Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Cheti Ni tatizo, Lakini dogo! Suala la msingi wamefanya kazi zinazostahili malipo na hatimaye mafao, ambayo kimsingi yamekatwa kwenye mapato yao?! Kwani Ni cheti, kiwe original Au fake, kilicho fanya kazi?
Na mshahara wa nchi yetu hulipwa mwisho wa mwezi, kwa maana muajiri ameridhishwa na utendaji wa kazi aliyompa ndipo akamlipa mshahara hivyo cheti hakihusiki hapa. Madai yao wapewe na kama walighushi vyeti wapelekwe Mahakamani wao na waajiri wao. Kwanini awasiliane cheti feki na kwanini muajiri aridhie cheti feki!
 
Siwezi kuvaa viatu vya majizi ya kitaaluma.

Mimi nimesoma nimeenda shule bwana. Siwezi kuwa sambamba na majizi ya vyeti.

Tumeelewana? Au niongeze sauti ya redio?
Wewe ni msomi cheti. Ndio nyie mnaharibu biashara za watu kisa mnataka kudhihirisha usomi wenu.
 
Hizo pesa zipo au ni mashairi ya jukwaani tu
Kuna pesa nyingi zilizoibwa na marehemu. Kuna pesa 1.5 trillion aluzogundua CAG kuwa hazieleweki zilienda wapi.

Kuna pesa walizoporwa wenye mafuka ya kubadilidha pesa. Hizi zilienda moja kwa moja kwa marehemu na watu wake wa karibu.

Kuna pesa ziluzoporwa toka kwawaliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi. Hizi zilikusanywa na Mganga, na kupelekwa kwa marehemu. Haijulikani alikiwa anazipeleka wapi! Lakini kuna taarifa kuwa kulikuwa na mabilioni ya pesa taslimu kwenye chumba kimoja huko Chato. Japo Serikali inajaribu kuficha, siku moja ukweli utakuwa kujulikana.

Tunahangaika dhidi ya vyeti bandia huku wevi wa matrillion bado wapo kwenye ofisi. Haya matrillion yaliyoibwa na marehemu, marehemu hajaenda nayo kaburini, serikali ichunguze yapo wapi. Mganga ndiyo mtu wa kuanza naye.
 
Ni ngumu kujikita kwenye mada ya vyeti feki. Maana humu wamejaa wezi wa taaluma wanaolilia huruma za wanasiasa.

Mimi nazungumza kuhusu umuhimu wa taaluma halali.

Kwanza inakufanya unajiamini muda wote. Hauwi na mashaka ya kutimuliwa kazini.

Lakini ukiwa na mavyeti feki unakuwa na msongo wa mawazo. Unaweza shangaa umetiwa hatiani na kushughulikiwa hata hayo mafao usiyaone.

ELIMU ELIMU ELIMU.
Hapa sitetei vyeti feki, nasapoti utaratibu ufuatwe katika kuadhibu kosa lililotendeka na kama haukufuatwa basi ili jambo limalizwe kwa kutumia busara. Samia katumia hiyo busara kwa kupendekeza walipwe hiyo 5% waliyokatwa ili tuufunge huu mjadala.

halafu kuhusu kujiamini, Katika sekta binafsi(Yenye uzalishaji kuliko serikali) hofu ya kutimuliwa kazini inatokana na ujuzi na utendaji si vyeti.

Ukishakuwa na ujuzi hata sheria zikilazimisha vipi mwenye vyeti aajiriwe ataajiriwa ila atakaa hapo kama pambo na kulipwa pesa kidogo kwa ajili ya vyeti tu, kuna mtu mwenye ujuzi na uzoefu atakuwa mastermind.

Tanzania tunatakiwa tujenge ujuzi wa vijana wahitimu wetu ndipo masuala ya vyeti yafuate. Sisemi tuwe na vyeti feki, nasema vyeti halali viambatane na ujuzi.

Hii itaondoa Pride kama hii unayoionyesha hapa kwamba ukiwa na vyeti umemaliza, vijana hawatashindana kufaulu mitihani, watapambana kupata ujuzi.
 
Walipwe haki zao mbona Bashite aliendelea kufanya kazi na huku anavyeti fake na wengine PhD fake!

Hongera Mama Samia kwa moyo mzuri Mungu atakulipa!
 
C
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
CCM wanaandaa mpango wa kupiga pesa kwa ajili ya 2025.
 
Safi sana mama.

Mwenyezi Mungu akubariki sana.

Wenye vyeti feki si wakosaji kuliko mafisadi waliotuibia mahela mengi na wako mtaani wanatanua!
 
Kwa Haki vipi na cheti FEKI?
Halikua suala la vyeti feki, project ilikua ni kupunguza watumishi serikalini ili kupunguza wage bill iende kujenge madaraja na viwanja vya ndege

Cheti feki maana yake bandia, mtu hakusoma lakini katengeneza cheti mtaani akapeleka kuombea kazi

Hawa walisoma taalima zao na vyeti halali vya taaluma wanavyo, lakini tu kabla ya kusoma chuo walitumia vyeti visivyo vyao kuingia form 5 na wengine walitumia vyeti vya darasa la 7 visivyo vyao kuongia form 1
 
Utajiju na mavyeti yako feki.

Kusoma raha bwana unakuwa unajiamini tu muda wote!

Lakini ukiwa una mavyeti feki unabaki kujiliza liza tu na kuomba huruma za wanasiasa!

Mara sijui fidia ya makato! Mahangaiko kweli kweli.

Someni muonje utamu wa taaluma. Ni mwendo wa kujiamini tu.
Sukumagang mkitaka kufeni, Lakini Mazaa atapangua moja baada ya jingine mpaka asafishe mabaya yooote ya Baba yenu! Na watalipwa utake ukataye!
 
Ndio maana watoto wetu wanajazwa ujinga mashuleni shauri ya walimu feki.

Unakutana na mtoto hawezi hata kujieleza lugha inayoeleweka kumbe shida imeanzia huko kwa walimu wenye vyeti vya kugundisha na gundi steshenari.

Ahsante JPM kwa kuwatimua hawa makanjanja.

Na hizo stahiki hampati ng'ooo! Ngoja. Tutaelewana tu.
Ujuuzi huwezi ufoji,kama ujui ujui.
Unamuondoa vipi kazini Mwalimu mwenye PhD amekaa darasani miaka 20 kisa eti cheti cha form four jina limekosewa una akili wewe?
 
So zito alipotoa lile agizo alikuwa na confidence akijua hana wa kumuuliza
 
Back
Top Bottom