Rais Samia aagiza kuandaliwe Kanuni za Mikutano ya Vyama vya Siasa Nchini

TLS ikiwa chini ya marais Dr. Rugemeleza Nshala na Fatma Karume tuliijua ingetoa ushauri bila kupepesa macho, ila hii TLS ya Dr. Edward Hosea sijui itatoa ishauri gani
 
Ushauri pekee wa kutolewa kwa sasa ni kuiheshimu na kuifuata katiba iliyopo ambayo inaruhusu shughuli za kisiasa za vyama vya kisiasa.

Hakuna tena haja ya kuandaa kanuni!

Kanuni za nini?

Tunaongozwa na viongozi ama wasioijua katiba au ambao hawaiheshimu kabisa!
 
Sijaele
Waziri wa Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa

Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021

Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu

View attachment 2147892

Eti katiba na uchaguzi ni mpango wa muda mrefu? Kwanini ziwe mpango wa muda mrefu?. Kwa hivyo Tume huru na Katiba Mpya sio priority kwa Sasa?.
 
#HABARI Rais @SuluhuSamia amemwagiza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene, kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Hapo kwenye kanuni ndipo shida ilipo. Vyama vyote viridhie kanuni hizo maana ndio wadau wakuu.
 
Ukishawapa Wanasiasa wanachotaka, kelele zote zinaisha.

Unaweza kufikiri nchi hii matatizo yote YAMEISHA😀😀😀

Mbona mikutano ilikuwepo wakati wa JK na kelele hazikuisha, sembuse leo mikutano na mikanuni juu? Kelele haziwezi kuisha mpaka kila mtu apate haki yake.
 
Ukishawapa Wanasiasa wanachotaka, kelele zote zinaisha.

Unaweza kufikiri nchi hii matatizo yote YAMEISHA😀😀😀

Uko sahihi kabisa mkuu, wanasiasa wanajua kutetea maslahi yao. Ni juu ya hayo makundi mengine kupigia kelele maslahi yao. Ajabu utakuta hayo makundi mengine yako kimya yakisubiri wanasiasa ndio wawasemee! Mfano mrahisi ni wakulima na wafanyakazi. Hawa wako kimya wanaburuzwa kama magunia mabovu.
 
TLS ikiwa chini ya marais Dr. Rugemeleza Nshala na Fatma Karume tuliijua ingetoa ushauri bila kupepesa macho, ila hii TLS ya Dr. Edward Hosea sijui itatoa ishauri gani

Wenyewe hawatatoa ushauri wowote, bali watamuuliza rais anataka nini, kisha wao wataiweka vizuri kisheria.
 
Ukishawapa Wanasiasa wanachotaka, kelele zote zinaisha.

Unaweza kufikiri nchi hii matatizo yote YAMEISHA😀😀😀
Wanasiasa wanyo platform kubwa ya kuongea tofauti na makundi mengine, wakishapewa hayo mahitaji yao hutosikia tena kuwatetea wananchi wanyonge wa nchi hii
 
Bado anatokea mmakonde mmoja na kusema wanawake ni viumbe dhaifu, wakati kila mianaume ya upinzani inaitwa ikulu na huko kwa mabeberu kisha inainamishwa vichwa kwa sauti laini inakuwa miimba mapambio.

Hata Samson na miguvu yake aliwezwa na mwanamke mmoja tu legevu legevu kimuonekano, the same kwa Zitto, Mbowe na Lissu.

Maendeleo hayana chama

Unamkosea Sana Rais Samiah kwa kumfananisha na kahaba. Kwamba anawatongoza wanaume kwa sauti yake ili wakubali kulala naye. Samiah anatembelewa kwa mamlaka aliyo Nayo sio kwa sauti yake.

Mbowe hakwenda kumuona Samiah bali alienda kumuona Rais wa nchi. Yule ni rais wa nchi achana an uanamke wake. Mbona hakua na hiyo nguvu alipokua makamu wa Rais. Tena akaenda kumsalimia Lissu Nairobi.

Unapokuwa Rais una mamlaka juu yako hata Kama ni mlemavu wa macho au miguu. Ndio maana leo Kikwete hawezi kucommand chochote maana Hana mamlaka. Ukitaka kujua mamlaka Ni Nini muulize makonda wa Sasa hivi anayelia kuzurumiwa kiwanja.
 
Waziri wa Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa

Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021

Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu

View attachment 2147892
Nchi hii tukiwaambia Rais ana madaraka ya kulevya wapo wenye umaskini wa akili hawaelewi.
Kuna haja ya kupatikana Katiba Mpya na Bora itakayoweka ukomo wa madaraka ya viongozi akiwemo Rais wa nchi.

Naomba usome ukitambua kuwa SSH vile vile ni mwenyekiti wa ccm (conflicting interests).
 
Kwa uzoefu wangu wa Siasa…sasa hivi watu wanajiandaa kula Nchi sasa maana wapiga kelele wote wanatafutiwa kivuli cha kupoza njaa

Kelele zipi?. Kelele haziwezi kuisha hata Viongozi wote wakiingia serikalini. Hata kenya walidhani kelele zitaisha kwa Handshake lakini Leo ndio zimeongezeka.
 
Waziri wa katiba na sheria ameagizwa atunge kanuni ambazo zitaratibu kufanya mikutano ya hadhara ya vyama. Vya siasa. Hivyo sasa ni ruksa.

===

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Machi 12, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi Machi 12, 2022 baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka kikosi kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa uliofanyika Desemba 15-17, 2021 Dodoma.

Rais Samia amemwagiza Waziri huyo kushirikiana na Tanganyika Lawa Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.

“Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 24, na ambacho kinawajibika moja kwa moja kwa Mhe. Rais, kiliwasilisha maazimio hayo Ikulu Jijijni Dodoma. Maazimio hayo yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa azimio la muda mfupi ni uandaaji wa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

“Baadhi ya maazimio ya muda wa kati ni pamoja na rushwa na maadili katika uchaguzi, ruzuku, elimu ya uraisa, huku masuala yanayohusu uchaguzi wa katiba mpya vikiwa ni mpango wa muda mrefu”

Mwananchi
 
Kiukweli kibali cha kufanya mkutano wa Siasa kutolewa na polisi siyo fair ndio maana inaonekana kana kwamba CCM inapendelewa na PT wakati siyo kweli.

Napendekeza kanuni hii isiwemo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuandaa kanuni za nini wakati sheria ipo na inajieleza vizuri?

Hicho kikao cha tarehe 15 -17 Dec 2021 Chadema hawakuwa na muwakilishi, mostly waliohudhuria walikuwa wale marafiki wa watawala.

Hapa sioni sababu ya kudanganyana, hizo kanuni Simbachawene anaandaa kwa malengo yapi? na wakina nani watakuwa waandaaji?

Nataka kuona mapendekezo watakayokuja nayo Chadema baada ya kukaa chamani yatafanyiwa kazi, vinginevyo hii serikali inaonekana bado haiko tayari kwa suluhu.
 
Wanasiasa wanyo platform kubwa ya kuongea tofauti na makundi mengine, wakishapewa hayo mahitaji yao hutosikia tena kuwatetea wananchi wanyonge wa nchi hii

Hao wananchi wao ni maiti hai hawawezi kujitetea?
 
Kwani hakukuwa na sheria za mikutano hapa nchini...?????maana katiba imeeleza vyema kabisa hili swala

Au ndio wanataka waweke Tozo kwenye mikutano...
 
Waziri wa Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa

Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021

Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu

View attachment 2147892
Kheee

IMG_20211029_105959.jpg
 
Mikutano ipo kisheria kbs, hizi kanuni za wap tena!!
Waziri wa Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa

Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021

Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu

View attachment 2147892

Screenshot_20220312-153728.png
 
Back
Top Bottom