Binafsi ninavoona sio suala la kutumbuliwa bali ni kila utawala huwa una aina ya Mkao wake inaotaka iwe. Ndio maana Kila Rais anapochaguliwa ni mara chache sana akaendelea na wateule aliowakuta.Wametumbuliwa bhana, siyo kwamba wanahitajika jeshini. Kwa uspesho gani wali nao ??
Wamevurunda warudi wakabebe magobore huko jeshini walikotoka. Usianze kuwapamba hapa.
Na sio kwa Rais tu ila hata wakuu wapya wa taasisi wanapoteuliwa hupenda kuwa na team yao. Nadhani hata IGP na CDF walioteuliwa juzi tu lazima vichwani mwao wana framework organization wanayoifikiria
Tukumbuke hata Mama alishatamka kuwa ni vema wajeshi wakajikita kwenye majukumu yao. Japo naona kuna makanali wawili kawabakiza.
Ni kweli kuna wanaotumbuliwa kwasababu ya kuboronga lakini mtu mwingine huondolewa sababu Mamlaka inataka kufanya kazi na mtu mwingine.