Rais Joe Biden awaalika Viongozi wa Africa kwa majadiliano Washington

Hakika
Ila kikubwa US EU na shost zao wanataka kurejesha ushawishi ambao umepotea ama unapotea huko AFRIKA kufuatia ujio wa UCHINA INDIA TURKEY nakwambaali RUSSIA
Je atafanikiwa huu mkutano utaleta mwanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta pia na ya NATO na wenzie
 
Tatizo la Africa ni sera za ujamaa zilizoharibu uchumi.Nchi ambazo hazikujiingiza kwenye ujamaa kama Botswana, Zimbabwe na Kenya ziliendelea kufanya vizuri kiuchumi.
 
Tatizo la Africa ni sera za ujamaa zilizoharibu uchumi.Nchi ambazo hazikujiingiza kwenye ujamaa kama Botswana, Zimbabwe na Kenya ziliendelea kufanya vizuri kiuchumi.
Hapa ndipo umuhimu wa elimu kuambatana na maarifa unapoonekana. Elimu itakufundisha kwamba ujamaa ulikuwa mbaya. Maarifa yatakuonyesha kwamba kinacholeta maendeleo ya nchi na watu si falsafa za ujamaa vs ubepari bali ni maono na mipango safi, watu sahihi na matumizi bora ya maliasili za nchi watu husika walizojaaliwa na mwenyezi.

Hivi unajua kuwa Israeli ni nchi ya kijamaa? google "kibutz". Hivi unajua kuwa maendeleo ya wajapan at the core ni spirit ya ujamaa? Msiwe mnasoma propaganda za magharibi -- tumieni
pia critical thinking. Hivi unajua kuwa hata hao tunaowaita mabepari na mabeberu wa magharibi lakini kwenye mipango yao inayofanyika sirini wanautumia ubepari kama strategy lakini spirit ni ya ujamaa? Hivi unajua mitaji iliyoanzisha corporations kubwa kama Microsoft, Facebook, Apple, ni pesa na dhamana kutoka kwa serikali ya Marekani (na serikali ina jicho lake kwenye hizo corporations kuhakikisha maslahi ya Marekani yanalindwa?) Ni nyie tu mnaoaminishwa kwamba ujamaa ni mbaya -- lakini tafsiri pana ya ujamaa maana yake ni Uzalendo, kufanya mambo kwa faida ya nchi na watu wa asili yako.
 
Ninachakiona ni kwamba huelewei hata Ujamaa na Ubepari ni kitu gani.

Unazungumzia sijui falsafa, spirit n.k kama vile unatoa mawaidha.
 
ttzo ni viongoz wetu wala sio hao tunaowalaumu kila siku yaan wapambane kuiangusha Afrika waiache China na India zinapiga hatua , afrika ndo makao makuu ya comedy dunian
Eti Afrika ni makao makuu ya comedy duniani😄😄🙌🙌 .daah mkuu umenivunja mbavu , Afrika sijui tumelaaniwa
 
Acha vichekesho, hao magharibi wanatuuzia nini? Magari tunaagiza yaliyotumika Japan, bidhaa nyingi tunatoa China, dawa zinatoka India, sasa sisi ni soko gani la magharibi?
Bana nawe jiongeze kupata tafsiri pana ya soko. Jichunguze hapo ulipo na angalia kuanzia asubuhi hadi jioni maisha yako, unavyokula na unavyovaa. Unajua kuwa ugali unaokula hayo mahindi mbegu zake ni new imported seeds? Wamagharibi kupitia systems zao za FAO na food security tumelazimika kuona mbegu zetu za asili hazifai. Matokeo yake lazima ununue mbegu kila msimu wa kulima, na hadi unavuna lazima uwe umeshanunua bidhaa imported kutoka kwao za kutosha.

Another thing: westerners wameadvance sana kwenye ukoloni wao mamboleo. Hata kama kitu umenunua kutoka China au Singapore lakini mwenye kiwanda na mtaji unaweza kukuta ultimately ni mmagharibi, na hapo sijaingiza "soft-products" kibao unazowalipa bila kujijua. Nyie kwenu mnahesabu kwamba ni maendeleo but mimi shida yangu ni namna ambavyo uwezo wetu wa kuingia katika hii system ya uchumi kama washiriki wazalishaji usivyokuwepo kabisa. We are reduced ti being mere consumers of imported technology, goods, service, etc. Na pale "tunapowauzia" tunawauzia mali ghafi mfano madini wanachimba na kuchenjulia nje huku watoto wetu wanaosoma mining processing kubakia kusoma theory and no real application. Yaani ni sheedah tupu. Fungukeni wajamenim
 
Tatizo la Africa ni sera za ujamaa zilizoharibu uchumi.Nchi ambazo hazikujiingiza kwenye ujamaa kama Botswana, Zimbabwe na Kenya ziliendelea kufanya vizuri kiuchumi.
Kenya, Zimbabwe njaa , rushwa , uchumi mbovu , madeni ya kutosha kutoka china [ wajamaa ] nao hawa ni wakutolea mfano. Afrika imeoza kote tena hasa hasa Kusini mwa jangwa la sahara.
 
Hamna kitu hapo ni utapeli mtupu.
 
US /Africa,Russia/Africa,,France/Africa,China/Africa,Japan/Africa. Kila nchi tajiri inatuvuta. Jamani watuwache sasa. Halafu hii dharau. Yeye si ndo angekuja Africa ?Au anaogopa mbu ?
 
Tatizo la Africa ni sera za ujamaa zilizoharibu uchumi.Nchi ambazo hazikujiingiza kwenye ujamaa kama Botswana, Zimbabwe na Kenya ziliendelea kufanya vizuri kiuchumi.
Mbona hizo sera za ujamaa hazijaharibu uchumi wa China. tatizo sisi waafrika [ watu weusi ] tuna matatizo Sana kwenye bongo zetu.
 


Hizo mbegu za mahindi ndiyo zinatoka Marekani? Hebu lete ushahidi kama ni kweli.

Bidhaa za westerners zinazozalishwa China kwa mfano Nike sisi hatuzimudu. Tunanunua feki ambazo Wachina wenyewe wametengeneza. Sasa Mmarekani anapata faida gani sisi tukinunua Nike feki au Iphone feki?
 
Zimbabwe ilikuwa ni nchi yenye uchumi mzuri, inayozalisha na kuuza chakula na bidhaa za viwandani kwa wingi nje mpaka pale Mugabe alipoanzisha vurugu zake za mashamba na ubabe wa kisiasa.

Kenya ni nchi yenye uchumi mkubwa na mzuri kuliko nchi zote za Africa Mashariki pamoja na migogoro ya kisiasa waliyoipitia kwa muda mrefu sana.

Nchi karibia zote duniani zinakopa na zina Rushwa, hata huko China Rushwa ipo sana tu.
Kenya, Zimbabwe njaa , rushwa , uchumi mbovu , madeni ya kutosha kutoka china [ wajamaa ] nao hawa ni wakutolea mfano. Afrika imeoza kote tena hasa hasa Kusini mwa jangwa la sahara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…