RAIS SAMIA, ACHANA NA HOJA YA HAKI SAWA. INAKUPOTEZEA USHAWISHI NDANI YA JAMII.
Na, Robert Heriel.
Kwa maoni na mtazamo wangu ambao kimsingi nauamini, ninaona mbele zaidi miaka kadhaa ijayo. Naomba Mhe. Rais uachane na hoja ya Haki Sawa bhaina ya Mwanamke na Mwanaume.
Nimesoma andiko lako; ni ama hujui nini linazungumziwa kuhusu concept ya gender equality au ni mtu very primitive na mwenye primitive notion ya patriarchy system. Nataka nikusaidie ili usirudi tena kumjadili Rais kitoto namna hii.
Mosi, kuanzia first wave feminism (1920) kule Marekani, watu kama Suzan Anthony, walipigania haki ya wanawake kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi. Wakafanikiwa. Second wave feminism (1960), ilihusu haki za kijamii na kifamilia.
Third na fourth wave feminism (1990-2000). Hapa ndipo unakutana na Maazimio 12 ya Beijing, Millennium Development Goals na Sustainable Development Goals (2015'230). Point ni nini? Ni kwamba ktk dhana ya usawa wa kijinsia ktk vipindi vyote hivyo hatuzungumzii mama avae wasifu wa baba wala baba avae wasifu wa mama ktk familia au jamii. Lazima muelewe.
Tunachojadili ni equal rights za kiuchumi, jamii na political arena. Tunajua hakuna usawa wa asilimia 100 unaweza hupatikana duniani ila kinachozungumzwa na kieleweke ni kwamba; mwanamke au mtoto wa kike ana uwezo sawa tena wakati mwengine kuzidi mwanaume au mtoto wa kiume. Hivyo kinachosisitizwa ni uelewa kwamba hakuna first class na second class ktk jamii kati ya wanawake na wanaume linapokuja suala la kazi. Hizi gender roles stereotype kwamba kazi hii anafanya mwanaume hii mwanamke ni culture zetu tu, hasa za KiAfrika. Ulaya na Marekani zinafutika drastically. Merkel kawa Kansela wa Ujerumani kwa miaka 16 hadi kaamua kung'atuka.
Hivyo, usawa wa kijinsia hatuzungumzii kupima misuli na kumwaga jasho kati ya wanawake na wanaume bali dhana nzima ya kwamba mwanamke au mtoto wa kike anaweza kufanya kazi nzuri tu kama au hata kuliko mtoto wa kiume au mwanaume. Family ni cornerstone ya Taifa lakini msimamizi kwa sehemu kubwa ni mwanamke. Wapo wanaume irresponsible, walevi na wendawazimu lakini mama analea. Hata huko mashambani vijijini wanawake ndiyo wakulima siye tukivuna tuna control na ku decide mauzo na matumizi ya mazao.
Hitimisho, gender and development ni taaluma. Siyo ya kujadili kichwa kichwa. Hakuna maendeleo wala kisiwa wanaishi wanawake au wanaume tu. Haitatokea. Kwa hiyo gender ni issue ya maendeleo . Lazima kuwe na full participation ya girls na boys na women na men. Full participation ndiyo inayozungumzwa ktk fursa za maendeleo ya kiuchumi, siasa na kijamii. Siyo mama awe baba au baba awe mama.
THAT'S IS MY POSITION.