Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

CCM ni kivuli tu.

There is REAL POWER behind CCM!

Hao wavaa kijani wengi wao wanatumika tu hawajui hata mamlaka halisi yameshikwa wapi!
 
Mleta mada nakupongeza kwa kutuletea pandikonhili. Hii ni mada muhimu sana katika kujadili siasa zinazoendelea sasa hapa nchini. Mwenye kuizingatia mada hii bila shaka atahitimisha kama ifuatavyo.

1. CCM ya Magufuli imejitathimini na kuona haina uwezo wa "kutoboa" kwenye majimbo yaliyochagua wapinzani.

2. Njia pekee kwa CCM kushinda katika majimbo hayo ni "kupora" wabunge kutoka upinzani na kuwasimamisha wagombee kupitia chama hicho dhidi ya makada walioko ndani ya chama.

3. Kumbe ni kweli "makada asilia" wa CCM wana kinyongo kutokana na maamuzi ya uongozi wa juu kuwapendelea "wakuja" dhidi yao.

4. Majibu ya Mwenyekiti wa CCM yanaonesha wazi kuwa wana CCM "wazawa" si "watu wa maana" tena kukiletea ushindi chama hicho katika majimbo/kata husika kwavile walishindwa dhidi ya wapinzani katika chaguzi zilizopita.

5. Mwenyekiti Magufuli wala hajali Ndugu Sojo anapotetea kuwa wana CCM wazawa walipambana kufa kupona na hata kupoyeza mali zao katika kukitetea chama katika chaguzi za 2010 na 2015.

Hata hivyo, kwa maoni yangu Mwenyekiti Magufuli anakosea sana kuwapendelea wageni dhidi ya wenyeji ndani ya chama. Anasahau kuwa wapinzani aliowapora na kuwapa nafasi kwa upendeleo ndani ya chama chake hawakuishinda CCM katika chaguzi zilizopita kutokana na nguvu zao wenyewe. Ushindi wa wapinzani hao ni maamuzi ya wananchi wapiga kura.

Inawezekana kabisa kwamba tatizo halikuwa "ubora binafsi" wa wagombea, bali ni mwamko wa kimageuzi walionao wapigakura; yaani waliikataa CCM na si wagombea wake. Kama hii ni kweli basi tutarajie CCM kushindwa tena kwenye majimbo hayo. Bali safari hii itashindwa "vibaya" ikiwa ni kweli kwamba wazawa wanahasira kutokana na kudharauliwa na uongozi wa juu.

Asante sana.
 
Mleta mada nakupongeza kwa kutuletea pandikonhili. Hii ni mada muhimu sana katika kujadili siasa zinazoendelea sasa hapa nchini. Mwenye kuizingatia mada hii bila shaka atahitimisha kama ifuatavyo.

1. CCM ya Magufuli imejitathimini na kuona haina uwezo wa "kutoboa" kwenye majimbo yaliyochagua wapinzani.

2. Njia pekee kwa CCM kushinda katika majimbo hayo ni "kupora" wabunge kutoka upinzani na kuwasimamisha wagombee kupitia chama hicho dhidi ya makada walioko ndani ya chama...
Umeongea jambo la maana na la msingi sana. Issue sio wagombea wa upinzani, issue ni muamko wa wananchi katika kutaka vyama na sera mbadala zenye kujali kweli maisha yao na uchumi wao.

Ni dhahiri sasa kuwa ndani ya CCM hali si hali na muamko wa wananchi wa Tanzania umekua kwa kiwango kikubwa sana.

Nimesema humu na nasema tena kati ya mwaka ambao ni rahisi kuiondoa CCM madarakani ni mwaka huu 2020. Upinzani wanachohitaji moja ni kuweka mtu sahihi na si mwingine ni TUNDU ANTIPAS LISSU na mbili ni kuhamasisha nguvu ya umma katika kupiga kura, kusimamia kuhesabu kura na kutangazwa matokeo yote vituoni husika. Zisiwepo kura ambazo zitahamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wakifanya haya upinzani mwaka huu Tanzania tunaingia kwenye historia kama Malawi.

Kwenye nguvu ya umma vyombo vya dola lazima vitainawa CCM mwaka huu.
 
Wakome kabisa, walishangilia kuua upinzani ili wamalizane wenyewe kwa wenyewe.

Mimi kazi yangu ni kupiga makofi
 
Yule Kijana alieuliza lile swali kaisha.

Ccm Mkoa wa Songwe wamekana kumtuma kuuliza hilo swali na atawajibika kwa kuwalisha maneno.

U NEC atauskia kwny kipindi cha Majira kuanzia 2022
Duh

Ova
 
Hata Lowasa alipopewa nafasi ya kugombea Urais kuna mabavicha walisusa kabisa, Dr. Slaa mwenyewe akajiuzulu sasa ni Balozi huko. Binadamu wana mioyo ya nyama hivyo inaeleweka katika kundi la watu sio wote wataofurahia maamuzi flani , ingawa nayo inataka moyo kuweka wazi baadhi ya mambo. Na kuelezana fikra ni utamaduni mzuri kuliko kuishi huku mtu akiwa na kinyongo.
 
Yule Kijana alieuliza lile swali kaisha.

Ccm Mkoa wa Songwe wamekana kumtuma kuuliza hilo swali na atawajibika kwa kuwalisha maneno.

U NEC atauskia kwny kipindi cha Majira kuanzia 2022
Wee kwa majibu aliyopewa na mungu wenu jiwe unafikiri kuna mtu atajitokeza kusema amemtuma na ccm mnavyomuabudu jiwe hv
 
Hata Lowasa alipopewa nafasi ya kugombea Urais kuna mabavicha walisusa kabisa, Dr. Slaa mwenyewe akajiuzulu sasa ni Balozi huko. Binadamu wana mioyo ya nyama hivyo inaeleweka katika kundi la watu sio wote wataofurahia maamuzi flani , ingawa nayo inataka moyo kuweka wazi baadhi ya mambo. Na kuelezana fikra ni utamaduni mzuri kuliko kuishi huku mtu akiwa na kinyongo.
Bora hao Bavicha na Dr Slaa waliosusa na kujiuzulu kuliko uvccm na makada wanaokufa na tai shingoni!
 
Back
Top Bottom