Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Halaf tumkumbushe tu kuwa alimfukuza kazi Oluoch wa CWT na sasa amegaragazwa mahakamani na wanatakiwa wamrudishe kazini..


Pia aliwahi kumfukuza kazi Mataragio wa TPDF lkn baadaye alimeza matapishi yake na akalazimika kumrudisha kazini
 
Ndio ugaidi wa waislamu dunia nzima inaoulalamikia. Kujilipua? Why do that? Kwani hakuna taratibu za kumwadhibu kisheria? Ndiyo ugaidi wa kiislamu huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa na akili sawa sawq, hata katik maisha ya kondoo, mbuzi, kichaaa, wanaweza kukufundsha kitu.
Dunia ana masomo na vipindi kila leo, lakini tu yahitaji kuwa timamu kuelewa haya.

Kama na hapa hujaelewa, nadhan utakuwa umejua kwanin, huelewi wala kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais ni mwajiri mkuu, anaweza kukufuta kazi au kupendekeza upandishwe cheo muda wowote ule.

Kiongozi mkuu wa serikali ni rais, huyo pimbi wa huko Kilosa ni muajiriwa wa serikali.

..mamlaka hayo amepewa na KATIBA.

..hivyo kuna sheria na miongozi ya kuyatumia mamlaka hayo.

..hoja yangu ilikuwa ni kumjibu KARLO MWILAPWA ambaye alidai Raisi anaweza kumfukuza kazi mtumishi yeyote bila kufuata sheria.

..kuhusu mpuuzi wa Kilosa nakubali kwamba anastahili kufukuzwa kazi.
 
Hiyo panel ya hao majaji ilikuwa ni balaa. Jamaa walikuwa wana-base maamuzi yao kwenye sheria tu na sio vinginevyo.

Pamoja na kwamba labda wote hawakuwa waislamu lkn kwao kilichokuwa muhimu ni haki kwa maana ya sheria na kulinda taaluma yao.

Kwa bahati mbaya mno tena mno, leo hii hatuna tena majaji kama hao. It's very pitiful and sad if not pathetic.
 
Hakuna tena na hawatakuja kutokea. These judges were appointed on merit and not on know who criteria! Kumbuka Judge kama akina Mwalusanya, Lugakingila, Katiti, Mroso and a few others!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ametenda jinai kubwa ya uchochezi.

Hafai kuwa mtumishi wa umma kwa sababu haheshimu asilimia 50 ya watu wanaomlipa mshahara kwa kodi zao.
 
Wansheria tusaidieni jamani hivi ni sahihi kosa moja mtu kuadhibiwa zaidi ya mara mbili.kusimamishwa kazi,kufunguliwa mashitaka kabla ya rulling kufukuzwa kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We unachanganya mada kwa Nini kuna vikao vya ajira na nidhamu ?kazi yake ni Nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue ya Kilosa ambayo nafikiri ni "Religious Profanity", ni kosa la jinai tu kama makosa mengine yoyote ya jinai.

Sioni mantiki ya rais kulivalia njuga namna hiyo hilo swala kwani hiyo tuhuma sio ya kikazi na maslahi ya serikali hayajaathiriwa kutokana na kosa hilo.

Kwa mara nyingine tena huyu mtuhumiwa anampa tena Mr. Magufuli jukwaa la kutafutia uungwaji mkono kutoka kwa waumini wa kiislamu huku uchaguzi ukikaribia.

Mwisho, huyo jamaa kama mtumishi ana haki zake, sio haki rais amtumie kama "Political Bait" kwa swala ambalo, kimsingi, serikali is, obviously, not an affected party.

This, like several others, is another hypocritical disposition displayed by the incumbent which must be condemned by all reasonable minded persons.
 
Exactly, reasonable minded people, umenifurahisha sana. Kuna mijitu humu ni kama karai za kuchotea cement na zege!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria si tumejiwekea wenyewe? Hata mtu ukimkamata mtu anaua red-handed, kumhukumu kifungo hapo hapo, ni lazima afikishwe mahakamani na asikilizwe kabla ya kuhukumiwa, right? Hata kazini ni hivyo hivyo. Huwezi kutoka huko ulikotoka ukamfuta mtu kazi. Hiyo itakuwa ni maisha ya banana republic. Sheria ni social contract. Tumekubaliana hivyo, kwamba sisi ni nchi inayofuata na kuheshimu misingi ya sheria. Hivyo tuwe wavumilivu na waungwana.
 

1. Tena ikithibitika alikuwa yuko "mbwiii" na kilevi, hata hahitaji kuweka hata wakili, anaachiliwa asubuhi tu na hakuna cha "upelelezi haujakamilika" wala nini....

2. Halafu mimi nashangaa sana watu na serikali yenyewe inavyolikuza jambo hili unnecessarily kabisa. Kwanza hebu tujiulize tangu lini "kitabu chochote cha makaratasi tu yanayoweza kuchanika, kuungua moto ama kuchanwa na mlevi barabarani, iwe Biblia ama Korani kiwe kitakatifu??"

Makaratasi yapo kwa ajili ya kutunza kumbukumbu tu za maandishi lakini hatuwezi kuziita "takatifu". Hayo maandishi yakisomwa na kukaa ndani ya moyo ama nafsi ya mtu yakatenda kazi kusudiwa, ndipo yanakuwa na maana. Ukishamaliza kusoma, waweza hata kutupa chooni kitabu hicho kwa sababu utakuwa umepakua na ku - install ndani ya moyo kila kitu...

Kama Yesu Kristo atarudi leo kuchukua watu wake, hatauliza ama kuwataka watu waoneshe " the so called - Biblia ama Korani takatifu" ndiyo iwe tiketi yako ya kuingia mbinguni. HAKUNA!!

3. Mimi ni Mkristo 100%. Lakini akitokea mtu ambaye anapesa zake zimekosa kazi ya kufanya na akaamua kwenda kununua Biblia zote madukani na kuzipeleka dampo kule Pugu na kuzitupa ama kuzichoma moto, nakuhakikishia kabisa SITAJALI LOLOTE!!...Why?

4. Kwa sababu Mungu yeye ndiye Mtakatifu na kamwe haishi kwenye makaratasi yanayoitwa "Biblia" au "Korani". Mungu anaishi ndani ya Roho ama Mioyo na Nafsi za WATU haishi kwenye makaratasi yanayochanika ama kuchomeka na moto ama kulowa na maji....!!

5. Ukichana makaratasi hayo yanayoitwa leo " matakatifu", haiwezi kuwa umemchoma au kumchanachana Mungu. Mungu Mtakatifu hachanwi wala haunguzwi na moto kana kwamba yeye amekuwa ni karatasi!!

6. Mtu anayeweza kuamushiwa hii inayoitwa "hisia ama hasira zake" na eti kutaka naye kulipiza kisasi eti kwa sababu makaratasi yaliyopachikwa na binadamu jina la "kitabu kitakatifu" yanechanwa au kuchomwa moto na mlevi fulani, hakika huyo mtu hapana jina jema linalomfaa kuitwa zaidi kuwa a useless chicken head, mtu asiyemjua Mungu Mtakatifu wala namna anavyotenda kazi katika maisha ya watu...!!

7. Umesema kweli, kuwa, kile ambacho ni kitakatifu kwako siyo lazima kiwe kitakatifu kwangu....
 
Mwambie Mtoa Mada asome kifungu namba 24 cha sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…