Rais Samia; Achana na hoja ya Haki Sawa inakupotezea Ushawishi ndani ya jamii

Mama ana-sound hopeless kabisa yaani... Ajikite kwenye hoja za kimaendeleo!
 
SSH bado ni mshamba wa Urais. Akimaliza hicho kipindi anaweza kuwa kiongozi mzuri sana.
 
Samia ni dikteta anaeumiza watu kuliko dikteta Magufuli:

1.Dikteta Samia amepiga pini mikutano ya ndani ya vyama vya siasa ambayo ipo kwa mujibu wa sheria.

2.Dikteta Samia anabambikizia wapinzani kesi.

3.Juzi serikali imetishia watu huko twitter kuwa ni marufuku kutoa maoni yao kitu ambacho ni kinyume na katiba yetu.

4.Dikteta Samia anatumia fedha za umma bila budget kupita bungeni wala wananchi kuambiwa matumizi(refer royal tour)

5.Wasiojulikana wamerudi tena kama enzi za dikteta Magufuli.Refer Moses Lijenje ambae mashahidi wamedai mahakamani kuwa amepotezwa.

6.Dikteta Samia anaficha wananchi mambo ya msingi sana yanayoendelea hapa nchini,mfano juzi kuna kero za muungano zimetatuliwa lakini hakuna anaejua kilichofanyika au pia kwenye ishu ya gaidi Hamza hakuunda tume huru.

7.Dikteta Samia ameshaiweka mahakama mfukoni mwake.Refer alivyohojiwa na BBC na kudai kuwa Mbowe ni gaidi na kudanganya dunia kuwa washtakiwa wenzake na Mbowe tayari walishahukumiwa.Hii ni kuenfluence mahakama.

8.Dikteta Samia ameshaviweka vyombo vya habari mfukoni mwake.Katika kesi ya Mbowe hakuna TV wala radio inayothubutu kwenda live achilia mbali magazeti kuripoti mwenendo wa kesi hiyo kwa uwazi.

9.Dikteta Samia anakaba koo wanaume.Hataki kuwasikia wakati ni raia wa Tanzania kwa mujibu wa katiba yetu.

10.Dikteta Samia anagawa hela pasu kwa pasu kati ya Zanzibar na Tanzania bara kitu ambacho ni kinyume na katiba yetu.Refer kwenye hela ya maandalizi ya nane nane ambayo hayakufanyika na hela ikapangiwa matumizi mengine kama sijachanganya file.
 
Mwanaume hawezi kuwajibika ikiwa tayari mamlaka yake imechukuliwa au kawapa WANAWAKE.

Hata MUNGU, hawezi kuwajibika na maisha ya binadamu wakati tayari binadamu keshabeba/kajipa majukumu ya mungu.
ningejiskia faraja zaid kama ungeendelea na nini kifanyike katika harakat za rais na wenzake kuhamasisha haki na usawa kwa viumbe wote ikiwemo wanawake. ni kama unataka hilo geti lifungwe bila kujari wahusika wanaweza kupita dirishan wakibanwa! mi ni muumin wa uwepo wa kanuni zinazoheshim utu wa kila mtu. usawa katika haki. kila binadam awe independent entity. equal though not same! adui wa yote haya ni dini, mila na sheria! sio nature
 


Unajua maana na Nature Mkuu??

Nature ndio inaleta utamaduni, Mila, sheria dini, maumbile na kila kitu unachokiona.

Utu wa mwanamke upo katika uanamke wake, utu wa mwanaume upo katika Uanaume wake.
Utu wa binadamu upo katika ubinadamu wake.

Ipo tofauti baina ya Haki za binadamu na haki za mwanaume na Mwanamke. Binadamu ni General term

Ipo tofauti ya Haki za viumbe na haki za binadamu na wanyama au Mimea. Viumbe mi General term.

Huwezi sema Mnyama na mtu wanahaki Sawa kisa wote ni wanyama hiyo ni kuchanganya madesa.

Tukija kwenye umri.
Huwezi sema mtoto na Mzee wanahaki Sawa, labda uwe umevurugwa,
Watakuwa na haki Sawa zile za kiujumla ambazo ni haki za binadamu na haki za viumbe lakini kwenye kategori ya umri yupo ambaye atakuwa na haki zaidi ya mwingine, na hapo upendeleo ndipo utakapoonekana kujitokeza.
 
Inabidi hata viti maalum vifutwe au navyo viwe balanced
 
Inabidi hata viti maalum vifutwe au navyo viwe balanced


Wanawake hawapendi haki Sawa Bali wanapenda kupendelewa tuu.

Wanataka haki za kiume alafu hawataki kuvuja jasho ajabu Sana hii.

Kuvuja jasho wanaita kunyanyaswa na kukandamizwa.
 
Watakuambia wanaweza kufanya mbona
Hata Arnold Schwazneger na yeye alibeba mimba pia! Sio kuweza kufanya, wakafanye.

On a serious note, kama ni Mwenyekiti wa CCM tunataka 2025 tuone wagombea wanawake wapo sawa na wanaume kwa idadi! Wizara ya Wanawake .... ibadilishwe iwe wizara wa Wazazi .... Viti maalum vya upendeleo aviondoe. Nasema hayo kwa kuamini kuwa wanawake wanao uwezo sawa na wanaume!
 
Haki sawa hazileti dawa hospitalini. Mama anafeli wapi?
 
Mwanamke atabaki kua mwanamke tu hawezi akalinganishwa na mwanamme.kwanza hawezi kutoa maamzi bila kushirikisha mwanamme.
 
Hapo kabla alikuwa anasisitiza sana mwanamke kuchukuwa nafasi yake kama mama, pamoja na heshima kwa waume zao, ila kama amebadilika kila kukicha kama anatangaza vita, na kama wanaume ni kikwazo kwake!
 
Keshaanzisha vita baridi...mke wangu hamkubali kabisa na mie ndio najazia hapo hapo namkandia anazidi kumkataa...bi mkubwa wangu hamuelewi kabisa...
Hi tabia alikua nayo makamu wa Rais wa Museveni wa zamani ikabidi Museveni amtimue.
 
Bila shaka kuna pressure ya kiume inamuingilia.

Huyu Mama ana upeo wake mzuri tu na anajua vizuri madhara yarudiyo kwake ya kuiinua gender ya kike ila anajua ni vema aongee tu kwa sababu ya anavyokumabana navyo kama alivyokuwa anasema aliyemtangulia
"Nioombeeeeni"
 
Umeongea vema dini zote hazimpi mwanamke mamlaka,kwa wapagani ndiyo kabisa.Makundi yote ndo wapiga kura2025🤣🤣🤣🤣 .
Jiongeze mtemi Hangaya huwezi kuibadili vitabu vya dini,huwa havibadiliki.
 
Aese kaka umenena vema! Hata Huko America nilishajiuliza kwa nini kwenye mabunge yao utakuta wanawake watatu wanaume hamsini! Lakini sisi watu weusi tumalishwa maneno! sasa kazi imekuwa ngumu huko majumbani hakukaliki kila mwanamke haki sawa!
 


Hajadharau mwanaume isipokuwa amejikita zaidi kuzungumzia suala la Jinsia Jambo ambalo Kwa muono wangu sio zuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…