Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Wengine hatupo huko
Wewe uliyetembea huna hata tupicha twa maendeleo na sisi tukaona sharing is caring

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Hiyo miradi iko wapi?au macho unayo peke yako ,nchi ameipatia wapi kuongeza umaskini na ufukara, kashindwa kuajiri , kupandisha mshahara ,kuteka ,kuua ,kufunga kwenye viroba ,kaharibu uchumi , mzunguko wa pesa ,kuvunja sheria na katiba ,kuteua watu wa hovyohovyo , kaharibu mahusiano ya kimataifa , kaharibu uhusiano na wawekezaji ,kesi 13 London , Siasa za chuki , visasi ,ubabe ,ukiukaji wa demokrasia na utawala bora ,wizi wa tilioni 2.4 , kivuki kibovu ,bombafdia za kuvutwa na kamba .
 
Utaiona vipi kama uko JF muda wote!! Tembelea TZ
 
Amelaaniwa mtu yeyote amtegemeae mwanadamu ..
 
Tangu Magufuli awe rais sijaona faida kwa taifa bali ni hasara tupu. Watu wanauawa, kupingwa risasi, kupotea na kutekwa ndani ya miaka 3. Akitawala miaka 10 ukweli atatumaliza.
 
Ukinitajia mradi wowote mkubwa unaoendelea iringa,njombe au mbeya tangu awamu hii ianze najitoa jf
Hakujawahi tokea serikali yenye kujali manendeleo kama hii ya tano tukiachana na baba wa taifa

Rais wa sasa kaiwezea tanzania kila unapo safiri ndani ya tanzania lazima kuna mradi mkubwa wa maendeleo una tekelezwa

Na hiki ndicho watanzania tunataka sio kukaa kwenye mitandao huku umejifungia chumban unalalamika lalamika .

Tembea uone namna nchi inavyo shambuliwa na maendeleo pamoja na ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pande zote za nchi kuna miradi mikubwa ya ujenzi inafanyika, hasa ujenzi mkubwa wa barabara ni watu wachache wanajua hilo, pesa ya serikali inafanya kazi , watu wana safiri wanajua hiki kinachosemwa
 
Nipo njiani naelekea kaskazini (Tanga) na nmetoka kùpita Daraja la Wami sasa hivi, hivi hukū kuna mradi gan unaoendelea?
 
Pande zote za nchi kuna miradi mikubwa ya ujenzi inafanyika, hasa ujenzi mkubwa wa barabara ni watu wachache wanajua hilo, pesa ya serikali inafanya kazi , watu wana safiri wanajua hiki kinachosemwa
Nitajie miradi inayoendelea kule Mtwara
 
Rais Magufuli katiba yetu ya jmt inasema urais ni miaka kumi mwisho atakaeongeza zaidi ya hapo atapaswa kuchukuliwa Kama mhaini

Kuna watu wanakupigia debe uendelee kutawala hata baada ya miaka kumi kwisha tunaomba uwakemee kwa maana wanataka kulitikisa taifa kuna mtu anaitwa mkulima huyu anataka kulitikisa taifa akemewe vinginevyo itatafsirika unavunga ila kimsingi unautaka muda wa nyongeza nje ya katiba kwa lazima.

Pia Rais tambua kwamba watanzania tuko milioni hamsini na tano hivi kweli haya sio matusi ya wazi kwamba hakuna mtu mwingine zaidi yako Kati yetu milioni hamsini na tano?

Mh Rais legasi aliyoiacha mwalimu ya kung'atuka kwa hiari ndiyo iliyoiletea Tanzania heshima

Mwinyi hakuivunja
Mkapa hakuivunja
Jakaya hakuivunja

Wewe ukiivunja kumbuka moja utaharibu na kuchafua historia ya taifa letu lakini pili ikitokea nchi ikaingia matatizoni kwa jaribio hili la kung'ang'ania madaraka wewe ndio utawajibika moja kwa moja

Mh Rais umezungukwa na wanafiki wanaokuogopa na wanaonufaika na uwepo wako Hawa wote wanakuambia unayoyapenda na kutaka kuyasikia hawakuambii ukweli

Mh Rais wakina mkulima wanajua wako salama wakijipendekeza kwako maana kinyume chake Ni maangamizo kwao watu wanaojiita mataga Ni wanafiki wa kutupwa usiwasikilize hata wanaccm wanaoimba nyonjera za wewe kubaki wanatetea mradi wao sio kweli kwamba wewe unapendwa hapana wanakuogopa na kimsingi hawakuogopi wewe wanaiogopa dola kutekwa kupigwa risasi na kubambikiwa kesi.

Ushauri wangu kwako

Muda wako ukifika ondoka kwa heshima vinginevyo mchuma janga hula na wakwao !!

Nakutakia baraka amani na upendo viendelee kutawala katika moyo wako na taifa letu kwa ujumla !!

Wasalaam!
 
Mkuu wetu wa nchi hii nchi unayoiongoza ina wananchi takribani mil 60. Kati ya hao ni 5% ni wanasiasa. Lakini wengi wao amaboa ni 95% ni wakulima na wafanyakazi.

Wewe unayo mamlaka ya kupata maoni ya nini 95% ya raia wa Tanzania wanatoa maoni juu ya uongozi wako.

Ukweli usiopingika wafanyabiashara wengi hawataki uongezewe muda hata sekunde moja. Maana tangu umeingia madarakani umekuwa mwiba kwao. Biashara zimefungwa sababu ya kutaka walipe kodi hata kama mazingira ya kibiashara sio rafiki. Kila sekta ya kibiashara imeganda.

Wakulima wapo kimya wanaugulia moyoni. Maana tangu uingie madarakani hali yao kuuza mazao imekuwa mbaya.Mazao ya nafaka mengi yamekosa soko hasa la nje ambalo ndio chanzo kikubwa cha mapato yao.

Wafanyakazi wa umma ndio wanakilio kikubwa. Wao wanaomba Mungu ustaafu hata kabla hujamaliza muda wako. Maana hujaongeza mshahara kwa miaka mitano tangu uingie madarakani. Hali ya maisha ni ngumu kwao maana maisha ni ghali.

Je kwa mazingira kama haya nani ambae ni mwananchi wa kawaida atataka uongezewe muda wa kutawala?

Hao wanasiasa wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ambao ni 5% ya watanzania? Wewe ni mkuu wa nchi. Fanya utafiti juu ya hili. Wananchi wa kawaida wanaomba Mungu miaka minne iishe haraka aje rais mwingine mwenye huruma ili maisha yaendelee. Usidanganywe na akina Jah pipo wa Njombe.
 
Je kama wanaosema amewatuma? Ni vyema kuweka akiba ya maneno
 
Kwani na yeye kaamini hili na anataka kulifanyia kazi??
 
Back
Top Bottom