Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, ninamwomba Mh. Rais Magufuli atoke hadharani na atoe kauli kuhusu hili suala la watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kucheza na katiba yetu. Wakitaka aidha kuondoa ukomo wa muda wa uraisi au wakitaka kumwongezea muda wa kusalia madarakani.
Ikiwa MH Rais hayuko nyuma ya hili Jambo la kiwendawazimu na ikiwa anaiheshimu katiba aliyoapa kuilinda basi kwa heshima namwomba atoke hadharani rasmi na awakemee wote wanaosuka mpango huu. Tena wakijinadi kwamba watamlazimisha Mh.Rais.
My.Rais ukiiheshimu katiba na kipindi cha miaka yako kumi kikiisha ukaondoka,basi utaondoka kwa heshima iliyotukuka.
MH.Rais endapo hutatoka hadharani ukalizungumzia hili basi sisi wananchi tutaamini aidha uko nyuma ya mpango huu na kama hauko nyuma ya hili na hujawatuma Hawa watu basi tutaamini unapenda hili lifanyike.
Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.
Nini mtazamo wako.