Sasa sijui tutaanza anzaje "kuzinduka" mkuu 'macho_mdiliko'?Mkuu watanzania huwa tunashangaza. Hatujui hasa tatizo letu ni nini. Na tukiambiwa mara kesho tumelisahau. Bila wananchi wote kuzinduka na kuliondoa tatizo hakuna namna. Nchi inazidi kudidimia.
Ni dhahiri kabisa kuwa kama nchi, tunatatizo kubwa katika eneo hili; kufanyike kitu/jambo gani kitakachostua kutoka kwenye hali hii mbovu?
Naona kama elimu pekee haisaidii kitu, maana mtu anaweza kudai kabisa na akasikilizwa kwamba siku hizi tunao watu wengi ndani ya nchi hii walioelimika kuliko nyakati zozote baada ya kujipatia uhuru wetu. Lakini ukiangalia tabia za watu utadhani ni nafuu ya wale waliokuwepo wakati tunajipatia uhuru wetu!
Ni nini kisichokuwepo miongoni mwetu?