beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa.
Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021.
Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu.