Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Mkuu umeuliza swali zuri, but omba mungu huku pia ikitumika mahalifa aliyokupa kujua hema na baya, mfano umepimwa umekutwa, typhoid, dawa zipo , na hutaki kunywa, alafu sema mungu tuone Kama hautazikwa,
Hoja hapa serikali pitia wizara ya afya , KWA kushirikiana na Tamisemi, lazima kuja na sheria ya mpito KWA ajili ya kujikinga na CORONA, maji tiririka kila mahali kila kaya , barakoa iwe lazima huna na unatembea mjini piga fain, mikusanyiko isiyo ya lazima piga chini,
Tutaweza vuka, ila kusema kwamba corona ya kwanza wenzetu walikufa Sana , ni sawa ila sio kigezo tusichukue hatua ,mpaka nasi yatukute, mdudu , huyu ana mutate kila wakati, hakuna sababu ya kusubili,
I wish , ningekua katibu mkuu, waziri or naibu , Ningeamuka hasubuhi natangaza mikakati tajwa hapo juu, wakati huo nikiwa na barua ya kujiuzuru , au kutumbuliwa mda huohuo!
 

Huu ujinga umeongea hapa ndio Kinjeketile aliwaaminisha waafrika kuwa mizinga ya wazungu itageuka maji, baada ya ujinga huo kuwaingia watu waliipata fresh. Mwaka jana Corona haiukuondoka kwa maombi, bali haikuenea vizuri na serikali iligoma kutoa taarifa za ugonjwa.
 
Kama ana itikadi Kali hivyo kama wasabato walokwenda airport Mungu awapeleke (sijui ulaya?) Haspitali zinajengwa za nini?
 
Chanjo, barakoa, kukaa mbalimbali
 
Naaminii kuna mahali Watanzania hatujaelewana hasa katika awamu hii ambayo watu wamejaa hofu ya kugopa watawala!!
Tumeshaona madhara ya lockdown na kwa umaskini wetu na kutokuwa na takwimu sawasawa kuweka lockdown ni kuua watu.
Rais amekazania lockdown lakini hatuhitaji lockdown ila tunahitaji kauli yake "from horse's mouth" juu ya uwepo wa covid 19 na uwepo wa kirusi kipya na kibaya zaidi.
Kauli hiyo ya Raisi itabadilisha nguvu na mwelekeo wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu.Kutokupata maelezo toka kwa Mkuu wa nchi kunaleta mkanganyiko na ndipo "wanafiki" wanapopatia pa kujikweza.
Kila binadamu anajua kufa kupo lakini kwa nini ubanwe na pumzi siku tano ndio ufe kwa ugonjwa ambao ungeweza kujikinga nao?
Binafsi naamini Mwenyezi Mungu akimpa ujasiri na akatamka hadharani ataokoa wengi na muda wa ugonjwa kwa nchi yetu utakuwa mfupi,Inshallah!
 
Hapa unapotosha mkuu.si dhani kama kuna kum jaribu Mungu hapa.Tunaambiwa tuendelee kuchukua tahadhari ila tusiache kumuomba Mungu.
Endeleeni tu kutetea upumbavu! Unasema vipi kwamba tuchukue tahadhali wakati mwenyewe huoneshi kwamba unachukua tahadhali?! Yaani kilichooneshwa kwenye ile shughuli ya kuaga kwako wewe ndo kuchukua tahadhali wakati rais na viongozi wakuu wote hata barakoa hawajavaa? Hivi unamwambia mwanao acha ulevu wakati mwenyewe kila siku unarudi ukiwa tilalila?!
 
Kama ndio hivyo muheshimiwa rais tugeuze shule zote na vyuo kuwa nyumba za ibada.

Haina maana tena kwenda shule kupata elimu ya kukabiliana na matatizo kama haya kwani Mungu yupo na ukiomba chochote atakupa bila jitahada zozote.

Hizi tiba zote na dawa zinazo patikana ni kutoka kwa shetani sio? Sio kwamba Mungu katupa elimu ?

Mh Rais hakuna mtu anataka ufanye lockdown, tulicho kuomba ni kubali ugonjwa upo, waambie wananchi wote wajikinge(barakoa lazima) tuepuke na mikusanyiko mikubwa, serikali iongeze misadaa kwenye hospitali zote hili waweze kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.

Sio kwamba hatumuamini Mungu, hapana, tunachukua tahadhali zote na kumuomba Mungu. Sio unaingia kwenye pango la nyoka alafu unamuomba Mungu akulinde; Mungu kashakupa akili ya kujua hatari na salama. Mungu anataka utumie akili pamoja na dua , sio dua peke yake.

Basi Mh. Rais naomba endelea na dua zako lakini sasa tumia na akili/elimu yako aliekupa Mungu kukabiliana na hili swala.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mods umeunganisha Uzi

Acheni hizo nyie

Mna vijiba vya roho
 
Mad president!Mungu huwa halipi maombi bali huwa analipa jitihada.Kama unamuomba Mungu bila ya kuwa na strategic plan nzuri pamoja na vitendo madhubuti vya kupambana na janga huko ni kumkejeli Mungu!
 
Tatizo hii Ni Africa, ingekuwa kwenye nchi zilizostaarabika ambacho angefanya Jiwe ili kuitunza heshima na ushujaa wake (Kama anavyo anyway) Ni kujiuzulu...Nyerere alipojikuta kwenye Hali Kama hii hakujiuzulu tu Bali aling'atuka kabisa na ndiyo maana Hadi leo Watanzania tulio wengi tunamheshim na kumpenda pamoja na madhaifu yake ya ki ubinadam
 
Mzee nadhani anakosea sana kutia shaka imani za watu. Mungu yupo na tunamshukuru kwa kila kitu. Ila Mungu katupa maarifa binadamu yeye anatoa rizki lakini ni yeye anataka wafanye kazi ndio anatoa. Unapokuwa na mgonjwa unatumia kila ulichonacho kumtibu lakini pia unamuomba Mungu haya mambo yanaenda pamoja, unajisaidia na Mungu anakusaidia. huwezi kupona kwa miujiza tumepewa maarifa na Mungu tutumie. Ningemuelewa kama angesema ugonjwa hatari kuwashukuru wafanyakazi wa afya kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na hatua gani za kuchukuwa kama serikali kusaidia, hakuna mtu amesema anataka lockdwon ila yako mambo yakufanya halafu baada ya jitihada zetu kwa uwezo wetu tumuombe Mungu atusaidie katika juhudi zetu, Mungu wa dunia sio wa Tanzania tu. enzi za mikate kushushwa toka mbinguni hakuna jitahidi, omba na Mungu huwa saidia wenye kujisaidia.
 
Dr Mpango Mungu amsaidie ainuke na wagonjwa wengine wote, mzee leo kasema katumiwa msg na Dr mpango lakini wakati huohuo kasema Dr mpango kapata salamu za mzee kupitia kwa mke wake hapa inakujulisha hali ilikuwa ni mbaya kiasi salamu zinapitia kwa mtu lakini majibu kwa mwenyewe kuna mashaka na hili. Kikubwa tumuombee apone na wengine wote. Huyu waziri kabla ya kupotea aliwaonya wafanyakazi wa wizara yake wajilinde alikuwa kishaona dalili labda. shida yangu kwanini mpaka watu wazushe uwongo ndio manakuja kukana hadharani? mambo kama haya mkiyaweka tu hadharani hata wale waongo watakuwa hawana jipya. kuna mawaziri wengi leo hawakuwepo watu wataanza kuongelea hata Ndungai leo kaingia mitini sijamuona na mzee kabudi kama sikumuona hivi.
 
Hujui chochote wewe
Mjuze na sisi tujue ili matendo ambayo tunaona Mungu hahusiki, tupate kujua kua ALIHUSIKA.

Mfano: Kupigwa risasi TAML, kupotea kwa Saa8 na mengine mengi ambayo mimi nawewe tunayajua.
 
Tuna muomba MUNGU lakini pia lazima tuchukue tahadhari maana hata MUNGU alisema jisaidie nitakusaidia
Hilo sijawahi kusoma popote kwenye maandiko labda uniambie imeandikwa wapi mkuu
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

[emoji40] [emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]
kweni alisha sema kua haipo?

wabongo bwana.
 
BAVICHA HILI KWAO CHUNGU.HAPO WALIPO WANATAMANI MODS WAUFUTE HUU UZIII. KATIKA RAIS AMBAE ATAKUMBUKWA KWA KUWA NA MAONO AMBAYO ILI UYAELEWE UNATAKIWA UWE NA THE WISDOM ABOVE NORMAL ni huyu jpm.I salute you!!!!
Akumbukwe kwa lipi au kwa nchi kuirudiaha kwenye umasikini? Yaani wewe duniani huyo ndoo unamuona raisi bora? Kweli una matatizo ndugu yangu.
 
Daa Bro Asante hhhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…