Rais Samia aagiza Wazazi waliofiwa na watoto 4 kwenye ajali watibiwe kwa VIP Class Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote nchini!

Kiki za kishamba sana, watengeneze mazingira watanzania wote waweze kupata huduma nzuri.... Hawa watu wamewahi kufika vijijini kweli? Wamefuta bima ya mtoto.... Wakatuwekea ma package ya ghali kweli... Yaani ujinga ujinga tu
Pumbavu! Hata Ulaya, Marekani na Asia sio raia wote wanapata VIP Treatment!
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako

Jambo jema, but why VIP?
 
Kiki za kishamba sana, watengeneze mazingira watanzania wote waweze kupata huduma nzuri.... Hawa watu wamewahi kufika vijijini kweli? Wamefuta bima ya mtoto.... Wakatuwekea ma package ya ghali kweli... Yaani ujinga ujinga tu
Si mupate ajari mitanzanzania yote, munangoja nini? Katorewa kafala Yesu itakua nyinyi?
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza Mzee Hashimu Msuya na Mke wake ambao ni Wazazi wa Watoto wanne waliofariki usiku wa kuamkia August 03,2023 baada ya gari (Toyota Prado) walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam, watibiwe kwa hadhi maalum (VIP Treatment) kwenye Hospitali za Muhimbili, JKCI na wasisumbuliwe kimatibabu kwenye Hospitali yoyote nchini.

Akiongea leo wakati wa Ibada ya kuuga miili ya Watoto watatu, RC wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema “Mh.Rais wakati ananituma hapa alisema nimesoma kwenye mtandao Watoto wale walikuwa wanawalea Wazazi wao, walikuwa wanawapeleka Hospitali na akaniambia niongee na Prof.Janabi wa pale Muhimbili, niongee na Dkt.Kisenge wa JKCI kwamba Wazazi hawa wapate VIP treatment watakapokwenda Hospitali pale" Na jukumu hilo akaniambia waambie na Wakuu wa Mikoa wengine wote mahali popote watakapokuwepo Wazazi hawa wasiwe na mnyororo mpana wa kusumbuka mwisho wataanza kuwakumbuka Watoto wao kama sisi tutaendelea kutokuwa faraja yao

"Miili ya Siah Hashimu Msuya (53), Diana Sukulu Mageta (47) na Dkt. Norah Msuya Mumburi (45), imeagwa leo Dar es salaam na mwili wa Kaka yao (Dereva wa Prado) ambaye walipata nae ajali hiyo, Neech Hashim Msuya ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Benki ya ABSA tayari umeshazikwa Jumapili katika Kijiji cha Msangeni Ugweno Wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
 
Mihemko tu,vipo vya msingi vya kuagizwa na raisi kuliko hivi,kuna malalamiko ya huduma mbovu kwenye gov hospitals hizi ndiyo changamoto anazotakiwa azitolee kauli hizo favour akaachia waziri wake wa afya azigawe.

Ni mayatima wangapi tunawajua mitaani hawana wa kuwatibu?hao wazee kwa vyovyote wanaweza kufaidika kwa amana walizoachiwa na watoto wao au ikiwa walikuwa waajiriwa kuna mafao yao.
 
Ni kweli lakino hapa amesimama.kama been nadamu na sio raisi 🙏
 
Sijui kama itakuwa, kwa hii nchi sijui.

Pole tu wazazi mlioondokewa na watoto.

Mungu awatunze tu.
 
Mihemko tu,vipo vya msingi vya kuagizwa na raisi kuliko hivi,kuna malalamiko ya huduma mbovu kwenye gov hospitals hizi ndiyo changamoto anazotakiwa azitolee kauli hizo favour akaachia waziri wake wa afya azigawe.

Ni mayatima wangapi tunawajua mitaani hawana wa kuwatibu?hao wazee kwa vyovyote wanaweza kufaidika kwa amana walizoachiwa na watoto wao au ikiwa walikuwa waajiriwa kuna mafao yao.
Ukumbuke tu Rais ndio Mfariji wa nchi, anatimiza wajibu wake wewe ndio una mihemko
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako
MBONA WAZAZI WA AINA YA HAO WAPO WENGI SANA AU KWA KUWA HAWAJATANGAZWA?
 
Back
Top Bottom