Rais ajaye Tanzania atokane na mmojawapo wa viongozi wafuatao

Duh Kinana tena..huyo na msoga pua na mdomo..haramu ya kinana halali ya msoga, haramu ya msoga halali ya Kinana.
 

Hussein Mwinyi hapana, hafai.
Anauza visiwa vya Zanzibar kwa Waarabu kama ambavyo Samia anauza bandari za Tanganyika kwa Waarabu wa Dubai.
Huo ni uhaini dhidi ya Jamhuri.
Uhaini unamwondolea kiongozi yeyote sifa ya kuendelea kuwa kiongozi.
KInana hapana, maana ile kashfa ya meli bado inamwandama.
Majaliwa hapana maana naye anaunga mkono hadharani kuuzwa kwa bandari zetu.
Kabudi na Kinana tuendelee kuwafikiria.
 
Huyo palamagamba toa kabisa
 
Makamu wa Rais
Dr. Philip Mpango anastahili kugombea Uraisi.
Kwakweli ana sifa zote.

Ni mnyenyekevu na Mchamungu.

Tunahitaji Kiongozi Mchamungu.
Kwa Karne hizi za Ukoloni Mambo Leo.
 
Hii ndio orodha ya wanasiasa na viongozi ambao ninaamini kama akampokea mikoba Rais Samia basi nchi itasonga mbele Kwa Kasi sana:
4. Dkt. Hussein Mwinyi
Naunga mkono No. 4, nami niliwahi kumpendekeza Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke nilisema
P
 
Kwa nini hukuniweka mimi wa kwanza?
 
1. Mzee.Abdulrahman Kinana

Meli ya huyu dingi ilikutwa na pembe za ndovu huko Vietnam akadai eti ni kweli yeye meli ni yake ila hajui mteja alikuwa kapakia nini. Hauwezi kupakia mzigo kwenye meli bila kujua kilichopakiwa. Uadilifu wake ni mashaka matupu. Hafai kuwa Rais wa Tanzania.

2. Prof. Palamagamba Kabudi

Huyu dingi hana kashfa za ufisadi ila alishiriki kudanganya watanzania kwamba tunaidai Barric trilioni 495. Kwa uongo alioshiriki hafai kuwa Rais.

3. Dkt Bashiru Ali Kakurwa

Katibu mkuu kiongozi wa zamani hafai kabisa kuongoza nchi ya kidemokrasia. Alishiriki kikamilifu kubomoa umoja wa watanzania uliojengwa kwa miaka mingi. Shukrani kwa Mama Samia kuleta maridhiano tena.

4. Dkt. Hussein Mwinyi

Dr Mwinyi anafaa kwa zaidi ya 100% kuwa Rais wa Tanzania. Sifa zake zinaeleweka hakuna haja ya ufafanuzi.

5. PM Kassim Majaliwa

PM pia anafaa sana. PM anaweza kulaumiwa ila kwa cheo chake sio mwamuzi wa mwisho kwahiyo mambo mengine sio kwa utashi wake. Imagine huyu ndo PM pekee aliyewahi kuambiwa na boss wake kuwa mashangazi zake watapigwa. PM anafaa kuwa Rais wa Tanzania.
 
Umewasahau hawa
1.Bashite
2.Sabaya
3..Polepole
4.Mama Janet Magu
 
Hii ndio orodha ya wanasiasa na viongozi ambao ninaamini kama akampokea mikoba Rais Samia basi nchi itasonga mbele Kwa Kasi sana...
Ni hivi , Rais wa halali hutokana na Uchaguzi ulio huru na haki , ambao unamtoa kiongozi wa Watu aliyechaguliwa kihalali , kiongozi hatajwi na mtu binafsi kama wewe .

Zipo taarifa humu kwamba Hussein Mwinyi alikataa kujiunga na mafunzo ya JKT wakati ule alipotoka Shule , Hata leseni ya Udaktari wake inadaiwa alijipa kimabavu baada ya kuwa Naibu Waziri wa Afya , inadaiwa aligoma kufanya Mafunzo kwa vitendo ( Internship ), huyu ana uzalendo gani wa kumpa urais ? ni vema mkawajua kiundani hawa mnaowapigia debe .

Kasimu Majaliwa alishiriki kuteka kila mtu wa upinzani aliyegombea ubunge kwao 2020 ili apite bila kupingwa , yaani unakuwa PM halafu unaogopa uchaguzi , mtu kama huyu awezaje kuwa Rais ? acheni kudharau watanzania .

Mpaka leo muulize Kabudi ile dawa ya corona aliyoenda kuisomba Madagascar ilitibu watu wangapi ? au muulize ule uongo kuhusu fidia tutakayolipwa kwenye madini ulimsaidia nini Mtanzania ?
 
Hii ndio orodha ya wanasiasa na viongozi ambao ninaamini kama akampokea mikoba Rais Samia basi nchi itasonga mbele Kwa Kasi sana...
Hata mmoja kati ya hao hafai. kwasa sasahivi ni zamu ya mgalatia na mtu toka bara. period.
 
Makamu wa Rais
Dr. Philip Mpango anastahili kugombea Uraisi.
Kwakweli ana sifa zote.

Ni mnyenyekevu na Mchamungu.

Tunahitaji Kiongozi Mchamungu.
Kwa Karne hizi za Ukoloni Mambo Leo.
Sifa ya urais sio unyenyekevu wala huo uchaMungu, kiongoz ukiendekeza hii tabia ya huruma Taifa kamwe haliwezi kupiga hatua.

Jifunzen kwa nchi zilizoendelea viongozi wao wako vipi?

Stable kimaamuzi na katili kwenye mambo ya kipuuzi.

Hao wacha Mungu ndio hao akina samia na huyo dct mpango wanyenyekevu mpaka wanafuga majizi nawao wenyewe wanaficha uwizi wao kupitia huo unyenyekevu uchwara...

Ni bora kuongozwa na dicteta kuliko hao wanafiki
 
Ninavyozidi kukua kiumri na kiakili nimejifunza kuwa RAMLI hizi chonganishi wala hazina ukweli....

Hayati JPM hakuwa mtajika mbele ya wale "wana mitandao"....

Mh.Rais SSH hatukumtegemea kuwa aliko....

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye kesho yetu na ikifika inakuja na maajabu mengi mno...

Kubwa tu uendelevu wa utulivu wa taifa letu teule duniani ,amen[emoji120]

Hakika nabii Adam A.S aliishi Ngorongoro [emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…