GE2025 Rais Chama Cha Wanasheria wa Serikali: Hakuna Anayeijua Sheria Kuliko Wakili wa Serikali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Yaani wamekimbilia vyombo vya habari kupata 'sympathy' baada ya Katuga na Mrema kudhalilishwa.

Umma unapaswa kuwashukuru sana Mawakili wa serikali kwa kuleta kinachoitwa ''blessing in disguise'' au kwa kiswahili '' balaa lenye neema mwishoni''.

Kumpeleka Lissu Mahakamani kumeondoa mashaka ya wale wachache waliosita sita kuhusu uwezo wake.
Tunaomjua Lissu hatuoni cha ajabu, wale waliokuwa na shaka sasa imewatoka.

Kinachojadiliwa sasa si kesi inayomhusu TAL ni jinsi anavyowabagaza waliotunga kesi !
Badala ya kumuondolea umaarufu kesi imempa nafasi si ya umaarufu bali '' Rais Mtarajiwa''

Mahakama iwasaidie mawakili wa serikali kwa kufuta kesi, ikiachwa iendelee ni tatizo kubwa kwa serikali lakini fursa adhimu kwa TAL. Huyu ni ''mtarajiwa'' huku 'site'' watu wanasema
 
Huyo OBSOLETE Lawyer anatudistract na hoja yetu ya No Reforms No Election..
Lissu siyo mhaini
 
Kuna walimu hutunga mitihani na ukiwapa hiyo mitihani bila marking scheme ndo imetoka hivyo
 
Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), Bavoo Junus, amewashauri wananchi kuepuka kujadili masuala ya kisheria bila kuwa na uelewa wa kutosha, akisema hatua hiyo imekuwa ikisababisha upotoshaji mkubwa unaoweza kudhoofisha imani ya jamii kwa taasisi za sheria.

Akizungumza leo Ijumaa, Septemba 12, 2025, jijini Dodoma, Junus amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitoa tafsiri potofu za sheria katika majukwaa mbalimbali bila kuwa na utaalamu wowote wa taaluma hiyo, jambo ambalo linaweza kuwachanganya wananchi na hata kuchochea vurugu.

“Hakuna mtu nje ya Serikali anayeijua sheria kuliko sisi. Sisi ndio hupitia, kuchambua na kuhakikisha kila sheria inazingatia masilahi ya Taifa kabla haijafika popote. Niwaombe wasio na uelewa juu ya sheria waache kupotosha umma,” amesema Junus.

Your browser is not able to display this video.
 
Competitiveness ya mtu inaonekana field si kwenye maneno ya vyombo vya habari

Ww ni mwanasheria , dokta au engineer tutakuona field umahiri wako
Else ww ni kanjanja mwenye cheti

Huyo jamaa anafanya damage control, too bad watu wameshajua wanasheria vihiyo na makanjanja ni wapi
 
Walioshauri fomu za Mpina zisipokelewe hawako serikalini?
 
Aase tundu ni kiboko.kawagaraza kweli kweli.ni mechi kali kati ya lisu (barcelona) vs serikali ( costi union).aibu wanayo wanategemea maagizo toka juu.kaz kila siku kukesha kwnye bar pombe na mademu.mwenzio lisu anakesha kusoma.
 
Hajielewi huyu, kutunga ndo kujua?Anaweka majigambo mbele, mnaweza mkajikusanya ka-kikundi kenu mkaona ndo majembe - mkileta nje wengine wanaona ni utopolo tu..thats life kwa binadamu wote sababu WE ARE ALL IMPERFECT...thats nature..
 
Kila kesi wameshindwa, yaani hawajawahi kushinda kesi hata moja.
 
Kwanini aongee sasa, kumetokea nini?

Mtu bila kuulizwa akija akaanza kukwambia "mimi siyo mwizi" unajiuliza maswali kulikoni?
 
His first name must be Middle finger and dumbass his surname
 
Wakili mkuu wa serikali alikuwa hajui kama Raisi anaweza kuitwa mahakamani kama shaidi....
 
Makosa tumeumbiwa binadamu - Wakili wa setikali.

Sasa kwanini mnawahukumu kama makosa tumeumbiwa?
 
KESI ZA MIGOGORO KWENYE MAHAKAMA ZA KIMATAIFA MMESHINDA NGAPI,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…