Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Samia anakula mlo mmoja na waislam wenzake na kila kitu kinaishia hapo. Vipi marehemu JPM aliyeamua kuijenga Chato ili iweze kuwa mkoa kabisa?.
Hiyo michakato ya kuibadili Chato kuwa ya kisasa zaidi, haikuhusisha matumizi ya mabilioni ya pesa yasiyoweza kuhojiwa?.
Kila awamu kuanzia ya kwanza kabisa inao upigaji wa aina fulani kwa msingi wa madaraka makubwa ya Rais anayekuwa ikulu. Nguvu za Rais ni kubwa sana.
Wapo watakaokuja na wazo la kuibadili katiba ili nguvu za Rais ziweze kupunguzwa. Ni hoja ya kina yenye kuhitaji mjadala mpana wa kitaifa lakini itakutana na pingamizi kutoka kwa hawa hawa wanaofaidika na nguvu nyingi za Rais kwani zinawatajirisha wao na jamaa zao.