Rais Nyerere na Rais Magufuli walikataa, Rais Samia usikubali Misaada ya kuingilia Sovereignty yetu!

Hakuna uchaguzi Tanzania bali kuna maigizo ya uchaguzi, chama kikubwa chadema hakishiriki uchaguzi alafu useme kuna uchaguzi hapo? bora wafute uchaguzi huu wasogeze mbele kuliko kupoteza mabilioni ya pesa bure huku wakijua hawana hawajachaguliwa wamejipachika kwa njia haramu za kishetani
 
Wana nia binafsi za kunyonya Tanganyika kwa manufaa ya familia zao.
 
Hakuna rais aliyekataa misaada katika nchi hii, Paskali hata kama unataka uteuzi usidanganye umma wa watanzania, nenda wizara ya fedha angalia misaada iliyotolewa tangu tupate uhuru. Ni mabilioni ya dola, ni nyingi na hakuna rais hata mmoja aliyewahi kukataa misaada ya EU/UK/USA. Kama watu wanaojiita wasomi (Siamini kama una usomi wowote wa maana, may be semi-illiteracy unadanganyaj, je mwananchi wa kawaida hatadanganyika kirahisi)
Acha kuandika uongo, tumia data. Ni aibu baba zima kama wewe umejaa uwongo hadi kwenye tumbo lako. SHAME ON YOU.
 
Topic ni Tanzania, hao watu wa Middle East wapambane na hali zao wenyewe. Unadhani nao wanahangaika with whatever you go through in TZ? Kila mja abebe mzigo wake.
 
Topic ni Tanzania, hao watu wa Middle East wapambane na hali zao wenyewe. Unadhani nao wanahangaika with whatever you go through in TZ? Kila mja abebe mzigo wake.
Yes na hao wazungu wapambane na hali zao wasituletee chokochoko wakati hii ni nchi huru
 
Una hela ya kuinunua ARV?
Au unataka watu wafe kama kuku?
 
Yes na hao wazungu wapambane na hali zao wasituletee chokochoko wakati hii ni nchi huru
Kwanza muache kwenda kwao na mabakuli kwa kulialia kisa mmeshindwa kujiendeshea mambo yenu bila misaada kutoka kwao, loans na grants huwa vinakuja with strings attached. Anayekulisha atakupangia tu whether you like it or not, behind closed doors wanalialia sana hao watawala wenu wakati wanaomba misaada ndiyo maana wakipigwa mikwara wanashindwa kujibu mashambulizi with the similar tone kama wanayoshambuliwa nayo. Mighty is right walisema wahenga and a beggar has no choice.
 
Unataka wampe uraji Mara ngapi ikiwa yeye huleta taarifa za nyeti kwakuwa anakaa jikoni .

Kama unakaa jikoni utashindwa vipi kula.

Mfano yule mtangazaji wa wasafi ,pasko n.k wapo wengi
 
Hiyo nchi unayosema inaua watoto siyo huru? Kwa hiyo kuwa huru ni kutokemewa ukifanya mabaya..hiyo ndio maana ya kuwa huru, mbona majanga yakitokea wanapokuja kusaidia husemi sisi tuko huru..? Acha kujitia ujinga..hakuna nchi itahoji km unatenda haki kwa watu wako..! Pili kabla hujaona ubaya wanaofanyiwa palestina ona na kemea ubaya unaofanyika hapo ulipo! Mambo ya wapalestina waachie wenyewe..lini uliwasikia wao wanakuongelea wewe mambo yako..?
 
Wameiba sana rasilimali zetu na wanaendelea kuiba , mikopo tutakopa hata marekani ana madeni makubwa sembuse sisi tanzania
watuache kwanza tumalize uchaguzi ndio tuendelee na story zao za kinafki, uhuru wetu tutaulinda kwa gharama yoyote
HUyo anayoongelea haki wanaishi kwa kuuwa watu kila siku ,wapuuzi watupu
 
Nani aliyemzungumzia mwenzake?
Kwani hapo wamefanya nini huko bungeni kwao? Si wameongelea mambo ya tanzania
Wakati jambo lipo mahakamani , sisi lini tuliongelea mambo yao ya uuwaji kila siku tena mamilioni ,
Africa ya sasa sio kama ya zamani
 

Nyerere alikataa kwa faida ya Taifa. Huyu akikataa itakuwa anafanya hiyo kwa faida yake binafsi au kikundi fulani.

Siamini kama kweli Paskali unaweza kumshawishi Maza akatae misaada ili tu asifanye Reforms ili abaki Magogoni.
 
Duh!
TZ hatuna uwezo wa kukataa misaada, hata iwe na masharti gani, $8m kwanza inapigwa 10%, MWIGULU na mama Abdul, itakayobaki chukuwachakomapema, masalia kundaa uchaguzi!
Hii ndio TZ mdau!
Hatarii sana sana sana!
 

Thread 'Bunge la Ulaya laitaka Tanzania KUSITISHA Matokeo ya UCHAGUZI' GE2025 - Bunge la Ulaya laitaka Tanzania KUSITISHA Matokeo ya UCHAGUZI
Huku sio ni kutuingilia mambo yetu ya ndani ?
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…