Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang

Eti amefupisha aendeele tu kula raha dunian kipi cha maana amekifuata huku na watu karibibia 700 huko

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Nakumbuka tetemeko la ardhi kule Kagera yule mwovu alisema siyo yeye wala serikali yake walioleta tetemeko hilo hivyo serikali haiwezi kugharamia hata senti tano. Hakika mtu yule alikuwa mwovu kuliko uovu wenyewe.
 
Hakuna la maana amefanya huko
Ila nyie watu mnamatatizo sana.hivi sijui kama mnakumbuka mwendazake hata zile hela za watu wanaochangia kusaidia wahanga kule bukoba alizichukua na mwisho aliwaambie kama tetemeko limebomoa na nyie tetemekeni mjenge..!!

Sasa mtu anaonyesha utu wake, bado mnasema mnavyojua nyie.
 
Haraka iwezekanavyo ndio vipi. Huyu arejee mara moja sio kuendelea kuwepo dubai kitu wala sio tija kwa nchi. Tuna gesi mafuta na makaa ya mawe matajiri wanakuja na mpango kuacha hizo nishati ili wakuuzieni magari ya umeme. Juzi tu wamesusa nishati za mafuta na gesi ya urusi wamerejea kwenye umeme wa nuclea wakati tuliambiwa ni hatari. Kwenye hiyo mikutano kuna mambo tunapelekeshwa sijui samia wala ana uwezo kuwakilisha maslahi ya nchi au ni kufungwa tela tu na mabeberu
...Arudi nyumbani haraka bhana.
 
Mhe. Rais Akatisha Safari yake ya Nje ya Nchi kwaajili tyuu ya Watanzania Waishio Manyara waliopata Janga la Mafuliko huko Manyara.

#2025 ni Samia Suluhu Hassan tena
#2025 Mimi na Kijiji Changu Tutakulipa Samia.
#2025 Tumepata Suluhuhisho na Samia
 
Hoja za watanzania wengi za kumpenda au kumchukia mtu hazina mashiko
 
Hujamsikia waziri mkuu au
Katika watu ambao.imani yangu imeshuka katika kutoa taarifa sensitive za serikali ni huyu..
Amedangany mara nyingi sana Sidhani kama atasema kitu ntakiamini hata akisema hii ni jf inabdi nipate uhakika..

Na huenda yeye angekaa kimya nisingekuwa na Doubt kubwa ila yeye kuongea ndo kinachoongeza wasiwasi zaidi tukumbuke Magu
 
Ni kweli Rais wetu Mpendwa kafanya jambo zuri kwa wanachi wake.


ACHA KUPIGA KAMPENI DOGO, MUDA BADO!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mhe. Rais Akatisha Safari yake ya Nje ya Nchi kwaajili tyuu ya Watanzania Waishio Manyara waliopata Janga la Mafuliko huko Manyara.

#2025 ni Samia Suluhu Hassan tena
#2025 Mimi na Kijiji Changu Tutakulipa Samia.
#2025 Tumepata Suluhuhisho na Samia
Uko Sawa kichwani kweli? Yaani wenzako wapo kwenye maafa wewe unaleta kampeni za 2025. Nadhani kwa chapisho hili ni definition ya ujinga inayojitosheleza kwako
 
Mhe. Rais Akatisha Safari yake ya Nje ya Nchi kwaajili tyuu ya Watanzania Waishio Manyara waliopata Janga la Mafuliko huko Manyara.

#2025 ni Samia Suluhu Hassan tena
#2025 Mimi na Kijiji Changu Tutakulipa Samia.
#2025 Tumepata Suluhuhisho na Samia
Nje ya maada kidogo...Mkuu wewe ni Ke?
Maana huo mwandiko wa "tyuu" wanaandika wadada wakimaanisha "tu"
Sasa kidume ukiandika hivyo nakuwa na mashaka au we ni mjomba?[emoji39]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…