Rais Samia aagiza kuandaliwe Kanuni za Mikutano ya Vyama vya Siasa Nchini

Rais Samia aagiza kuandaliwe Kanuni za Mikutano ya Vyama vya Siasa Nchini

Huu ni muendelezo wa Sarakasi...,

Kanuni ?; Je zilizopo zinafuatwa ? Haya hizo Kanuni zitasema Polisi wasifuate inteligensia yao kama wakiona sio vema kutoa vibali ?

Au kutakuwa hakuna hitaji la Vibali ? Hapa nadhani we are just putting lipstick on a Pig...
 
Kuandaa kanuni za nini wakati sheria ipo na inajieleza vizuri?

Hicho kikao cha tarehe 15 -17 Dec 2021 Chadema hawakuwa na muwakilishi, mostly waliohudhuria walikuwa wale marafiki wa watawala.

Hapa sioni sababu ya kudanganyana, hizo kanuni Simbachawene anaandaa kwa malengo yapi? na wakina nani watakuwa waandaaji?

Nataka kuona mapendekezo watakayokuja nayo Chadema baada ya kukaa chamani yatafanyiwa kazi, vinginevyo hii serikali inaonekana bado haiko tayari kwa suluhu.
Kanuni za nini!!?? kwani KWA miaka HII 60 mikutano ya siasa haikuwa na kanuni!!??nini kiliharibika kwani!??waache ujinga Hawa jamaal!!
Magufuri aliharibu Sana kwa hili
Inavoonekana mwendazake alizifuta kanuni kimya kimya,ndiyo maana haionekani kwenye katiba,vinginevyo Kama ameakiza kanuni zitungwe sasa,inavoonekana vyama vingi ndiyo vinaanzishwa sasa.
 
Hicho zamani hakikuwepo,Ila baada ya mihadhara ya waislam kuzidi,mkapa akakiweka,ilikua unatoa tu taarifa polisi ili waje kulinda...Kuna upande ulifurahia sana
 
Hazikuwepo kanuni zinazoongoza ufanyaji mikutano zaidi ya sheria
Sasa kanuni si ndio zinakuja kupiga pin zaidi kuliko ambavyo hazikuwepo. Hivi sasa mikutano chama kinaweza kufanya kwa namna yoyote kitakavyo, sasa kanuni zinakuja ma kusema (mfano) mikutano itaanzia ukumbini tu, hakuna msafara wala maandamano.

Halafu kama Sheria haifuatwi sembuse kanuni!!
 
Waziri wa katiba na sheria ameagizwa atunge kanuni ambazo zitaratibu kufanya mikutano ya hadhara ya vyama. Vya siasa. Hivyo sasa ni ruksa.
Kanuni za kazi gani wakati Katiba ina maelekezo ?
 
Tusikimbilie kuandaa kanuni za kuogopa Vuguvugu la Katiba Mpya kwani muda huo tunaotumia kuandaa kanuni afadhali tujipange kukubaliana na matakwa ya Wananchi.
Kwani upepo auvumi vizuri tukumbuke mstakabali wa hili Vuguvugu uko mkononi mwa baadhi ya Vyama vya Upinzani kwa hiyo ccm tusijisahau kwa kuwa naona Vuhuvugu kali liko mioyoni mwa Tanzania waliowengi tusome alama za nyakati mapema bila kusombwa na mafuriko.
Mfano tangu Mbowe ametoka kuna jambo jipya kwake na tukumbuke huyu ni binadamu huwa tunabadilika kuendana vikwazo kwa ujumla Mbowe wa sasa kwa siasa za Tanzania siyoyule tuyemzoe kabla hajawa gerezani kwa hiyo tujiandae kwa kikao cha Kamati ya Chadema kwa sasa tukumbuke Siasa ya Tanzania iko mkononi mwa hiki Chama ndo maana mpaka sasa Watanzania wanajiuliza Mbowe aliongea nini na Rais.
Mstakabali umebadilika kwa kushikiliwa na Chadema kwa kupitia hiyo Kamati Kuu yao
 
Tunaongozwa na viongozi ama wasioijua katiba au ambao hawaiheshimu kabisa!
Wengi wao ni wahanga wa kipindi cha giza, waliisha nogewa na uholela.
Wandhani ETI kuvunja vunja katiba na ukandamizaji ndio uimara.
Hebu ngoja kwanza tuwaone wana muujiza gani.
 
Kila kitu kipo basi tu kampeni ndani ya kampen
 
Kama kuna uhitaji wa kanuni nyingine tena mpya, basi mchakato wa katiba mpya uharakishwe ili zitumike zilizoko huko kwenye rasimu ya Jaji Wrioba.
 
#HABARI Rais @SuluhuSamia amemwagiza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene, kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Kwani sheria ya vyama vya siasa inasemaje kuhusu haki na wajibu wa vyama vya siasa !
 
ina maana miaka yote mikutano ya kisiasa inafanyika bila kanuni yoyote ile?
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa.

Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021.

Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu.

View attachment 2148206

Nonsense. Katiba imeainisha kila kitu.
 
Back
Top Bottom