maana kesi ya ugaidi haitamuacha mbowe salama

USSR
 
Huenda watamfunga Mbowe kwa hila na najua Mbowe pia anajua hilo lakini ipo siku haki itatamalaki hutwezi kujuatify kifungo cha kuonewa na uwalifu wa Makonda
 
Natamani hizi moves ziende kwa viongozi wote wanaotumia madaraka vibaya.

Taarifa za mkaguzi Mkuu wa Serikali huwa zinaonyesha jinsi ofisi za umma zinavyofuja fedha sana. Ila hakuna Kiongozi ameshawahi kushtakiwa.
 
Duuu wanamisha magoli......tuhame nae tuache ya msingi.....basi sawa mleteni huyo....tuhangaike nae
Ccm ndio chama pekeee kina viongozi wajinga na walio na hekima inch inazama wao wanafukua makaburi haha ngoja tuone
 
Ingependeza zaidi tungepata habari kamili kabla ya kuchangia.

Haya magazeti ya Bongo mara nyingi kichwa cha habari na habari yenyewe ni vitu viwili tofauti.
Wewe endelea kusubiria hadi ziandikwe na uhuru
 
Kwa vyovyoye iwavyo, hakuna namna Paul Makonda akaishi bila kushtakiwa, iwe kwenye utawala huu au mwingine.

Huyu ana uovu wa kupindukia, kuwanyima watu haki ya kuishi, haiwezekani ipite tu hivihivi. Atambue kama siyo leo au kesho, lakini ipo siku ambapo makazi yake lazima yawe jela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…