Rais Samia aagiza kuandaliwe Kanuni za Mikutano ya Vyama vya Siasa Nchini

Take that, bitch!







 
Sheria ya Msajili wa vyama Part IV (11)(a , b) imeeleza wazi kwa tafsiri isiyo rasimi
'' (a)Chama chenye usajili wa muda au kamili kina haki ya kufanya mikutano katika eneo lolote la Jamhuri kwa kutoa taarifa kwa polisi ofisa wa eneo husika kwa minajili ya kujitangaza au kutafuta wanachama (b) Kwa kupata ulinzi na msaada wa usalama ili kufanikisha mkutano kwa amani na taratibu.

Hakuna mahali imesemwa Polisi watatoa kibali cha mkutano. Polisi wamejivika tu jukumu hilo kinyume na sheria
Sawa, hapo ndipo Polisi wanatakiwa wamchukulie mhusika sheria wakiwa na ushahidi si maneno ya kipuuzi kama vile tishio la ugaidi Simiyu.
Kama kuna mtu anavunja sheria kuna taratibu za kisheria za kumshughulikia , si Ramli za kwamba kutatokea vurugu.

Polisi ndio chanzo cha matatizo. Mfano, Mbowe alipokamatwa ilikuwa kila siku kuna 'tension' mara apelekwe kwa njia hizi mara zile.

Kesi ilipofika katikati Polisi na Magereza wakaacha kumkimbiza Mbowe.
Wafuasi wao wakawa wanakula sijui chakula na kuimba nyimbo.
Polisi na Magereza walilinda usalama wa Mbowe na Wafungwa na kulinda usalama wa wafuasi

Hakuna hata siku moja imetokea vurugu! Hivyo ndivyo Polisi wanatakiwa wafanye

Kinyume na hilo Polisi wanapiga RAMLI, kutatokea vurugu, kuna intelejensia n.k. wakati mkutano ni wa ndani na watu wamekaa hakuna tatizo

Fikiria yule Polisi aliyetaka Wanawake wa Chadema waondoe bendera , hivi anajua sheria kweli
Polisi yule alitaka nini kama si kuzusha vurugu!.
 
Duh!mkuu mbona kama una chuki zako binafsi
Siyo kwamba wewe ndiye mshamba! [emoji848]
Hawa nyumbu wakiishiwa na kuzidiwa hoja, huanza viroja!

Mtu anadai sikuwahi kumkosoa Magufuli vikali.

Nimemwonyesha jinsi nilivyomkosoa Magufuli kwenye mambo mbalimbali. Kaishiwa hoja. Kabaki na viroja tu sasa.

Kuna wengine waliwahi kusema kuwa sijawahi kumsema Magufuli alipokuwa anaendesha vikao vya CCM ikulu lakini ile majuzi eti nimemsema Samia.

Nilipowaonyesha hii mada hapa chini, wote wakala kona 🀣🀣🀣

 
Unaweza kuwa unakanyaga sheria nyingingine za usalama wa raia kwa kuinua sheria moja tu ya mikutano ya siasa. Jukumu namba moja la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, na kuzuia uharifu ndani ya jamii. Sheria hiyo ya mikutano ya siasa haisemi kuwa chama kikitaka kufanya mkutano lazima kipewe ulinzi wa polisi, ila sheria ya mikusanyiko ya watu hadharani ndiyo inayowataka wapate ulinzi wa polisi.

Sasa iwapo polisi hawatakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa ulinzi huo, basi mkutano hautafanyika. Siyo kwa sababu ya sheria ya msajili wa vyama kutotekelezwa, bali kwa sababu ya sheria ya polisi kuhusu mkusanyko wa watu hadharani. Sikumbuki sheria hiyo vizuri kichwani mwangu, ila ninajua kuwa ipo.

Hayo makosa ya polisi mmoja mmoja kwenda kinyume na maadili ya majukumu yake ni tatizo moja kubwa sana kwenye jamii yetu linalohitaji kushughuilikiwa mara moja. Kweli kuna polisi wengi wanaotumia madaraka yao vibaya ama kwa kutaka rushwa au kutaka kujionyesha ubabe. Makosa hayo ya polisi mmoja mmoja yastumiwe kama makosa ya serikali na jeshi zima la polisi
 
Kila Mara ni kuingiza igizo mpya kwa kila kitu kama Wana mziki na rekodi mpya. Sijui hii ni single au album, ikiwa single maana yake utekelezaji ni wa haraka lakini kama ni album basi utekelezaji ni after 2025. Tusubirie na tuone.
 
Mbona utaratibu wa kufanya hayo upo!

Why are these people reinventing the wheel???

Katiba, hata kama ni pungufu na iliyopitwa na wakati, ipo lakini haifuatwi.

Hiyo mpya ndo itakuwaje sasa?

Huu ni ujuha.
Wanataka wazilete taratibu zilizopindishwa na kuzifanya ni rasimi. Taratibu zilizopo wanaogopa kuzifuata. Wanataka kurekebisha taratibu za mikutano ya siasa, mbona ni waoga kukubali kurekebisha Katiba ya nchi na taratibu za uchaguzi? (Tupate Tume huru ya uchaguzi).

Tumesikia wanataka kurebisha pia Katiba ya CCM, lakini KATIBA ya nchi hawaoni haja ya kurekebisha.
 
Mbona utaratibu wa kufanya hayo upo!

Why are these people reinventing the wheel???

Katiba, hata kama ni pungufu na iliyopitwa na wakati, ipo lakini haifuatwi.

Hiyo mpya ndo itakuwaje sasa?

Huu ni ujuha.
Umetoa hoja muhimu sana! Rais aache kukataza mikutano iliyopo kisheria na kanuni zipo. Hawezi akawa anavunja sheria iliyopo halafu atake sheria itungwe kwa jambo lilelile!

Tufuate iliyopo na kuiboresha ikibidi.
 
Kwahiyo watu wote hawana akili,mwenye akili ni wewe tu?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
🀣🀣🀣🀣
Pep njoo uwasaidie nyumbupori kusoma hizi mada.
Mada zimewekwa ila bado wanabishaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
 
Nadhani hiyo haki kuna watu waliitumia vibaya, sasa ni muda muafaka wa kuangalia hiyo mikutano inafanyika vipi, haiwezekani baada tu ya uchaguzi nchi nzima ianze kampeni kwa uchaguzi ujao

..kampeni za uchaguzi zina kipindi maalum, na sheria, na taratibu zako.

..basically shughuli za kisiasa zinazofanyika kabla ya tume ya uchaguzi kutangaza kuwa kuna uchaguzi haziwezi kuitwa kampeni za uchaguzi.

..pia sio makosa kwa vyama vya siasa kufanya jitihada za kujiimarisha kwa njia ya mikutano ya hadhara, makongamano, warsha, mafunzo, etc ili viweze kufanya vizuri zaidi ktk chaguzi mbalimbali.
 
Hakuna hata siku moja kanuni za sasa zimelalamikiwa! hakuna
Kilicholalamikiwa ni matumizi mabaya ya mamlaka kama Polisi na Serikali kukiuka kanuni zilizopo

Kuandika kanuni mpya kuna lengo moja, kuandika mambo yatakayowabana Wapinzani

..binafsi napenda kujua kama hizo kanuni mpya zinatoa uhuru zaidi kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zao au la.
 
Mbona utaratibu wa kufanya hayo upo!

Why are these people reinventing the wheel???

Katiba, hata kama ni pungufu na iliyopitwa na wakati, ipo lakini haifuatwi.

Hiyo mpya ndo itakuwaje sasa?

Huu ni ujuha.
Wanapigwa mark time tu, one step forward, two steps backwards.

Hakuna kitu hapo.
 
Moja ya michango yako yenye maneno kagumu toka wewe kuingia jf ni hii aseee
Mzee mwenzangu umekutwa na nini tena aseee
Ni utapiamlo wa akili kumwita 'Rais' mtu ambae yupo busy kuhamasisha ufisadi katika Taifa.
Your browser is not able to display this video.
 
Yaani Hii nchi bana!

Rais anaweza kui suspend katiba vile ajisikiavyo. Anavunja katiba vile ajisikiavyo.

Halafu anaunda isiyo na kichwa wala miguu kufanya kazi ambayo tayari ilishafanywa!
Kwa kuwa wengi hawajui tunakotakiwa kwenda basi kila njia waelekezwayo kwao ni sawa tu...!
Kanyaga twende, SSH!
 
#HABARI Rais @SuluhuSamia amemwagiza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene, kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Mara Simbac'wene mara Pindi Chana; yupi anahusika?
Na hizo kanuni si kama za Tume ya Uchaguzi Mkuu ambazo watakaoweza kuzielewa ni team CCM pekeyao? Hii ni kusogeza magoli ili timu teule ishinde!
 
Aisee

Ngabu amechafukwa 🀣🀣🀣
 
🀣🀣🀣🀣
Pep njoo uwasaidie nyumbupori kusoma hizi mada.
Mada zimewekwa ila bado wanabishaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
Nyumbupori? hao ndo wakoje? maana sijawahi ona nyumbu ambaye sio wa porini 🀣🀣

Sema hawa wanaingia hadi JF wametisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…