Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Wametumbuliwa bhana, siyo kwamba wanahitajika jeshini. Kwa uspesho gani wali nao ??

Wamevurunda warudi wakabebe magobore huko jeshini walikotoka. Usianze kuwapamba hapa.
Binafsi ninavoona sio suala la kutumbuliwa bali ni kila utawala huwa una aina ya Mkao wake inaotaka iwe. Ndio maana Kila Rais anapochaguliwa ni mara chache sana akaendelea na wateule aliowakuta.

Na sio kwa Rais tu ila hata wakuu wapya wa taasisi wanapoteuliwa hupenda kuwa na team yao. Nadhani hata IGP na CDF walioteuliwa juzi tu lazima vichwani mwao wana framework organization wanayoifikiria

Tukumbuke hata Mama alishatamka kuwa ni vema wajeshi wakajikita kwenye majukumu yao. Japo naona kuna makanali wawili kawabakiza.

Ni kweli kuna wanaotumbuliwa kwasababu ya kuboronga lakini mtu mwingine huondolewa sababu Mamlaka inataka kufanya kazi na mtu mwingine.
 
Kafulila sio fair kabisa labda wale wa escrow wamemchongea au wadau wa michomoko walifanya Dua za kisukuma
 
Mbona walioachwa wengi wangeweza kupiga kazi( wanajeshi na vijana)?

Wamekwama wapi?
 
Kafulila sio fair kabisa labda wale wa escrow wamemchongea au wadau wa michomoko walifanya Dua za kisukuma
 
Anahitajika makuu ya JWTZ, kumbuka kuna Majenerali wamestaafu na wengine wametuliwa ubalozi na wengine wamepandiashwa vyeo hivyo wanaenda kuziba nafasi.
Hapa sikubaliani na wewe eti anahitajika Makao Makuu ya Jw. Kauli ni Moja tu kuwa hawahitajiki tena kwenye ukuu wa mikoa, hivyo hata wakifika huko jeshini na kupewa nafasi au hata kupandishwa vyeo sio sababu kwamba walihitajika.

Mbona wapo wengi tu huko jeshini ambao ni Smart na wana qualification za maana zaidi kuliko hao. Kwamba jeshi halina watu hadi liwahitaji hao.

Hebu tuacheni hii tabia ya kupaka mafuta kwa chupa. Je, Ali Hapi, Kafulila na wengine wamehitajika wapi.
 
Brig. Gen. Mbuge alitolewa jeshini kwa muda na kupelekwa kuwa RC Kagera na baada ya teuzi za CDF na Mnadhimu sasa anarejea tena jeshini
Wabongo kwakuremba maneno. Eti alitolewa kwa Muda na sasahivi baada ya uteuzi wa CDF mpya anarudi jeshini.
 
Mtaka very brightly, tatizo nafasi za kuteua ni za kiutashi sio ubora ndio maana siku hizi hata akina mchopanga wachekeshaji wanateuliwa that is nonsense.
Ni katika dunia ya tatu ndio utakuta vitu kama hivyo !! Teuzi za fadhila na bakshish !!
 
Tatizo la hawataki mwenzao awe maarufu kuliko mwing8ne bila Kupepesa Mh Mtaka ni level ya uwaziri kabisaa sema kwaajili ya kuongea sana anaonekana kama anajijenga binafsi kapekwa njombe akapigwe ubaridi kidogo siasa sii hasa
Hata Uwaziri Mkuu anafaa huyu jamaa!
 
aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara (Alitokeaga Kagera) mbona simuoni kwenye orodha?
 
Back
Top Bottom