Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Kwa waliosikiliza kilichosemwa leo tayari serikali ya CCM na viongozi wake wapo mguu ndani mguu nje. Wanaondoka na tuseme wanaondolewa au neno zuri la kikwetu wanafurushwa na haizidi mwaka...
Wanampangia Mungu, ngoja tuone
 
Jamaa kakasirika sana anarusha vigogo na kubwa ni kuwa kazi waliyopewa imeharibika mambo ya uchaguzi yamemwagika hali haikuwa shwari wala haikuwa na uangalifu.
Yajayo yatawashangaza .
 
Kwa waliosikiliza kilichosemwa leo tayari serikali ya CCM na viongozi wake wapo mguu ndani mguu nje. Wanaondoka na tuseme wanaondolewa au neno zuri la kikwetu wanafurushwa na haizidi mwaka. Kilichosemwa leo kwa ufupi wana uhakika gani kama watamaliza miaka mitano ? Akili kichwani mwako ongeza za kuchagiwa.
Mkuu tusaidie ambao hatukufanikiwa kusikia kimesemwa nini?
 
Hivi safari za JK hazikuwa na Tija kwa taifa.

Hapo ndipo tunapomkosea sana Mzee wetu Kikwete...

Sipingi moja kwa moja safari zake huko nje, ila nyingi zilikuwa zinaepukika. Maelezo yako ni mazuri na una Utetezi wa nguvu kwake, ila safari zake nyingi zilikuwa zinaepukika maana kulikuwa na waziri wa mambo ya nje.
 
Kuwachagua marais vijana sana kwa katiba tuliyo nayo na sheria za mafao ya viongozi wa ngazi za Juu ni hasara kubwa sana.

Tuangalie sasa maslahi ya Taifa na sio maslahi ya mtu.

Mfano tunaweza kumchagua Jafo kuwa Rais wa nchi. Akastaafu baada ya miaka kumi kama marafiki zake watakubali kumuona rafiki yao anayewapa ulaji akiachia kitu. Lakini wakiona vipi watapiga kampeni aongezewe muda awe raisi wa kudumu.

Kama Katiba itafuatwa Kiongozi mwenye umri mdogo kama Jafo au makamba au Mwigulu Nchemba Au Zito Kabwe ni kwamba atastaafu akiwa na miaka 55 au 60.

Miaka 60 Mungu akimjalia akaishi umri wa miaka 90 basi serikali itaendelea kumtunza kwa muda wa miaka 30 mbele wakati huo marais wengine watatu watakua wamestaafu.

Tunaweza wakati mmoja tukajikuta tuna marais wastaafu 30 kwenye nchi na mawaziri wakuuu na makamu wa raid n.k. wote wakajengewa majumba ya mabilioni huku wakiendelea kulipwa 75% ya waliopo madarakani.

Hapana hii haifai hata kidogo. Wapo watu wenye umri wa miaka 60 mpaka 70 wenye uwezo mkubwa tu wa kuongoza. Tunahitaji viongozi sio watawala wa kutufokea na kututisha . Magufu ni ya majeshi . Hata maCDF kwenye nchi zilizostaarabika ni watu wenye umri zaidi ya miaka 55.

Kwa Marekani ,Israel,urusi n.k. Mtu kama Warioba ,sumaye, Pro. Safari, Bado anaweza kugombea na kuongoza watu kwenye mifumo imara ya nchi.

Hawa vijana wapewe nafasi za Chini kwanza wajifunze kuwa wanaongoza watu na sio ngombe kama Morani.

Afrika tunakwama sana kwa sababu ya kutaka kutawaliwa badala ya kuongozwa, kutawala badala ya kuongoza.
 
Kwa gesture ya Dkt. Mwinyi pale alipokaa ni kama ana woga au hofu fulani hivi, kama haamini kinachotokea maana muda wote anasugua viganja huku akitupa jicho huko na huko.

Kweli damu za watu si mchezo, lazima zikuamishe kimawazo!
Huyu jamaa ana nidhamu ya uoga kinoma . Umesahau na kujichekeshachekesha bila sababu
 
Hata kazi ya urais haina guarantee, wanyonge wakiamua hata kesho wanakuhamisha Ikulu.
 
Ki ukweli kabisa, mtindo anaoenda nao Raisi, ulipaswa kuwa msingi wa Taifa letu!!

Mtanzania huwa tunamazoea mabaya, utasikia mtu anasema ni Moto tu wa mabua, Maana yake ni kwamba kuna mazoea au mienendo mibovu ambayo baada ya mabua kuisha na Moto wake unakoma, uzembe unarudi pale pale, wizi pale pale n.k

Sasa Kwa Aina hii ya Magufuli naomba iwe ndio msingi wa viongozi wote wakuu nchini, Maana maendeleo ya Nchi yetu tutayaleta Sisi na hata tukichelewa tutakuwa Tumejicheleweshea sisi
 
Hivi PM kwa sasa hivi amebakishiwa majukumu yapi?
Bado najiuliza kauli ya mwenyekiti wa saccos alivyosema atakuwa waziri mkuu ndani ya saa72 sijui majukumu Yake yangekuwa yepi!
Angekosa wa kumsingizia akilewa.
 
Back
Top Bottom