Hii ngouma ukitazama between lines ni NASABA ya walio wahi kuongoza manake wanaendelea kwa vizazi vyao, kidogo kuna mix lakini kama mtego hili watakao baki ni majina yale yale. Ukizama zaidi ni ngumu sana kupata maajabu katika maendeleo kwa mfumo huu.
Miaka mingine hamsini haitatosha kuleta maendeleo sababu weledi, uzoefu na records za accomplishment sio vigezo vya kupata viongozi na watendaji. Technical know who bado inachukua 80 katika 80:20 rule, tutegemee kuhudumiwa na warasimu, viongozi wasio sikia, wala rushwa, kodi, tozo zisizo na kichwa wala miguu kuendelea tena.
Wangetaka ushauri tungewaambia:
Mfumo wote wanaotumia kupata watendaji na viongozi umefeli kuleta maendeleo ya haraka, wajifunze taasisi, kampuni yalitafuta skills yamekuwa haraka sana kuliko wao. Ukiangalia Azam, CRDB, NMB na wengine miaka 30 nyuma hawakuwa hawa wa leo, ukiitazama serikali na changamoto zake kwa miaka 30 bado ziko pale pale. Wenyewe hawajui tatizo lakini hili la teuzi ndio tatizo lao kubwa kuliko hayo mengine.
Ndio mana unakuta mkurugenzi anatuma wagambo na madalali wakakamate gari zinazopakia na kushusha mizigo Ubungo, Huku Tanroads wao wanachukua pesa za parking za gari hizo hizo. God Bless hii nchi na tunamuachia mwenyezi aamue kile atakacho ona kinatufaa leo, manake hili jeshi ni kwa ajili ya chaguzi zijazo na matokeo wala hayahitaji ramli.