Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 37 (5) ; inasomwa pamoja na ibara ya 40.

Ambapo, Rais mteule (makamu wa Rais) , kama atashika nafasi ya Urais kwa muda wa chini ya miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea kwa awamu mbili zingine.

Ambapo, Rais mteule (makamu wa Rais) , kama atashika nafasi ya Urais kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea tena kwa awamu moja tu.
Sawa mkuu, ngoja nigoogle katiba nipate mawili matatu
 
Kiutaratibu mkuu wa majeshi hushikilia kitu kwa muda hadi tume ya uchaguzi itakapoamua au mpaka miaka ambayo ilikuwa ndo mwisho wake kura zipigwe tena..
Hii ni katiba ya nchi ipi Mkuu wa Majeshi anachukua nchi? Likitokea la kutokea?
 
Jitafakari. Usitafute kiki za kina Sosopi mitandaoni. Mwisho wa siku utasumbua watu kutafuta wadhamini wa kukuwekea dhamana Mahakamani.
Msitishe watu, hakuna ambaye hafi, hivyo si kosa kuwaza akifa Leo itakuwaje. After roll tangu tupate Uhuru hajawahi kufa raisi akiwa madarakani, hivyo si vibaya kuwaza ili tujue likitokea inakuwaje. Hata mkimuogopa vipi (maana si kweli kuwa mnampenda) Siku moja atakufa tu.
 
Katiba inasemaje kuhusu hili,wajuzi naomba kujua iwapo Rais atafariki kabla ya kumaliza muda,nini kinafuata!!!

Kangi lugola÷"kifo ni mtego na humkuta mtu mahali popote na wakati wowote"

Una mpango wa kumuondoa jiwe?
 
37(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.
 
Mtu aliyeshika namba mbili katika kura za Uraisi
 
Lakini labda mama akikaa mambo yanaweza yakaw na afadhali
 
Nadhani mkuu unawaandaa watu kuikubali hali iwapo punde atakufa.. nawewe ushaukwaa ushehe nini... katiba iko wazi juu ya hilo na hata na hata atakaemwachia nae akifa..chukua muda kidogo uipitie utajifunza mengi.
Mkasome habari za wasudukayo....walimwuliza ikiwa mtu akaoa mke akafa bila kumpatia mtoto, na kaka yake akamwoa mjane naye hakumwachia mtoto...ikaendelea hivyo hivyo kwa waliofatia...je siku ya ufufuo atahesabika mke wa nani?
 
Back
Top Bottom